Mchezo wa mpira wa miguu Tanzania ni moja kati ya kitu ambacho kinapendwa sana na kuunganisha watu wengi kwa wakati mmoja kutoka sehemu mbalimbali na haswa mechi ambazo zinazikutanisha timu kubwa za soka hapa Tanzania.

Ni sehemu pekee ambayo huwa kuna hisia na utani na ushabiki mkubwa zaidi huku ukichangiwa na matukio ambayo hujitokeza viwanjani huku mara nyingi yakiwa ni yale ambayo yanawahusisha waamuzi wa soka nchini kutokana na maamuzi ambayo yamekua yakijitokeza kutoka kwa waamuzi hao.

Wakati nguvu kubwa inatumika ya kumshambulia mwamuzi wa kati Ramadhan Kayoko tukumbuke hata hao wenye mpira wao kuna wakati wanashindwa kutafsiri Sheria 17 za soka. Miaka nenda rudi timu zetu kongwe za Simba na Yanga zimekuwa zikinufaika na hawa hawa waamuzi lakini hakuna hata siku moja siku timu hizo zikipendelea viongozi au mashabiki wake wakatoka mbele na kukemea madudu yao

Nitamkumbuka refalii Heri Sasii ambaye naye alikuwa akihukumiwa kwa kufanya makosa mara kadhaa tena aliwahi kuwapa goli Simba SC mchezo dhidi ya Azam FC na Ngoma ile kwenda sare, sikuwahi kuona mashabiki wakiandamana na kumkataa Sasii.

Nashangazwa na hizi kampeni za kutaka kumkataa Kayoko wakati huyu ndiye mwamuzi ambaye kama Taifa tunamuangalia kwa umakini zaidi kwani tunafahamu kupata watu bora kama wao inakuwa ni ngumu na kuna muda tuache kulazimisha matokeo kama inakuwa siku mbaya kazini tusitengeneze presha kwa watu wengine.

Leo hii kwenye vijiwe vya soka kila mtu ana lake kuhusu Kayoko vipi na hizo timu zingine ambazo zilikuwa zikiangukia pua maamuzi kama hayo nazo zisemejee, tuuwache mpira tusije kutengeneza vurugu kwa kuja na matokeo yetu mfukoni. Kufanya hivyo tutaaribu mpira na kupelekea kunyimwa hata ile nafasi ya kuaandaa michuano ya AFCON 2027.

SOMA ZAIDI: Mzimu wa Mayele Uliomtesa Konkoni Na Sasa Uko Na Guede?

1 Comment

  1. Pingback: JKT Tanzania vs Simba Mchezo Wa Historia Jeshini - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version