Ilipoishia “Hayo ni majina ya Watu wa siri wa Mzee Dawson, Sande yupo  hai, moja ya kaburi hapo linaweza kuwa kaburi la Zola,  fukueni haraka sana.” Ilisikika sauti ya John Brain, aliamini  Dawson ni Mtu mwenye akili sana kwenye mambo yake. 

Mengine yalionekana kuwa ya zamani sana lakini moja lilikuwa  bado jipya, wakalifukua hilo kwa kutumia chepe iliyo kwenye  kona ya chumba hicho chenye makaburi. Kazi hii ilifanywa na Six aliyekuwa amebana rasta zake kwa nyuma. Jasho lilikuwa  likimtoka, harufu kidogo ilianza kutapakaa pale, haikuwazuia  kufanya kazi yao. Endelea

SEHEMU YA KUMI

“Oooh Shit!” Alisema Six huku akitema mate, Malaika ilimbidi  asogee pale 

“Duuh! Kweli huyu jamaa alipitia mafunzo makubwa sana”  Alisema Malaika, mwili huo ulikuwa umeharibiwa kwa kemikali  maalum ambayo iliwafanya akina Six washindwe kuitambuwa sura  hiyo, wakati wanaendelea kushangaa tukio lile Malaika aliona  kitu kama redio Call hivi kando ya aliposimama tena ikiwa  imefukiwa kidogo, akaifuata na kuiokota akakuta redio hiyo  ikiwa inafanya kazi. 

Haraka Malaika akakimbilia alipoliacha begi lake, akatoa  Laptop na baadhi ya vifaa fulani kisha akavaa Head Phone,  akawasha kitu fulani kutoka katika Laptop yake akaona mawimbi  ya redio hiyo yakiwa yanatoka kando ya Bahari ya Hindi. 

“Umefanikiwa kugundua chochote?” Aliuliza Six akiwa  ameshikilia chepe 

“Eneo ulipo mtambo wa redio hii ni kando ya Bahari ya Hindi  upande wa Mashariki” 

“Inaweza kuwa mhusika wa andaki hili yupo huko, kama ni  Dawson basi arobaini yake imefika” Alisema Six kisha kwa  pamoja wakapanda juu kutoka katika lile andaki wakijiandaa  kufuata mawimbi hayo. Walipotoka wakakutana na waumini  waliokuwa wamesimama nje ya andaki hilo, walionekana  kushangaa 

“Nani amechimba andaki hili hapa?” Aliuliza Malaika huku  akiwa ameshatoa kitambulisho feki walichopewa na Rais ili  waonekane ni Watu wa Usalama wa Taifa. Macho ya watu hao  yalionekana kujawa na woga wakawa wanasakiziana kujibu, mmoja  akasikaka akisema 

“Hatukuwahi kuona wala kuhisi uwepo wa shimo hilo, kwa miaka  mingi nimeishi hapa lakini hili shimo sijawahi kuliona”  Alisema huku akitikisa kichwa chake, alionekana kuwa Mzee  sana mwenye mvi nyeupe zisizo na matunzo 

“Kanisa hili limejengwa lini?” Aliuliza Six 

“Miaka 15 iliyopita”

“Nani alihusika na ujenzi wake?” Six aliuliza tena,  alichotaka kusikia ni jina la Mzee Dawson likitajwa ili wawe  na uhakika wa wanachoenda kufanya 

“Mfadhili alishafariki miaka mitatu baada ya kanisa hili  kukamilika” Alijibu tena yule Mzee ambaye alijibebesha mzigo  wa kujibu maswali ya Six 

Walipoona hawawezi kupata walichokuwa wanakitaka waliondoka  haraka eneo hilo ili kuanza safari ya kuelekea Kando ya  Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, upande huu ndiko ambako  nyumba ya siri ya Marehemu Zola ilijengwa. 

Kitendo cha Six na Malaika kuondoka kilimpa mwanya yule Mzee  akawaacha wenzake wakiendelea kushangaa uwepo wa andaki  kanisani, akaenda nyuma kabisa ya kanisa hilo, alihakikisha  hakuna aliyemuona tena akionekana kuwa mwenye wasiwasi  Mkubwa. 

