Ilipoishia “Kama Maisha yangu yatakoma leo Ikulu, Sande uje kufanya hii  kazi kuliokoa Taifa mara moja” Alisema Zola kisha chozi  lilimtoka, akakata simu hiyo. Visa vya baadhi ya Askari  kupotea vilikuwa vingi katika Taifa hilo, Zola baada ya Masaa  mawili alikuwa akikaguliwa kwa ajili ya kuingia Ikulu,  ilikuwa ni mara ya kwanza Zola kuitwa na Rais huyo, si Rais  huyu Pekee bali Zola hakupata kujulikana na Rais yeyote  aliyepita, hii ilimpa shaka sana Zola kwanini Rais ampigie  simu wakati ambao alikuwa akimbana yule Askari amwambie  ukweli kuwa Nani anafanya Mauwaji yale.  Endelea 

SEHEMU YA SABA 

Upande wa Sande Olise, Chozi la Zola lilimkumbusha mbali sana  wakati huo Zola alipokuwa akiogopa kwenda kufanya mafunzo  hayo ya Ujasusi na Upelelezi Nchini Mexico, mafunzo hayo  yaliambatana na Mafunzo ya Ukomando, Sande ndiye  aliyemshawishi Zola kuingia huko laiti kama asingelimshawishi  basi Zola angekuwa Askari wa kawaida kabisa, Mafunzo haya  hufanywa siri sana, kitengo cha siri cha Mzee Dawson ndicho  kilichokuwa kikifanya uchaguzi wa nani aende na Nani asiende  hivyo Dawson alificha sana majina ya Askari wake wa siri  ambao ndio alikuwa akiwatumia kwenye majukumu mazito ambayo  Serikali ilimpa, haraka akafungua Kabati lake lililo chumbani  kwake akaitoa simu ya Siri ambayo ilitumika kwa ajili ya  Mawasiliano yao ya Kiaskari, akampigia Mzee Dawson. 

Mzee Dawson ( Google ) aliposikia sauti ya Sande alijuwa  kulikuwa na tatizo, akameza funda zito la Mate, sauti hiyo  hakuisikia kwa miaka mingi sana. Licha ya kuwa ni Mmoja wa  vijana wake wa Kitengo lakini Sande alikuwa Botswana kwa  miaka mingi mno, alipojitambulisha ndio Mzee Dawson akapata  kujihakikishia zaidi 

“Sande! Bado unanikumbuka?” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaa  wasiwasi sana huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio, mara  nyingi hakuwa akipokea simu za siri sababu yeye ndiye  aliyekuwa akiratibu kazi za Kijasusi hivyo yeye ndiye  aliyekuwa Mpigaji mara zote kutafuta vijana wake, leo  alitafutwa yeye na Sande!! 

“Naam! Mkuu wa Kitengo, Mimi ni P045! Simu ya dharura, narudi  Nchini kwa kazi maalum, nahitaji Baraka zako!!” Ilikuwa ni  sauti iliyojaa uzalendo na ujasiri wa hali ya juu uliombatana 

  

na Utii sababu licha ya Mzee Dawson kuwa Mkubwa kiumri bado  alikuwa ni Askari mwenye Cheo kikubwa sana! Alikuwa ni kama  Baba yao mzazi kwenye kazi za Kijasusi. 

“Zola amewasiliana na wewe?” Aliuliza Dawson 

“Ndio, yupo hatarini. Maisha yake yapo mikononi mwa Rais  Zagamba, narudi kumkomboa” Alisema Sande 

“Uuuupss!!” 

“Ndio Mkuu! Kwasasa Mkuu wa Nchi anawinda maisha ya Zola, ni  ngumu kujuwa kama atatoka salama sababu yupo njiani anaenda  Ikulu ameitwa na Rais” Kauli hii ilimpa mshituko Mkubwa sana  Mzee Dawson, 

“Tuongee baada ya dakika chache” Alisema Dawson, kisha  alikata simu hiyo. Mara moja kanyanyua simu yake akampigia  Zola ili kuthibitisha alichokisia, Simu ya Zola ilikuwa  imezimwa. 

“Shit!!” Akasema Dawson kisha akatoka nyumbani kwake  akaelekea Ikulu, Sande alikaa kusubiria simu ya Mzee Dawson!! 

