IlipoishiaKama siyo huyu basi Zola alikuwa anakufa kwa mikono yangu” 

“Hata hivyo Zola ameshakufa, aliyebakia ni huyo Mtu,  anahitajika kumfuata Zola alipo haraka iwezekanavyo”  Aliongeza Rais kisha picha ya Dawson ikarejeshwa mikononi  mwake 

“Malipo kwanza kisha umuachie Mtu wangu ndipo kazi yako  itafanyika, vinginevyo Nchi yako itatangaza Mlipuko wa  Ugonjwa wa Ebola ndani ya wiki moja, Raia Watakufa kama Kuku, utakuwa ndio mwisho wa utawala wako” Akasema John Brain akiwa  amemtumbulia macho Rais . Endelea 

SEHEMU YA NANE

Rais akamuita mmoja wa walinzi wake ambaye alikuja na  Brifkesi yenye pesa 

“Haya ni malipo ya kazi ya Kwanza ya kumuuwa Makam wa Rais na  nyingine ni kwa ajili ya kazi mpya, nawaahidi kumuachia Mtu  wenu endapo mtakamilisha kazi yangu sababu yupo hai” Alisema  Rais kisha John akamtazama Rais kwa umakini sana 

“Kumbuka kauli yako na utekeleze kwa vitendo, ukitugeuka tena  hatutokuwa na muda wa mazungumzo, tutaacha simanzi ambayo  itasababisha maandamano Nchi nzima, utaondolewa kinguvu  madarakani kama mwenzako wa Moroco” Tayari, John na Malaika  walikuwa wamesimama kwa ajili ya kuondoka 

“Ndani ya masaa 48 nisikie habari njema John Brain,  nakuamini” Ilikuwa ni sauti ya Rais kisha John na Malaika  wakaondoka pale. 

Siku iliyofuta Usiku wa saa nne, Ndani ya Uwanja wa ndege wa  Kimataifa, Sande Olise alikuwa akitua Nchini kwa maelekezo  maalum ya Mzee Dawson, kifo cha rafiki yake kilimuuzunisha  sana Sande, alijuwa kutua kwake ndani ya Nchi hii kunaweza  kuweka Maisha yake katika hatari sababu aliwajuwa Vizuri  Mafia Gang na kiongozi wao John Brain, akajuwa hatakiwi  kumuamini Mtu kirahisi, siku hiyo Baridi kali lilikuwa  limezingira Uwanja huo wa ndege, Sande akiwa ndani ya Koti  akaona ni bora aanze safari ya kuelekea mahali ambapo  alielekezwa na Dawson kuwa watakutana. 

“Nipeleke Kanisa la Nabii Eira” Alisema Sande akiwa tayari  ameingia ndani ya taksi hiyo yenye rangi nyeupe, mara moja  safari ilianza. Sande alipata wasaa wa kuangalia uzuri wa taa  za barabarani, alifarijika sana kurudi katika Ardhi ambayo  aliitoroka kwa muda mrefu sana, hakuwa na ndugu na hakujuwa  chochote kuhusu ndugu, ilikuwa ni kawaida kwa Askari wa siri  wa Dawson kwani wengi wao walitokea kwenye vituo vya kulelea  Watoto Yatima, sio yeye tu hata Zola hakuwahi kujuwa asili  yake ilikuwa wapi 

“Unaonekana hukuwepo hapa kwa muda mrefu hadi umesahau kuwa  kipindi hiki ni kipindi cha Baridi” Alisema dereva Taksi,  Sande alikuwa nyuma ya gari hilo lenye siti nne 

“Ndio lakini haina maana kuwa nimesahau kila kitu, siwezi  kusahau mnara wa wapigania uhuru wa Nchi hii” Walijikuta  wakianza kuzunguma huku safari ikiwa inaendelea.

“Pengine kitambulisho chako ndio kitu kingine ambacho unaweza  kukisahau” Alisema Dereva yule kisha alimpatia Sande  kitambulisho kilichomtambulisha kuwa ni Askari maalum, 

“Umekitoa wapi?” Akauliza Sande kwa sauti iliyojaa Mshangao  mkubwa 

“Wakati ulipokuja ulikidondosha nikakiokota” Sande  akamshukuru yule dereva wa teksi, walipofika kanisani Sande  alimshukuru tena yule dereva 

“Usijali ndugu yangu” Alisema yule dereva kisha akaondoka  zake, pale wakaja akina Chande na Kisko, wakampokea mabegi  Sande na kumpeleka kwneye andaki. Wakati wao wanazama kwemye  andaki yule dereva wa Teksi hakuondoka bali alishuhudia  wakiingia kanisani akiwa amejificha mahali, akachukua simu  yake kisha akamtumia Ujumbe mfupi John Brain, alikuwa ni  miongoni mwa Watu wa siri wa John Brain ambao kazi yao  ilikuwa ni kuchunguza Maafisa ambao wataingia Nchini. 

