Ilipoishia “Umefikia wapi Sande!” Alihoji Mbaga baada ya kuwasha redio Call
“Nakaribia ila nimeumia eneo la mbavu nilitereza wakati napanda juu ya Bomba, sasa nakaribia ulipo umeme” ilisikika sauti ya Sande Olise ambaye alikuwa Ikulu
“Safi sana! Ongeza mwendo huku hali shwari” akasema kisha akazima redio akaongeza mwendo kuelekea kwenye ghorofa. Endelea
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Sande Upande wake alikuwa akitoka kwenye chemba na mwili ulikuwa ukivuja maji taka, akakumbuka alichoambiwa na Mbaga kuwa hapaswi kupita bila kujifuta maji, akafungua begi kisha akatoa kitambaa akajifuta yale maji ndipo akapita eneo lenye umeme, akapita kwa umakini ili asije sababisha shoti.
Alikuwa ameshachoka baada ya kutembea ndani ya chemba kwa zaidi ya nusu saa huku akiwa na maumivu makali kwenye mbavu zake, alipovuka umeme akajikuta akihitaji kupumzika kwanza kabla ya kuanza kufungua nati zilizo katika dirisha la juu ambalo akishaliondoa basi anakuwa amefika chooni kwa Rais huyo, punde akasikia sauti ya kufunguliwa kwa mlango akasimama na kuchungulia akamuona Mwanaume mmoja mwenye asili ya kiarabu akiwa anachunguza eneo hilo hapana shaka alisikia purukushani,
mwanaume huyo ndiye Jamaal ambaye amekuja pale Ikulu kumlinda Rais, Jamaal alionekana kuwa makini, akasogea hadi lilipo dirisha mahali ambapo Sande Olise alikuwa amesimama, dirisha hilo lilikuwa dogo na lenye Alminium na matundu madogo madogo.
Sande akabonyea kwa chini, Jamaal akaangaza bila kuona chochote kisha ikasikika sauti ya kufunga Mlango, hapana shaka Jamaal alikuwa ameondoka, Sande akajipa likizo fupi ili kutuliza maumivu ya mbavu zake, akaliondoa begi Mgongoni kisha akakaa kwenye bomba!!
Upande wa pili taarifa ya Kifo cha Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa ilianza kuvuja kwa Askari wa juu wa Taifa, wakaitana ili kujadili. Wakati huo, Mwanaume Sande Olise alikuwa akipandisha ngazi kuelekea Ghorofa namba tano,
Ghorofa hilo lilikuwa halitumiki, hakuna aliyeshtuka kuwa eneo hilo liligeuzwa kuwa uwanja wa vita sababu Bunduki zilizotumika zilikuwa na vifaa maalum vya kuzuia sauti,
Malaika alikuwa ameshafika Ghorofa namba tano akamkuta Six akiwa amelala sakafuni damu ikiwa inamtoka, alikuwa hawezi kuzungumza. Muda huo huo Malaika akapiga simu kwa John Brain kumpa taarifa kuwa Six anakaribia kufa
“Nini?” Aliuliza kwa mshituko John Brain
“Hali yake sio nzuri, ameshambuliwa na mlengaji mwenzake ambaye yupo ghorofa lingine!! Hali sio shwari Boss” Alisema kwa sauti ya Chini huku akijuwa fika kuwa mlengaji anaweza kuja pale ili kuhakiki kama Six amekufa, ndicho ambacho Mzee Mbaga alikuwa akifanya.
Akakata simu kisha akaenda kuchungulia dirishani akapokelewa na ukimya uliopitiliza, akajuwa sasa
yupo mawindoni na Mtu asiyemfahamu.
Malaika na kamwili kake kadogo kama Miss Utalii, akachomoa Bastola yake akafunga kifaa maalum cha kuzuia Mlio wa risasi kisha akajiweka sawa!! Akatafuta mahali akajibanza, muda huo Mtaalam Mbaga alikuwa akizidi kusogea juu taratibu.