Akawa anatafuta kitu ardhini kwa kukita mguu wake, alifanya  hivyo kwa dakika kadhaa hadi alipokita mahali aliposikia kama  kuna sauti inamuitikia, ilikuwa ni sauti iliyoashiria uwepo  wa kitu fulani sehemu hiyo, akafukua kwa kutumia mikono yake  sababu eneo hilo lilikuwa limeloa kutokana na maji yaliyokuwa  yakimwagika kutoka katika tanki, akafanikiwa kufukua na kutoa  sanduku la rangi ya fedha, akapanda juu ya ukuta akiwa na  sanduku hilo dogo kisha akatokomea zake pasipo kuonwa na  yeyote yule. 

Turudi kule kwenye Makazi ya siri ya Marehemu Zola, hali ya  kutafakari ilikuwa imechukua nafasi kubwa sana. Dawson hali  yake kiafya haikuwa nzuri hasa baada ya kupata mikiki ya hapa  na pale kwa zaidi ya masaa nane bila kutuliza akili yake,  kifua kilikuwa kikimbana mno huku Kisko akimsaidia baadhi ya  dawa na huduma nyingine 

“Asante Kisko! Natamani sana siku moja niwaone mkitoka katika  Maisha haya ambayo nahisi yanawapa mateso makubwa sana, hamna  uhuru wa kufanya mambo yenu. Nimewalea kwa muda mrefu sana”  Alisema Dawson huku akiangalia saa yake mkononi, kisko  akamuuliza 

“Kwanini unaangalia saa hiyo kila wakati ilhali haioneshi  chochote?” Mzee Dawson akajilazimisha kucheka kidogo 

“Inaonekana kutokufanya kazi ndio lakini Je kama nikikwambia  Hii saa ndiyo Mimi utaamini?” Kisko akacheka kisha akasema

“Hata Mtoto mdogo hawezi kuliamini hilo, Mtu anawezaje kuwa  saa?” 

“Bahati mbaya au nzuri, nyie mna majina yenu. Majina ambayo  mlipewa huko mlipotoka, licha ya kupewa majina ya Kijeshi  lakini hayakuweza kubadili uhalisia kuwa wewe ni Kisko,  wenzako ni Jesca na Chande” Akasema kisha akakohoa na kutoa  damu nzito sana, akapewa maji ya kusukutua 

“Nawaza Jesca atakuwa wapi, ni masaa mengi yamepita bila  kuwasiliana naye. Ulifanya kama nilivyo kwambia?” Alihoji  Dawson 

“Ndio redio Call niliiacha kwenye kile chumba chenye  makaburi” Alijibu Kisko huku akionekana kuwa mwnye kiu ya  kutaka kujuwa mengi 

“Hata wewe pia ni mwenye Bahati kama ni hivyo, una jina lako  halisi Kama Dawson” Dawson akacheka tena kisha akasema 

“Sababu Mimi ni Afsa wa juu katika Nchi hii ni lazima nitumie  jina halisi lakini kuna jambo lililo nyuma ya Pazia, utakuja  kuelewa siku moja endapo Mungu atanijalia uhai mrefu wa  kuishi” Yalikuwa ni maongezi yaliyojaa mafumbo ambayo  hayakumshibisha Kisko, Muda huo Chande alikuwa kwenye chumba  kimoja na Sande Olise wakiwa wanazungumza 

“Tunasubiria nini?” Aliuliza Chande akiwa anamtazama Sande  Olise aliyekuwa ameegesha nwili wake kwenye moja ya kioo na  kujipa fursa ya kutazama chini ya jengo hilo la kifahari 

“Hatuwezi kukurupuka! Tupo mawindoni Chande, kosa dogo  unaadhibiwa kifo. Nchi inatutambua kama waasi kutoka masaa  machache ya kujulikana kama Wazalendo wenye kulipigania  Taifa, Dunia wakati mwingine inaweza isikupe maana halisi ya  Binadamu” 

“Ha!ha!ha!” Alicheka Chande, muda huo Kisko alikuja mbio na  kuwaambia 

“Mzee Dawson hali yake ni mbaya sana” Taarifa ikazua taharuki  pale, wote wakaelekea chumbani kwa Dawson! Wakamkuta akiwa  ana pumua kwa shida sana. 