Basi, Sande alipofika Chini ya andaki alifurahi sana kumuona  Dawson ambaye hawakuonana kwa kipindi kirefu sana, ilikuwa ni  faraja kwake lakini alipoliona kaburi la Zola alitokwa na  machozi. 

“Wote waliohusika na kifo chake hawastahili kuishi,  wanastahili kilicho halali yao” Akasema Sande akiwa anapiga  magoti kwenye kaburi hilo, wakati anapiga magoti akajikuta  amedondosha kile kitambulisho alichopewa na dereva teksi kwa  madai kuwa alikiangusha, alipokitazama vizuri akaja kugundua  kuwa kilikuwa bandia, akaanza kujipapasa haraka pale bila  mafanikio kisha akamwambia Dawson ambaye alikuwa amemkodolea  macho kuwa 

“Wanajuwa kuwa nipo hapa Nchini, wamebadilisha kitambulisho  changu” Alisema Sande 

“Shiti!! Nilitaka uwe Ajenti wa Siri ili tufanikishe mipango  yetu” 

“Na kama yule dereva ndiye alicheza huu mchezo basi amegundua  mahala hapa na kwa vyovyote watakuja kututafuta” Ukimya  ulitawala huku kila mmoja akiwa amezama kwenye tafakari,  ilionesha ni jinsi gani John Brain alikuwa na mtandao mkubwa  sana anapoingia Nchi yeyote ile ndio maana kazi zake zilikuwa  zikifanikiwa mara zote. 

Ndani ya dakika kumi na tano yule dereva alikuwa amewasiliana  na John Brain na kumpa taarifa kuhusu ujio wa Sande Olise, moja kwa moja John aliona ndio wakati sahihi wa kuuwa ndege  wawili kwa wakati mmoja, alikuwa akimfahamu vizuri Sande  sababu alikuwa na data zote zilizohusu Usalama wa Nchi,  aliwajuwa Maafisa wengi hasa huyu Sande ambaye alipata  umaarufu katika Operesheni Upepo. 

Taarifa ikawafikia Malaika na Six ambao walipewa kazi hiyo,  walitakiwa kuwauwa wote wawili ili waweze kumkomboa jamaal  ambaye alikuwa ndani ya Magereza Ikulu, Usiku huo Six na  Malaika walijiandaa kupambana na Mzee Dawson na Sande Olise  kwa maelekezo maalum yaliyotolewa na Rais. 

Kibaridi kilichokuwa kikipiga kilifanya Watu wengi waingie  majumbani mapema, ulikuwa ni wakati mzuri kwa Six na Malaika  kulivamia kanisa la Nabii Eira, hawakuwa na siri ya andaki  lililo katika maegesho ya Magari, humo ndimo Mzee Dawson,  Sande na Vijana wake wawili walikuwa wakifikiria nini cha  kufanya ili kuokoa uhai wao baada ya kugundua kuwa Sande  Olise alikuwa akipelelezwa na dereva Taksi tokea Uwanja wa  ndege akitokea Botswana. 

Ndani ya nusu saa, gari nyeusi aina ya Toyota V8 ilikuwa  ikisogea karibu na Kanisa hilo ambalo lilikuwa na ukuta wa  mawe, pembezoni mwa Kanisa hilo kulikuwa na mawe makubwa  ambayo yalifanya kanisa. Liwe na muonekano wa kuvutia sana.  Gari lao walilisimamisha mbali kidogo ili kutoruhusu akili ya  Kijasusi ya Mtu yeyote kugundua kuwa kuna damu iliyokuwa  ikienda kumwagika mahali hapo, Six akapanda juu ya jiwe moja  kubwa wakati huo Malaika akijipenyeza kuingia ndani. 