“SHIT” alisema John Brain akasimama kutoka kitini kisha akampigia simu Jamaal akamuuliza
“Kuna usalama ulipo? Six amepigwa risasi eneo baya sana huenda akafa, unatakiwa kuwahi haraka eneo la tukio” Alisema kwa sauti iliyojaa Kupagawa, kwa jinsi alivyokuwa akimuamini Six hakutegemea kama angelipigwa risasi kirahisi hivyo akajuwa kuwa mlengaji alikuwa Mtu hodari zaidi ya Six
“Natamaani kutoka hapa lakini nina hisia mbaya kuwa huenda ikulu imevamiwa pia, angalia nini cha kufanya Boss” Alisema Jamaal
“Okay!” Kisha simu ikakatika, akamrudia tena Malaika lakini simu ya Malaika haikupokelewa, wakati huo Malaika alikuwa akisikia namna Mtu alivyokuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya chumba hicho.
Moja kwa moja akajuwa Mtu huyo alikuwa ndiye aliyempiga risasi Six, akabana Pumzi zake ili asimpe mwanya wa kujuwa yupo wapi kutokana na ukimya uliokuwa umetawala pale. Mbaga alizidi kusogea bila kujuwa kuwa anayemuwinda naye ameshakaa mkao wa kujibu mapigo, mara nyingi Mzee Mbaga hakupendelea sana kutumia Bastola lakini ilimlazimu kutokana na namna sifa za Mtu anayeenda kupambana naye zilivyo.
Fumba na kufumbua Mbaga na Malaika wakajikuta wakiwa ndani ya chumba kimoja kisicho na vitu ndani yake, Malaika alikuwa amejibanza nyuma ya moja ya kona za chumba hicho huku Mwili wa Six ukiwa bado sakafuni, hakukuwa tena na cha kusubiria kwa Malaika akafyatua risasi ili impate Mbaga eneo la Kichwa, lakini bahati mbaya Bastola yake haikutoa risasi, ilikuwa ni kama Bahati kwa Mbaga akafanikiwa kumuona Malaika, wakati Malaika anahangaika kufyatua risasi Mbaga alishamfikia na kuipiga teke Bastola ya Malaika.
Wakawa wanatazamana kwa macho yaliyojaa ufundi wa kusomana, Malaika alishasikia sifa za Mbaga na Mbaga alikuwa na sifa za Malaika, mviziano baina yao ukawa mkali huku kila Mtu akitafuta namna ya kumdhibiti mwenzake.
Upande wa Ikulu, mapumziko kwa Sande Olise hayakuchukua muda mrefu, akafungua begi akatoa Staa kwa ajili ya kufungua nati ili aweze kuingia kwenye Choo cha Rais bila kujuwa kuwa Jamaal alikuwa ameshtuka. Alizifungua haraka bila kupoteza muda kabisa, ndani ya dakika moja akawa amefanikiwa kisha akatoa dirisha hilo akaliweka pembeni kukawa na tundu ambalo angeliweza kupita na kwenda chooni kwa ajili ya kuanza mpango wake.
Muda huo Rais alikuwa akipewa taarifa ya kifo cha Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa, na kushambuliwa kwa Six. Ilimfanya Rais akose amani akiwa ofisini kwake, akamuita Jamaal
“Usikae mbali na Mimi Jamaal, siwaamini hawa walinzi wengine, tegemeo langu lipo kwako tuu” Alisema huku akiwa anamtazama Jamaal aliyekuwa na ndevu nyingi.
“Nipo hapa Mkuu” akasema Jamaal wakati huo Sande akiwa anachumpa ili aingie chooni, akajikuta akinasa shati lake kwenye tundu hilo ambalo lilikuwa na baadhi ya misumali midogo baada ya kung’oa dirisha. Akajitahidi kujitoa lakini ikawa ngumu, katika purukushani akajikuta ameangukia chooni, mshindo ukamshtua Jamaal. Akamwambia Rais akae hapo pasipo kutoka kisha taratibu akaelekea chumbani kwa Rais.