“Inabidi tumsaidie!” Alisema Chande akionekana kuwa na wenge  la kutosha 

“Tulia!! Hatuwezi kufanya hivyo kwa sasa, hatuwezi  kuhatarisha Maisha yetu kirahisi hivyo!!” Alisema Sande kisha  alimgeukia Dawson

“Yupo sahihi! Rais anajuwa Mimi naumwa kwa muda mrefu  simalizagi wiki mbili kabla ya kupelekwa JNI Hospital kwa  matibabu ya ugonjwa wangu sababu wao ndio speshelist wa  tatizo hili, huu ni mtego mtakamatwa wote. Ni bora mniache  nife nyie mbaki kuwa hai” Alisema Dawson kwa sauti iliyojaa  maumivu mno 

“Baba usiseme hivyo unayo nafasi ya kuendelea kuishi, sema  unataka nifanye nini Baba” Chande alisema kwa uchungu huku  macho yake yakibubujika chozi laini lililolowesha mashavu  yake madogo, Mzee Dawson kwao alikuwa ndiye Baba yao sababu  aliwatoa kwenye kituo cha kulea Watoto yatima miaka mingi,  akawapeleka mafunzoni, wakapata mafunzo ya kijeshi na  kijasusi 

“Chande anayejuwa mwisho wangu atawapa tumaini endapo  atanichukua” Alisema Dawson huku hali yake ikizidi kuwa  mbaya!! Sande Olise akahisi jambo, haraka akaelekea kwenye  kioo kutazama chini akaona gari nyeusi ikiwa imesimama nje ya  uzio wa jumba hilo la siri, walikuwa ni Malaika na Six ambao  walikuwa wakifuatilia mawimbi ya Redio Call kutoka kanisani  hadi Ufukweni, kifaa chao kiliwaambia kuwa walikuwa wamefika  eneo husika. 

“Kuwa makini!” Alisema Six kisha akampatia Bastola Malaika.  Sande akarudi kwenye kile chumba akawapa taarifa kuwa Kuna  hali ya hatari wanapaswa kuokoa Maisha yao haraka  iwezekanavyo, muda huo Mzee Dawson alikuwa katika hali mbaya  ya kuumwa. 

Ndani ya msitu mmoja ulio kando na Jiji hili, alionekana Mtu  mmoja Mzee Akikimbia, mkononi alikuwa ameshikilia sanduku  lenye kutu, alikuwa ni yule Mzee aliyefukua Sanduku kule  kanisani. Alikuwa amechoka baada ya kukimbia kwa muda mrefu,  mikono yake ilikuwa ikitetemeka. Akaingiza mkono mfunoni  akatoa funguo kisha akasimma chini ya Mti mmoja mkubwa,  akalifungua sanduku hilo. 

Ndani ya sanduku kulikuwa na kifaa kimoja kilichoonekana kuwa  cha zamani sana, akakiangalia kisha chozi likawa linamtoka.  Akabonyeza kitufe cha kuwasha, kikawaka. 

Kifaa kile kilikuwa kimeunganishwa na vifaa vinne ambavyo  vilikuwa kwa Watu wanne, Mtu wa kwanza kupata ishara alikuwa  ni John Brain, Mtu wa pili ni Mzee Dawson, wa tatu ni Malaika  na Wanne ni Six ambaye alikuwa akitembea kuelekea kwenye  jengo lingine kama kawaida yake kutafuta eneo zuri la kulenga  shabaha, kitendo cha kuwashwa kile kifaa na yule Mzee kule  msituni kilimfanya Six aanguke na kuhisi baridi kali sana, vivo hivyo kwa Malaika ambaye alikuwa ameshafika kwenye geti  la kuingia katika jumba la siri ambalo Mzee Dawson na vijana  wake walikuwemo, kwa Mzee Dawson iliwaka ile saa ambayo Kisko  alimuuliza Dawson kwanini alikuwa akiiangalia mara kwa mara  lakini wakati inawaka Mzee Dawson alikuwa ameshapoteza Fahamu  zake, wote walishangaa kuona saa ya Dawson imewaka ghafla na  kutoa mwanga wa kijani, katika saa hiyo kulikuwa na kitu kama  ramani iliyokuwa ikizunguka ndani yake. 

John Brain alishtuka sana baada kupata ishara kutoka katika  moja ya saa yake ndogo ambayo mara nyingi alikuwa akitembea  nayo, saa hiyo ilikuwa ikifanana sana na saa aliyokuwa  akiivaa Mzee Dawson! Akasimama na kutabasamu kisha akajikuta  mwenye furaha isiyo kifani. 