Alipofika Ikulu, Dawson alikaguliwa kabla ya kuruhusiwa, moja  kwa moja akaelekea ofisini kwa Rais, akamsimamia Rais na  kumpigia Saluti kisha akaketi kwa heshima 

“Dawson!! Kwanini umekuja kama Mkimbizi kutoka Somalia?”  Alihoji kwa dhihaka huku akiwa anaandika kitu 

Dawson alimtazama Rais Jacob Zagamba huku akili yake  ikipingana na mawazo yake juu ya kuuliza kuhusu Inspekta  Zola, hakutaka ijulikane kuwa Zola ni Askari wake wa siri wa  Kitengo 

“Nimekuja tuongee kuhusu Hii kesi” 

“Umefikia wapi Dawson?” 

“Bado uchunguzi unaendelea lakini nimefikia mahali pazuri  sana na siku si nyingi nitakupa mrejesho kuhusu Kundi la  Mafia Gang” Alisema Dawson huku macho yake yakionesha kuwa  sicho kilichompeleka pale. 

“Dawson nahitaji hili jambo ulimalize ndio maana nikalileta  katika Meza yako, ninachotaka kusikia siku moja ni kuwa  umeuwa Wahusika wote na kuileta miili hapa, hao Watu  hawatakiwi kuishi kabisa” Alisema Rais na kumpa maswali  Dawson, kwanini Rais atake Watu hao Wauawe?

“Nitawakamata kisha watahukumiwa kufungwa kifungo cha Maisha,  hiyo ni ahadi yangu kwako Mkuu” Rais akamtazama Dawson kwa  hasira kisha akagonga meza 

“Nimesema nahitaji Miili yao, fyeka kundi hilo haramu na  mazalia yake hapa Nchini, Dawson narudia tena nahitaji miili  yao, hawana kesi ya kujibu….hili jambo linapaswa kufanywa  siri, kinachotakiwa ni kuwa Watu hao wakifa basi vifo  vitakoma, hakuna atakayeuliza wako wapi, haya ni maagizo  yangu” Alisistiza Rais, muda huo akaingia Jamaa mmoja mweusi  aliyepanda Hewani, alionekana kuwa ni Usalama wa Taifa, Rais  akamuuliza Mtu huyo 

“Safari inaanza?” 

“Ndio Mkuu” Alijibu kwa Utii, kisha Rais akachukua funguo ya  gari akampatia jamaa huyo, Dawson hakuelewa kilichoendelea  pale japo hakujuwa Zola yupo wapi. 

Baada ya jamaa huyo kuondoka Dawson akaaga ili aweze kuondoka 

Alipofika karibu na Lango kuu la Ikulu alikutana na walinzi  wawili ambao ni dhahiri walikuwa wakimsubiria yeye ili wamtoe  nje, alipowafikia walimpa ishara kuwa wao walikuwa  wanamsubiria, Dawson akatupa macho yake huku na kule, Milango  mingi ilikuwa imefungwa, walinzi hao ambao walivalia suti  nyeusi waliongozana na macho makali ya Dawson ili kujuwa  alikuwa akiangalia nini, basi wakampa tena ishara kuwa  aongozane nao, wakati anatoka pale mlangoni macho yake  yalitupa uangavu kuelekea kwenye maegesho ya Magari ya Ikulu,  ndipo alipomuona Jamaa aliyetoka kuzungumza na Rais akiwa  amebeba begi kubwa lililomzidi uzito, Dawson alijikuta  akiingiwa na shahuku ya kutaka Kujuwa jamaa huyo alikuwa  akifanya safari gani. Akawageukia walinzi akawaambia 

“Asanteni! Nitafika” Alikuwa na nia ya kuwatoroka ili afanye  upelelezi wake sababu bado kichwa chake kilikuwa kinalia  alamu kuwa Zola yupo matatizoni, 

“Ni wajibu wetu kukufikisha lilipo gari lako” Alisema mmoja  wa walinzi hao tena akiwa anatabasamu, walimjuwa vyema Dawson  kuwa ni mmoja wa Askari waliotegemewa sana na Kila Rais  aliyepita, alikuwa na cheo kikubwa mno, pale pale Zola  akapata akili, akakohoa na kutoa damu kitu ambacho  kiliwashtua wale Walinzi wakiamini anaumwa, ni kweli Dawson  alikuwa anaumwa mapafu yake kutokana na uvutaji wa sigara ila  hapa aliamuwa kucheza na akili za Walinzi hao ili awatoroke,  taharuki ikazuka pale huku mmoja akijaribu kuita gari ya  wagonjwa

