Klabu ya Yanga imefanikisha kutetea kikombe cha ligi kuu ya NBC msimu huu wa 2023/2024 baada ya kuibuka na ubigwa wa kombe hilo kwa mara ya nne mfululizo huku azam na simba wakichuana kwa ajili ya nafasi ya pili.

Kabla ya kurejea kwenye swali nikutajie vitu viwili ambavyo vimemfanya Yanga kuwa bingwa msimu huu kwanza ni kushinda mechi nyingi dhidi ya vilabu vidogo kwa magoli mengi lakini pia kuwa na idadi ya wachezaji wengi kwenye kikosi wenye uwezo takribani unaoshabihiana kitu kilicho punguza madhara ya majeraha.

Hizi ndio sababu ninazohitaji kuziongelea ambazo nani yuko tayari kuzifanya msimu ujao wa NBC ambaye atakuwa tayari basi ndio bingwa wa ligi hiyo.

Hakikisha unakusanya point nyingi dhidi ya vilabu vidogo Simba na Azam wameshindwa kufanya hivyo wamegawana points na vilabu vingi na muda mwingine kuviachia vilabu hivo point zote tatu hili lilikuwa kosa la kwanza.

Kikosi cha Azam na Simba nikikuuliza leo Chama amekosekana nani atakuwa mbadala sahihi wa Chama ambaye ataweza kutoa walau asilimia 70% ya anachokitoa Chama vipi Feisal kwa Azam wakimkosa wanaweza bado wakashinda michezo.

Kwa Yanga jibu ni ndio wamemkosa Aziz ki, Pacome, Aucho, Lomalisa, Yao katika nyakati tofauti ila walikuwa na mbadala wa wachezaji hao hivo haikuwapa changamoto Yanga.

Kwa point hizo mbili Simba na Azam inabidi wahakikishe walau kila namba ina mbadala wa mchezaji husika endapo akiumia sio Tanzania tu hata ulaya mara nyingi Liverpool ameshindwa kubeba kombe mbele ya Man City sababu ya ufinyu wa kikosi.

Yanga wata drop baadhi ya wachezaji kuelekea msimu ujao , Simba na Azam pia je sajili za kufidia wachezaji hao zitawashirikisha makocha na zitakuwa sahihi kutokana na kocha husika?

Najua kwa mpira wa tanzania ni ngumu sana kocha kushiriki kwa asilimia 100% katika usajili ila kuna faida hizi kama kocha atakuwa sehemu ya maamuzi kwanza kujua mfumo halisi wakuendana na kikosi chake pia na matumizi mazuri ya mchezaji husika sababu kupitia mkono wake ndio usajili umetokea.

Kwa Azam sina hoja juu ya swala la kocha ila kwa simba je watabaki na juma au kuna mbadala wa juma kama upo utakuja mda gani ili upate nafasi ya kufahamiana na wachezaji na kutengeneza aina yake ya uchezaji kutokana na timu ni mada ndefu sana kwenye mambo ya kimbinu naimani tutaiongelea siku nyingine kwa sasa tuyashike hayo .

Kwa ufupi tu Azam na Simba wakifanya haya msimu ujao watawapa Yanga changamoto zaidi kwanza kushinda mechi dhidi ya timu ndogo lakini pia kuwa na upana wa kikosi bila kusahau kushiriki kwa kocha wakati wa usajili angalau 60%.

SOMA ZAIDI: Je Yusuph Kagoma Ni Mbadala Sahihi Wa Khalid Aucho Yanga?

3 Comments

  1. Mimi naona kama team ya simba watakuwa na mbadala wa kocha wangefanya mapema ili kocha ajipange yeye mwenyewe nime semea simba kwasababu simba ndio tunaongoza kwa kubadili makocha

  2. Pingback: Dodoma Jiji vs Simba Sc Vita Ya Nafasi Ya Pili Makao Makuu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version