Wakati wa kuandaa mkeka mara nyingi baadhi ya watu hushindwa kuelewa kati ya Over 1.5 na Over 2 na hujikuta wakiweka ubashiri bila ya kuelewa wanachagua kitu gani na ni muhimu sana kujua kuwa wakati wa kuandaa mkeka unatakiwa usikurupuke na kuandaa mkeka wako vyema zaidi.

Leo tutazame tofauti kubwa iliyopo katika mkeka haswa katika odds za Over 1.5 na Over 2 na kwanini ni muhimu kuzingatia zaidi kabla ya kuweka mkeka wako.

Over 1.5 Katika Mkeka

Katika uchaguzi wa option hii wakati wa kuweka ubashiri ni vyema kufahamu kuwa ili ushinde mkeka wako ulioweka kupitia kampuni unayotumia kubashiri inapaswa ulichobetia kiwe na magoli kuanzia mawili katika mchezo husika. Mfano mechi ikiisha 1:1 au 2:0 au 0:2 basi umeshinda kwakua mchezo husika umetoka na goli zaidi ya 1 yaani magoli mawili. Kiasi cha kushinda inategemea na dau ambalo umeweka katika mkeka wako.

Over 2 Katika Mkeka

Kwenye kuandaa mkeka ambao utakua na option ya Over 2 ni kwamba unatakiwa kufahamu kuwa ili uweze kushinda mkeka wako inapaswa mechi uliyowekea dau lako iwe na magoli zaidi ya mawili na ikitokea kuwa yameishia magoli mawili basi mkeka wako utakua haujashinda na kiasi chako ulichowekea mkeka kitarudishwa katika akaunti yako ila ikitokea limepatikana goli moja basi mkeka wako umechanika lakini pia ikitokea yamepatikana magoli matatu basi utakua umeshinda. Mfano ikiwa 3:0 Umeshinda , ikiwa 2:0 pesa zako zitarudishwa katika akaunti yako ikitokea 1:0 mkeka utakua umechanika.

Endelea kujifunza zaidi kuhusu masuala ya UBASHIRI katika michezo mbalimbali kwa kusoma hapa.

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Mkeka wa AFCON 2023 Wenye Odds 90 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version