“Baada ya miaka mingi hatimaye umeonekana, niliweka Maisha  yangu rehani kwa muda mrefu kukutafuta” Alisema John Brain. 

Muda huo yule Mzee ambaye hakujulikana ni nani na ametokea  wapi, alichukua kifaa kingine ndani ya sanduku, kifaa ambacho  kilikuwa kama simu hivi kisha akapiga mahali. Simu iliita  ndani ya Ikulu, ilikuwa ni katika ofisi ya Rais 

“Mimi ni P55 Mbaga” ilikuwa ni sauti komavu kutoka kwa Mzee  huyo, Rais alishtuka sana kusikia jina hilo yaani P55 Mbaga,  akakata simu haraka sana baada ya kusikia hivyo kisha  akanyanyua simu kumpigia John Brain ambaye alikuwa katika  hali ya furaha sana 

“Mimi ni mfu John!!” Alisema Rais kwa sauti iliyoonesha  alikuwa kwenye butwaaa 

“Kivipi?” Alihoji Brain 

“P55 Mbaga amejitokeza!!” 

“Imarisha ulinzi haraka, Naingia kazini kupambana naye”  Alisema John huku tabasamu likiwa limeimarika katika sura  yake. 

Muda huo yule Mzee ambaye ni P55 Mbaga alikuwa akitoka kule  Msituni na kufunga safari ya kufuata uelekeo wa saa ya Mzee  Dawson, alikuwa na kifaa chake alichokiamini sana, alionekana  kuwa mtaalam wa kifaa hicho, Dakika tano baada ya vifaa  vilivyofungwa katika miili ya Six na Malaika kuwaka,  iliwafanya wabadili maamuzi yao. Mpango ulikuwa ni kuwauwa  Sande na Mzee Dawson, haraka wakaingia kwenye gari na  kuondoka eneo lile, huku maswali yakiwa mengi vichwani mwao.

Yule Mzee alifika hadi eneo la Mashariki ya Bahari ya Hindi,  kifaa kikamwambia kuwa alikuwa amefika eneo ambalo saa hiyo  ilikuwepo, muda huo Mzee Dawson alikuwa akirejea kwenye  fahamu zake!! Alipoamka alishangaa kuona saa yake imewaka,  akashtuka kisha akauliza 

“Imeweka saa ngapi?” Aliwatumbulia macho vijana wake ambao  walikuwa wamesimama mbele yake, alikuwepo Kisko na Chande 

“Nusu saa iliyopita” alijibu Chande huku akimtazama Mzee  Dawson aliyekuwa kitandani 

“Na Sande yupo wapi?” 

“Nafikiri yupo kwenye korido, unamuhitaji?” 

“Hapana!! Nipe Maji ya kunywa” Alisema tena Mzee Dawson kisha  alikohoa na kutoa damu. 

“Baba kwanini hii saa ni muhimu sana kwako umeamka hujali  afya yako unauliza kuhusu saa?” Alihoji Kisko 

“Nilikwambia hii saa ndiyo Maisha yangu, Mimi ni hii saa,  niliisibiria kwa miaka mingi na jambo hili lilibakia kuwa  siri ambayo sina budi kuwaeleza mkiwa pamoja” Muda huo Chande  alirejea akiwa na glasi yenye maji ya vuguvugu ambayo mara  nyingi Mzee Dawson alikuwa akiyatumia. Ghafla, Sande aliingia  chumbani bahati nzuri Dawson alikuwa ameshapata fahamu  akasema 

“Kuna Mtu anakuja upande huu, anaonekana kuwa anafuatilia  jambo maana yupo bize na kitu mkononi, nafikiri ana GPS”  Alisema Sande, Mzee Dawson akanyanyuka na kwenda kuangalia,  alipofika dirishani alimuona Yule Mzee ambaye mara nyingi  alikuwa akishinda kule kanisani akajiuliza alikuwa amefuata  nini pale 

“Unamfahamu?” Aliuliza Sande 

“Ndio….huyu Ni Miongoni mwa Wazee wa kanisa letu, najiuliza  amepajuaje hapa” Akajibu Mzee Dawson huku akionekana kujawa  na mshangao 

“Niachie Mimi” Sande alisema kisha akashusha ngazi kuelekea  chini, akafungua mlango kisha akatoka. Akakutana yule Mzee 

“Wewe ni nani?” Alihoji Sande lakini kwa tahadhari sababu  Mzee huyo alikuwa makini kumtazama Sande na jinsi  alivyomtazama Sande aligundua Mzee huyo alikuwa na macho  makini kuliko maelezo.