Kazi ya Six ilikuwa ni kuhakikisha Malaika anaingia kanisani  na kutoka akiwa salama, alikuwa mlenga shabaha mzuri sana  ambaye John Brain alikuwa akiliimba jina lake kila mahali,  Giza kwa upande wa nje lilikuwa limekithirika vya kutosha,  haikuwa rahisi kutambua kuwa eneo hilo la kanisa lilikuwa  limevamiwa na Manyambisi wawili waliokuwa kama mapacha vile.  Baada ya kuwa Six amemaliza kujiweka sawa, akaweka jicho lake  katika Kiwambo kish kampa ishara Malaika asogee akiwa na  Bastola. 

Wakati Malaika alipokuwa akisogea, Jesca yule Kijana wa  Dawson ambaye alipandikizwa pale kanisani ili kulinda andaki,  alihisi jambo lisilo la kawaida akiwa anamtazama Malaika  aliyekuwa akitembea kwa maringo sana akiwa ndani ya suruali  nyeusi na Tisheti jeupe, Jesca akiwa anaendelea kumshangaa  Malaika…..Kule kwenye andaki…. 

Mzee Dawson na Vijana wake walikuwa wakipandisha ngazi,  harufu ya hatari ilikuwa imenuswa vyema sana.

“Wewe ni nani?” Aliuliza Jesca akiwa ndani ya mavazi ya  Kitawa, aliuliza akiwa anamsogelea Malaika aliyekuwa  amesimama getini kwa nje 

“Mimi ni Malaika” Alijibu 

“Malaika?” Akauliza kwa mshangao Jesca, alishawahi kulisikia  jina hilo, akajipa muda wa kutaka kumsikiliza Malaika bila  kujuwa kuwa alikuwa kwenye shabaha ya Six aliyekuwa juu ya  jiwe kubwa. 

“Ha!ha! Ndio, Mimi ni Malaika mbona umeshangaa?” Alihoji tena  Malaika akionekana kutafuna Bigijii 

“Una shida gani?” Aliuliza tena Jesca huku mwili wake ukiwa  unajiandaa kufanya tukio pale, alihisi hali isiyo ya kawaida  kila alipozidi kutazamana na Malaika 

“Nani huyo Jesca?” Ilikuwa ni sauti ya Mlinzi ambaye alikuwa  kwenye kijumba kidogo ambacho Jesca alitokea, mara nyingi  Jesca alikuwa akiutumia muda wa Usiku kulinda mazingira ya  kanisa kitu ambacho Watu wengi walikuwa wakimsifu. 

Mlinzi alikuwa akisogea karibu na Jesca, kisha akaona ishara  ya mkono wa Jesca kwa chini ukimwambia asisogee pale, Mlinzi  akaelewa kisha akasimama pasipo kuendelea kuuliza. 

“Nimekuuliza una shida gani?” Alihoji tena Jesca, laiti kama  angelijuwa basi angelikaa mbali na Mwanamke huyo kwani kama  Zola na ufundi wake wote alishindwa kumdhibiti yeye ataweza? 

“Nimekuja kuchukua roho za Watu wawili, ukiwa mdadisi sana  nitachukua roho za wengi, fungua geti” alisema Malaika huku  ile sura ya kicheko ikipotea, sasa Jesca akajuwa kuwa Malaika  aliyekuwa akimsikia kupitia kwa Mzee Dawson alikuwa mbele  yake, alijuwa ni jinsi gani Malaika alikuwa hatari,  akakumbuka visa vyote alivyovisikia. Kuhusu Malaika.  Akapelekea mkono wake ndani ya sketi yake ili kuchomoa  bastola, kitendo kile kilimfanya Six afyatue risasi kutoka  juu ya lile jiwe, Risasi ikatua kwenye mkono wa Jesca na  nyingine ikatua katika shingo ya Jesca, Milio ya Risasi  iliwafanya Mzee Dawson na Vijana wake kusitisha zoezi la  kutoka kwenye andaki, wakawa wamesimama kwenye ngazi ndani ya  andaki hilo la siri. 

Risasi mbili zilitosha kugeuza jina la Jesca kutoka Mtu hadi  Marehemu, Jesca alikufa pale pale bila hata kumeza mate.  Mlinzi akakimbilia kwenye kibanda chake na kuanza kupuliza  filimbi, akasikia tu mlio wa Risasi, akaona kioo cha dirisha kikiwa kimepasuka alafu akahisi ubaridi kwenye koo lake,  Risasi ya Six ilikuwa ikipita katika shingo ya Mlinzi huyo,  naye alikufa pale pale. 