“Msijali nahitaji Kitambaa” Alisema Zola kwa sauti yenye  kikohozi, Walinzi hawakuwa na kitambaa, mmoja akatoka kwenda  kuchukua tishu ili imsaidie Dawson, ulikuwa mtego. Haraka  Dawson akajikunjua na kumpiga ngumi kali sehemu ya shingo na  kufanikisha kumzimisha pale pale, akamburuza hadi maegesho ya  magari yaliyo karibu, Wakati huo yule Jamaa akiwa analipakiza  lile begi ndani ya buti. 

Akamficha mlinzi yule kwenye maegesho, akaingia kwenye gari  yake na taratibu akaanza kulifuata gari hilo ambalo lilikuwa  likianza kutoka taratibu kuelekea getini, Naam!! Dawson  aliliangalia gari hilo kwa taswira yenye mashaka sana huku  akitilia mashaka lile begi, hakuacha hata hatua moja alikaa  nyuma ya gari hilo lililokuwa likiingia barabara kuu  iliyokuwa ikitoka Mjini, Gari hiyo ilibadilisha uelekeo na  kuelekea eneo la Bahari ambako ni nadra sana kuona Magari  yakiongoza huko, Dawson alisogea kwa spidi sawa na gari hilo  kisha mbele aliona gari hilo likiwa limesimama kando ya Miti  ya Mikoko, Dawson akalipita gari hilo makusudi ili  kumuaminisha jamaa huyo kuwa yupo peke yake. 

Alipofika mbele Dawson alisimama kisha akashuka ndani ya gari  akawa anarudi Taratibu liliposimama gari lile alilokuwa  akilifuatilia, walikuwa mbali zaidi ya Kilomita 15 kutoka  Ikulu, eneo hilo gari chache sana zilikuwa zikipita. Yule  jamaa akafungua buti na kulitoa begi kisha akalitelekeza eneo  lile, Dawson alikuwa amejificha mahali, jamaa alipoondoka  Dawson alisogea na kulifungua. 

Alijikuta akianguka kwa Mshituko huku macho yake yakishindwa  kuamini alichokiona ndani ya begi hilo, chozi lilianza  kumbubujika Dawson, aliuwona mwili wa Inspketa Zola ukiwa  ndani ya begi hilo, Dawson alijikuta akiwa amepoteza mmoja wa  Maaskari wake wa siri ndani ya Kitengo hicho, alilia kwa  uchungu sana! Maisha ya Inspekta Zola yalikuwa yametamatishwa  ndani ya Ikulu, mwili wake ulikuwa na vidonda na matundu ya  risasi, Dawson akalifunga begi hilo kisha akalivuta hadi  kwenye gari yake akaliweka kwenye buti akaondoka na mwili  huo. 

Akiwa barabarani alionekana kuwa na hofu, nyuma yake kulikuwa  na lile gari lililotoka Ikulu lilikuwa likimfuatilia kwa  nyuma, Dawson aligundua hilo haraka akafanya ujanja ili  kulipoteza lakini gari hilo lilikuwa bado nyuma ya Dawson kwa  zaidi ya kilometa 35 kutoka usawa wa Bahari ambako aliuokota  mwili huo ndani ya begi, Dawson alichofanya ni kutembea kwa  mwendo wa kawaida ili apambane na Mtu aliye ndani ya gari  hilo baada ya kuhisi kuwa hakukuwa na usalama wa Maisha yake,  alisogea kwa umbali ndipo akaona kuna uzio wa Polisi waliokuwa wakifanya msako barabarani, Dawson akagundua kuwa  kuna mchezo umechezwa ili yeye apotee, haraka akabadilisha  uelekeo na kuingia Barabara ya pili ambayo ilikuwa ya vumbi  kisha akaenda kutoka barabara nyingine, muda huo gari lile  lilikuwa nyuma yake. 