Punde ikasikika sauti ya Dawson ikisema 

“Mruhusu aje ndani” alipogeuka alikutana na macho ya Dawson,  Mzee huyo akaruhusiwa kuingia ndani lakini tayari kila mmoja  alikuwa na umakini mno. Tembea ya Mzee huyo bado ilikuwa  makini sana, alionekana kutafuta kitu lakini alipoingia humo  kifaa chake chenye GPS kilizimika sababu nyumba hiyo ilikuwa  maalum kwa ajili ya kazi za kipelelezi hivyo ilikuwa ni ngumu  kwa baadhi ya vifaa kupenyeza. 

Alipewa kiti akakaa kisha akaulizwa 

“Umefikaje hapa?” Aliuliza Mzee Dawson, yule Mzee akawatazama  kisha akasema bila kujibu swali la Dawson 

“Nimekuja kwa ishara yako Dawson, nimetoka mbali, nimesubiri  kwa miaka mingi kukuambia kuwa Dunia ilikuwa ikikutafuta kwa  miaka hiyo, nilikuficha kwa muda mrefu sana” Alisema Mzee  huyo 

“Wewe ni nani hasa?” 

“P55 Mbaga” Alijibu Mzee huyo na kusababisha mshangao kwa  Mzee Dawson ambaye alionekana kulifahamu jambo hilo 

“Haiwezekani, wewe ni Mzee wa kanisa umeijuaje siri hiyo  niliyoificha kwa muda mrefu!” 

“Hukuificha siri hiyo, siri hii inajulikana ila kuwaka kwa  saa hiyo ni ishara kuwa mapambano yanaanza upya! Mapambano ya  kung’oa mizizi ya utawala huu wa Mabavu” 

“Una maana gani?” 

Mzee huyo alisimama kisha akasema 

“Naitwa Mbaga, nilikuwa rafiki mkubwa wa Baba yako japo  alinizidi umri lakini alinipenda sana. Baba yako alikuwa ni  miongoni mwa Askari wa ngazi ya juu, wakati huo, akatoroka na  nyaraka za siri ambazo alianza kuzisambaza kuhusu Urais wa  Nchii namna unavyo rithishwa, uozo na ufedhuli uliokuwa  umejaa serikalini, aliishia kuuawa huku Taifa likiambiwa kuwa  Baba yako alikuwa ni muasi” Alimeza mate kisha akaendelea  Mzee Mbaga 

“Kabla ya kuuawa kwake alinipa kifaa maalum, akaniambia  unatakiwa kuvaa saa mkononi mwako na wakati wa ukombozi  utakapofika mimi nitakuja kukusaidia. Teknolojia hii  iligunduliwa huko Ujerumani, mmoja wa Watu wa siri wa Baba yako walimwambia Rais juu ya Mpango wetu Mimi na Baba yako,  nilitafutwa kila kona bila mafanikio yoyote yale, ndipo Baba  yako akapiga simu ukiwa masomoni ukabadilishwa Ubin wako ili  usitambulike, akakuandaa ukawa Mwanajeshi lakini Alipouawa  ulikuwa bado hujamaliza Mafunzo ya Kijeshi Nchini Cuba, Baada  ya Teknolojia kugundulika wao wakatengeneza ya kwao ili  kujuwa muda na mahala ambapo nitawasha kifaa nilichopewa na  Baba yako kama ishara ya uhuru na ukombozi” Aliendelea kusema  Mzee Mbaga na kuwaacha akina Dawson kinywa wazi 

Machozi yalimtoka Dawson akakumbuka jinsi Mama yake  alivyomwambia mpango huo, kuanzia kipindi hicho aliivaa saa  hiyo katika Maisha yake yote hadi anafikia uzee wa Makamo,  alimkumbatia Mzee Mbaga. Taarifa hii ilikuwa ni ajendaa kuu  kwa kila Rais aliyetokea katika ukoo wa kurithi nafasi ya  Urais, alitafutwa sana Mbaga bila mafanikio na Marais Kadhaa  waliopita. 

Comments ziwe nyingi apa KESHO itoke EPISODE NDEFU YA 11

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx 

  

15 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version