Haraka Malaika akapanda juu ya geti na kuingia ndani, kisha  akatoa bastola yake akawa anazama kanisani humo, akafungua  lango kuu la kanisa akakuta Waumini wakiwa katika hali ya  hofu sana. 

Bastola ya Malaika ilikuwa mbele, mkono mwingine akiwa  ameshikilia sprei Maalum ambayo ilikuwa imejazwa sumu kali,  akawasogelea kwa tahadhali kubwa sana kisha akawauliza 

“Dawson yupo wapi?” Sauti za vilio ziliendelea kusikika kisha  akazinyamazisha kwa kuwatisha kuwauwa, akapekuwa huku na kule  bila mafanikio ndani ya jengo la Kanisa, alipowakosa  akapuliza ile Sprei kisha akatoka nje haraka na kufunga  mlango, akaendelea na Msako mkali katika nyumba za watawa,  akapuliza ile sumu kila chumba kisha akampigia simu Six na  kumwambia kuwa hakufanikiwa kuwaona Ila amepuliza sumu kila  chumba 

“Hatuna muda wa kuendelea kuwa hapa, tumia sekunde 30  zilizobakia kutoka humo kanisani” Alisema Six, Malaika  akafanya kama alivyoambiwa lakini akiwa anatoka alihisi kama  kuna sehemu ilikuwa ikicheza hivi, akasimama karibu na  maegesho ya Magari, akasogea chini ya uvungu wa gari akafunua  lile shuka akaona kuna mlango mdogo, kwa namna eneo lile  lilivyo, hakutaka kujiaminisha kuwa kilikuwa ni kisima sababu  kilikuwa kimefunikwa kwa shuka alafu kipo chini ya gari,  akataka kufungua ili kutazama ndani ya shimo hilo wakati huo  Mzee Dawson akiwa anachomoa Bastola yake na kujiweka sawa kwa  Majibizano, Malaika akapeleka Mkono ili afungue kusudi aone  kulikuwa na nini mle, Ghafla akasikia king’ora cha polisi,  akachomoka uvunguni kisha akaelekea getini na kuruka,  akakimbilia gari lao liliposimama, wakaingia kwenye gari na  kuondoka, Polisi wakalizingira eneo la kanisa mara moja baada  ya kupigiwa simu kuwa kuna risasi zimesikika kanisani hapo. 

Wakaingia kwa tahadhali ndipo wakakutana na miili miwili ya  Jesca na Mlinzi wa kanisa lile, miili yao ilikuwa na joto kwa  mbali kuonesha kuwa Mauwaji hayo yalitokea muda mchache  uliopita. 

“Hizi ni risasi zilezile, chukueni maiti hizi na wengine  fanyeni msako hapa haraka sana” Ilikuwa ni sauti ya mmoja wa  Askari waliokuja pale kanisani, bado Mtaalam Sande, Mzee  Dawson na vijana wake wakiwa ndani ya Andaki bila kuwa na  taarifa kuwa Jesca alikuwa ameuawa na Six, lilipofunguliwa lango kuu la Kanisa ndipo mshituko na Mshangao mkubwa  ulipowashika polisi hao, walikuta Miili ya watu ikiwa  inatokwa na mvuke kama vile nyama inayochomwa, harufu ya  nyama ilitapakaa kanisa zima wakaagiza zima moto kumwaga Maji  katika kanisa hilo, muda mchache polisi walifanikiwa kuingia  ndani ya kanisa na kukuta Miili mingi ikiwa imeharibika  vibaya sana. 

Taarifa ilizagaa kwa haraka sana juu ya shambulio hilo la  kutisha ambalo lilitumia silaha ya sumu na risasi, Sande  akawashauri akina Mzee Dawson kuwa hawapaswi kutoka kwa  wakati huo hadi polisi watakapo maliza msako wao.

Comments zikiwa 100 naachia ya 9 leoleo

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx 

29 Comments

  1. Simulizi ya 🔥
    Maskini W kwenye Handaki😭😭
    Simulizi ya huzuni yaani kama kweli vile
    Watu wabunifu jamani
    Mtunzi wa Simulizi hii nataka niongee nae Kuna Zawadi yake
    ♥️♥️♥️♥️

Leave A Reply


Exit mobile version