Dawson alikuwa na sifa kubwa juu ya ujuzi wa kuendesha  magari, sifa ambayo Zola aliwahi kuishuhudia siku moja  alipotembelewa na Dawson, Naam! Akaongeza spidi kwa haraka  akachomoka kama ndege ya kivita, alifanya hivi makusudi ili  kulipoteza gari lile lililotoka Ikulu, dakika chache alikuwa  amesha lipoteza, akasogea hadi karibu na jengo moja chakavu  sana, Dawson aliona sasa Maisha yake yanaweza kuingia dosari,  aliona kuna kila dalili kuwa Rais alikuwa na lengo la  kumpoteza baada ya kufanikisha kumfyeka Zola pale Ikulu, japo  alikuwa Mzee lakini nyakati hizi mbaya alijitahidi kulibeba  begi lenye mwili wa Zola akapanda nalo juu ya jengo hilo la  ghorofa ambalo lilikuwa halijaisha. 

Hadi anafika juu alikuwa hoi, akajikuta akianguka chini kisha  akatoa simu yake yenye mkonga kutoka katika mfuko wake  akapiga mahali. 

“Sande! Zola ameuawa Ikulu muda mchache uliopita” Alisema  Dawson huku akijifuta jasho, jioni ilikuwa ikiingia 

“Unasemaje?” Ilisikika sauti ya Sande upande wa pili 

“Ndio hivyo, mwili wa Zola nipo nao hapa lakini hata Maisha  yangu yapo hatarini, huyu Rais ni Mtu hatari kuliko  inavyodhaniwa” Ilikuwa ni sauti iliyotoka kikomavu sana,  Ghafla akasikia mchakacho, Dawson akakimbilia sehemu yenye  uwazi kwa ajili ya kuchungulia chini, akaliona lile gari  jeusi lililotoka Ikulu, ni wazi kuwa Rais alituma Mtu kwa  ajili ya kumfuatilia Zola 

“Mkuu mbona Kimya?” Aliuliza Sande Olise baada ya kuona  ukimya umetawala 

“Nacheza sarafu ya Kifo Sande!” Akakata simu mara moja baada  ya kuwa ameshamuelekeza Sande, mara moja akatafuta sehemu ya  kujificha, begi lile lilikuwa katikati ya chumba kimoja. 

Hakuwa Mtu mmoja bali walikuwa wawili wakiwa ndani ya suti  nyeusi, mmoja akiwa amevalia miwani nyeusi na mwingine akiwa  na macho makavu sana, sura zao zilimtambulisha Dawson kuwa  Watu hao walitoka Kitengo cha Usalama wa Taifa Ikulu, Dawson  alishazoea Maisha ya kuwindana akavuta pumzi zake mara moja  kisha akajikunja mithiri ya nyani Mzee huku Mgongo wake ukiwa umevunjika vilivyo, masikio ya Dawson yalikuwa makini sana  kusikiliza hatua za Wataalam hao ambao wazi walikuwa na  mafunzo maalum na walijuwa wanamtafuta Mtu wa namna gani,  jinsi walivyokuwa wakipishana huku wakilindana ilimfanya  Dawson afunge kiwambo cha kuzuia sauti ya Risasi kusikika. 

Hata kabla Dawson hajafyatua Risasi, alisikia mlio wa gari ya  polisi, kisha hatua za jamaa wale kukimbia zilisikika, Haraka  Dawson akaenda kuchungulia akawaona jamaa hao jinsi  walivyokuwa wakidanda kushuka chini kama nyani, akashusha  pumzi zake kisha akili ya kujuwa afanye nini ili polisi  wasiukute mwili wa Zola ilimjia, kando yake kulikuwa na  dirisha lililokuwa na mabomba mawili yaliyoshuka hadi chini,  akajivuta haraka akalibeba begi na kuteleza nalo hadi chini  kisha akajificha nyuma ya kichaka kwa umakini zaidi sababu  alijuwa maadui zake walikuwa eneo hilo, akanyata huku akiwa  amelibeba begi akakatiza mtaro wa maji machafu akaenda  kutokezea Barabarani akasimamisha Bajaji na kutokomea zake,  Jamaa wale walipofika hawakujuwa Dawson aliondoka vipi pale,  mmoja akavuta simu na kupiga mahali 

“Mkuu!! Dawson ameyeyuka” Alisema kwa utii huku mkono wake  uliobeba simu ukiwa na misuli na Glove! 