Jamaal akawa anaelekea taratibu eneo ambalo alisikia mshindo huo, ilikuwa ni kule chooni ambako Sande Olise alikuwa ameangukia, Sande hakutaka sana kupoteza muda licha ya kuumia kidogo wakati alipoanguka, akajiokota haraka ili aanze mpango wa kumpata Rais bila kujuwa kuwa Jamaal alikuwa ameshakaribia mlango wa Choo hicho.
Upande wa pili, Mbaga alikuwa ameangushwa chini, Malaika akionekana kumdhibiti Mbaga kisawasawa, Mbaga akajiokotanisha kisha akamfuata Malaika na kutupa mapigo mawili takatifu, moja lilikuwa ni teke kali ambalo Malaika aliliona na kulikwepa lakini alikuwa ameunganisha na pigo jingine la teke la kushoto ambalo lilimpata Malaika akaanguka chini, bila kupoteza muda akajiokota pembezoni kukiwa na gongo, akalinyanyua ili kupambana na Mbaga, akatoka spidi na kujirusha mithiri ya ndege aina ya Mwewe anavyowinda
vifaranga vya kuku,
kisha akatua chini na kurusha gongo ambalo lilimpata Mbaga eneo la Bega hadi akapepesuka na
kujigonga ukutani, jinsi Mbaga alivyokuwa mwepesi ikawa ngumu kwa Malaika kuusoma umri sahihi wa Mbaga kama ni Mzee au Kijana kwa jinsi ambavyo alikuwa akipambana.
Mbaga akajiweka sawa kwa ajili ya kujibu mapigo kutoka kwa Malaika, akabonyea kidogo na kukaa staili ya nyani Mzee anayetaka kurukia Tawi la Mti, kisha akakunja miguu yake sawasawa huku akiwa anamtazama Malaika ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa mwepesi kutokana na umbo lake dogo na jembamba.
“Nitakuuwa kama nilivyomuuwa mwenzako” Akasema Mbaga ikiwa ni mbinu ya kumtuliza Malaika
Comments ziwe nyingi apa LEO kwa Kaka Mkubwa
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx
26 Comments
🔥🔥🔥
Leo ni fupi sana ndugu admini
Nilitegemea leo itaisha
Mambo yanazidi kuwa safi
Leta mwendelezo maana ni🔥🔥🔥🔥
Hapo ndo hatriii
Leo umetupiga na kitu kizito jamani ni fupi sana
Hatariìi mbagaa ni mzeee kweliii ahahaha
Hatari sana
Ongeza sauti
Daaj leo umetupa fupi san mkuu
Adimini leo fupi sna
Admin admin admin nimekuita mara tatu hatari sana ujengewe Sanam lako kabisa
Nzuri sana ni balaa aisee
Tupe vitu kaka mkubwa
Leo umejuwa kutubania admin
💣💣💣
Duu stor leo fupi jamn
Admin
Daaaaaaah nawaza kwa sande olise…..hv kutakuwa salama kwel.
🥴🥴🥴🤦🏽♂️🤦🏽♂️🤦🏽♂️🤦🏽♂️🤦🏽♂️
Nnigejua ndo fupi hv jmn .mpk nimepata na kikohozi sijui kimetoka wapi jmn mbona fupi hivi Admin Leo umetuweza baba
Mambo ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Jamani mbona fupi ivi
Simulizi tamu ajabu
Kaka MKUBWA ZAWADI YAKO IPO HEWANI INAKUJA
MTUNZI MASHUHURI MBUNIFU SIJAPATA ONA💕💕💕
NIMESOMA VITABU VYA KIINGEREZA ZAIDI YA VITABU 20 ILA SIJAONA MAMBO KAMA HAYA❤️
Umenifanya kupenda kusoma Vitabu vya Kiswahili tangu nianza kusoma Simulizi Nzuri ya Osman na Jacklin…
Admini Nakupenda pia❤️
Daaah nzuri San hii toa mwendlez
Imesisimua sana
Too short
Kaz nzuri sana kak naqubal sanaa