“Mnamjuwa huyo Mtu vizuri, hakikisheni hachomoki” Ilikuwa ni  sauti ya Rais Zagamba ikisikika katika sikio la Jamaa huyo 

“Sawa Mkuu!” Aliitikia kisha alikata simu. 

MSAKO GIZANI 

Malaika, Six na John Brain baada ya kuona imekuwa ngumu kwao  kumpata Mtu wao ambaye walihangaika Nchi nzima katika vituo  vyote vya polisi bila mafanikio, waliuwa Maafisa wengi wa  polisi ili kumtisha Rais aamuru kuachiwa kwa Mtu wao  ilishindikana. John Brain akaja na Mpango wa kutaka kusambaza  Ugonjwa hatari wa Ebola, Kabla ya kuanza kwa mpango huo John  Brain alimpigia simu Rais ili kumtaka amuache Mtu wao haraka  sana. 

Kilichowafanya Mafia Gang kuendelea kuwepo Nchini ni Mtu wao  ambaye alikamatwa, kesi iliyokuwa ikimkabili Mtu huyo ilikuwa  ni kesi ya Mauwaji ya Makam wa Rais. Muda huo Rais alikuwa  nyumbani kwake Ikulu akitafakari nini cha kufanya baada ya  kumkosa Dawson ambaye sasa alikuwa ameshaupata mwili wa Zola  na kwa vyovyote Dawson atakuwa ameifahamu siri ya Mauwaji  yanayoendelea kutokea, mezani alikuwa na kikombe kidogo cha Kahawa ambacho kilikuwa kikitoka mvuke kuashiria kuwa Kahawa  ilikuwa ya moto sana. 

Simu ilipoita ilikuwa imemzindua kutoka Mawazoni, akaangalia  ni nani aliyekuwa akipiga akaona ni John Brain. Akalamba  midomo yake kabla ya kupokea huku akiwa anaelekea Chooni. 

“Kazi yako imeshaisha, tumekutoa katika kesi ya wizi na  ufisadi ambayo ushaidi alikuwa nao Makam wa Rais,  kilichobakia kilikuwa ni kutupa Pesa zetu lakini cha ajabu  unamshikilia Mtu wetu hadi hivi leo, tumekupa taarifa kupitia  vifo vingi tulivyovisababisha lakini inaonekana hujataka  kuelewa” 

“Brain! Tukae mezani tulizungumze hilo” 

“Michezo ya kitoto isiwepo tafadhali, kama utashindwa  kukubaliana na sisi basi tutahakikisha unang’oka madarakani”  Alisema John Brain 

“Usijali Brain, hakuna kitakacho haribika” Rais alipotoka  Chooni alisimama kando ya mlango, Mlinzi wake alisogea na  kumuuliza kama yupo sawa! 

“Hakikisheni Dawson anauawa haraka iwezekanavyo” Yalikuwa  ndio maagizo pekee aliyoyatoa Rais kisha akarudi ofisini  kwake. 

Mzee Dawson, akiwa ndani ya Bajaji alitafakari mambo mengi  aliyoyafanya na Rais huyo, jinsi alivyotumika kwa ajili ya  Taifa, hakuwahi kufikiria kama Rais angelikuwa ndiye tatizo.  Alijikuta chozi likimdondoka baada ya kulitazama begi hilo  ambalo lilikuwa na mwili wa mmoja wa Askari wake wa siri  sana, akapiga simu sehemu kisha akatoa maagizo fulani ya siri  ambayo ni lazima uwe kwenye mfumo wake ili uweze kuelewa,  hata dereva bajaji aliachwa njia panda, kisha akageuza na  kumpigia simu Sande Olise. 

“Sande ni lazima urejee Haraka sana” Alisema Dawson kisha  alikata simu bila kusikiliza jibu la Sande Olise 

“Hapo kunja kushoto! Ukiona kibao cha kanisa simama”  Alielekeza Dawson, mara moja Bajaji lilifuata maagizo kisha  likasimama. 

“Pesa yako hii hapa” Dawson alitoa noti ya Elfu kumi na  kumpatia dereva kisha akamwambia 

“Chenji itakusaidia”

“Asante sana Kaka!!” Dereva alisema kisha akaondoka zake,  Dawson alikuwa amesimama mbele ya geti la kanisa hilo. Wakaja  Vijana wawili ambao walikuwa wamevalia nguo za kitawa  wakalibeba begi hilo huku Dawson akiwa anatokwa na machozi,  akawafuata huku vijana hao wakionekana kujuwa nini cha  kufanya. 

Walitembea na kuingia kanisani, wakasogea hadi kwenye  maegesho ya magari, wakaweka begi chini kisha, mmoja akaingia  kwenye gari moja iliyokuwa hapo maegesho, akalisogeza mbele  kidogo alafu akashuka, Kijana aliyebakia akafunua kitambaa  cheusi ambacho kilikuwa chakavu sana, pakaonekana kuwa na  andaki fulani, akafungua mlango mdogo uliokuwa na hadhi ya  mlango wa kisima cha maji, pakaonekana kuwa na ngazi ya  kushuka chini, kisha mmoja akaingia na begi hilo huko chini,  mwingine akafuatia kisha Dawson akamalizia, walipofanikiwa  kuingia humo, akaja Mwanamke mmoja ambaye naye alikuwa  amevalia nguo za Kitawa kisha akafunga ule mlango, akaweka  kile kitambaa chakavu na kusali, alipomaliza akaingia kwenye  gari na kulirudisha pale lilipokuwa mwanzo, huwezi kugundua  kuwa kulikuwa na watu waliozama Ardhini. 

Walipofika chini, waliwasha taa ndani ya andaki hilo ambalo  Mzee Dawson alikuwa akilitumia kwa ajili ya kazi zake za  siri, vijana hao walikuwa ni wanafunzi wake. Mmoja aliitwa  Chande na mwingine Kisko, walikuwa ni vijana ambao alitumia  gharama zake Binfsi kuwasomesha na kuwapeleka mafunzoni  Nchini Korea, walijiingiza Katika kanisa hilo ili waweze  kufanya kazi na Mzee Dawson. 

Andaki hilo lilichimbwa muda mrefu kabla ya Mzee Dawson  kufadhili ujenzi wa kanisa hilo. Ilikuwa ni siri kubwa sana  na Watu wengi hawakujua kama kanisani kulikuwa na andaki  lililotumika kufanyia kazi za Kijeshi, Mwanamke aliyekuja  kuziba pale juu alikuwa ni miongoni mwa Watoto ambao  walipoteza Wazazi wao kutokana na visa mbali mbali,  aliwachukua na kuwafundisha kazi za Kijeshi, Mwanamke yule  aliitwa Jesca. Huyo ndiyo Mzee Dawson. 

Huzuni ilikuwa imetanda ndani ya andaki hilo, Chande na kisko  walimpa pole Dwson kwa kumpoteza rafiki yake Kipenzi na  Askari wake wa Siri aliyefanya naye kazi kwa muda mrefu, Zola  alijulikana kama Polisi wa kawaida lakini nje alikuwa ni  komando mwenye mafunzo ya Kijeshi na kijasusi. 

Saa ya Dawson ilikuwa ikilia kushiria kuwa eneo hilo lilikuwa  kimya sana, Chande akaenda kufungua mlango mmoja ambao  ulionekana kufungwa muda mrefu sana, wakaingia huko wakiwa na  begi, ndani ya chumba hicho kulikuwa na Makaburi matatu lakini kulikuwa na mashimo mengine mawili ambayo yalionekana  kuchimbwa muda mrefu 

Dawson akatoa amri ya kufunguliwa kwa begi hilo, hata akina  Chande walijawa na maumivu ndani ya mioyo yao, Zola alikuwa  amekufa, wakamzika kwemye moja ya mashimo yale lakini  lilikuwa limebakia shimo moja, Kisko akauliza 

“Mkuu Mashimo manne yamepokea Watu, bado moja. Kwanini  ulichimba matano?” Dawson alicheka kwa maumivu kisha akamjibu  Kisko 

“Marafiki hukaa pamoja, hawa ni marafiki zangu pekee  niliokuwa nawategemea katika Maisha yangu, wote wameniacha,  hilo shimo moja ni kaburi langu mwenyewe” Chande na Kisko  walimtazama Mzee Dawson kwa jicho lililojaa huzuni sana kisha  akawaambia 

“Muda wangu ukifika mtanifukia hapo kisha mtaharibu kila kitu  hapa, hamtaishi tena kanisani, mtakuwa huru kuyatumikia  Maisha yenu, mna muda mchache sana wa kuendelea kuwa pmoja na  Mimi, nifuateni” Dawson alikaza sura yake kisha akaelekea  mahali huku vijana wake wakimfuata huko. 

Akafika mahali akasimama akawaambia 

“Mwisho wa mtawala katili umefika, nawapa kazi ya kumfuta  haraka sana” 

“Mtawala gani huyo?” Dawson akafunua Shuka sehemu ambako  kulikonekana kuwa na mitambo mingi sana, akawasha Projekta  kisha akawaonesha picha ya Rais wa Nchi 

Vijana wake wakashtuka sana sababu Kwa muda mrefu Dawson  alikuwa pamoja na Rais huyo, Chande akauliza 

“Tumfute Mkuu wa Nchi?” 

“Hafai kupewa hicho cheo, yeye ndiye chanzo cha Mauwaji  yanayoendeelea kutokea hapa Nchini, anapaswa kulipa kwa damu  alizomwaga, anapaswa kulipa kwa Kifo cha Zola, kama sio Ujuzi  wangu basi nami ningekufa kama Zola” Wakashusha Pumzi zao  kisha mmoja akauliza 

“Tutaweza vipi kumfuta Mtu mwenye Ulinzi mkali, Mtu ambaye  anaishi Ikulu, Mtu mwenye jeshi?” 

“Yupo atakayewasaidia” 

“Nani huyo?”

“Anaitwa SANDE OLISE” 

“Ndio Nani huyo?” 

“Nalazimika kuvunja kanuni nilizowawekea, sikuruhusu Ma  Ajenti kufahamiana lakini imenibidi, huyo ni P045 Olise” 

“Familia inaungana” Alisema Kisko kisha wakampa saluti  Dawson, aliwatengeneza vijana wake kujuwa kuwa Ajenti wake ni  Familia yao. 

Jioni ya siku hiyo, katika Ukumbi wa Maktaba maarufu ya  vitabu iliyopo katikati ya Jiji, Rais alikutana na John Brain  kwa ajili ya mazungumzo, walitazamana kwa sura mbili huku  kila mmoja akiwa na silaha inayomlinda, John Brain alikuwa  ameongozana na Malaika wakati huo Six akiwa kwenye moja ya  majengo akiwa ameweka Ulinzi kwa kutumbia Bunduki, alikuwa na  sifa nzuri sana ya Ulengaji wa shabaha kitu ambacho kilikuwa  kikimpa sifa na Umaarufu Mkubwa kwa John Brain, taa nyekundu  iliyoashiria kuwa Rais alikuwa akilengwa na Bunduki iligonga  kwenye kifua, huku John Brain akiwa ana tabasamu, walinzi wa  Rais walipogundua hilo wakataka kuingia kazini lakini Rais  aliwazuia sababu alihitaji zaidi kuzungumza na John Brain. 

Akaamuru Walinzi wake watoke nje kisha Kamwambia John Brain 

“Haina haja ya kuwindana, sisi ni marafiki John, bado  nahitaji kufanya kazi na nyie” Alisema Rais kisha akatoa  picha kutoka katika mfuko wake wa koti jeusi lililomshika  vizuri, 

“Huyo anaitwa Dawson! Ni mmoja wa Askari wa kutumainiwa zaidi  hapa Nchini, nahitaji mumpoteze sababu kuendelea kuishi ni  sawa na Kuyaweka Maisha yangu rehani” Akasema Rais, John  Brain akaivuta picha hiyo 

“Namjuwa huyu nimewahi kumuona” Akasema Malaika kisha wote  wakamtazama 

“Kama siyo huyu basi Zola alikuwa anakufa kwa mikono yangu” 

“Hata hivyo Zola ameshakufa, aliyebakia ni huyo Mtu,  anahitajika kumfuata Zola alipo haraka iwezekanavyo”  Aliongeza Rais kisha picha ya Dawson ikarejeshwa mikononi  mwake 

“Malipo kwanza kisha umuachie Mtu wangu ndipo kazi yako  itafanyika, vinginevyo Nchi yako itatangaza Mlipuko wa  Ugonjwa wa Ebola ndani ya wiki moja, Raia Watakufa kama Kuku, utakuwa ndio mwisho wa utawala wako” Akasema John Brain akiwa  amemtumbulia macho Rais  Comments zikiwa 100 naachia ya 8 leoleo

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx 

42 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version