Uwekezaji  ni  njia ya  kufanya kitu ama fedha  kuzaa fedha zaidi na zaidi. Ili uwe  mwekezaji unapaswa kuwa  na shughuli inayokuingizia kipato halafu ndipo unaweza  kuwekeza sehemu ya kipato chako ambacho kinaweza kuongeza ulichonacho.

Ili uweze kuwekeza unapaswa kuweka sehemu ya kipato chako kwenye mwendelezo wa uinuaji na malengo yako kwa manufaa ya baaadae. Tunaweza kujifunza kutoka kwa watu tofauti tofauti ambapo waliwekeza sehemu ya  Kipato chao kila mwezi na malengo yao.

Siku moja katika chuo kikuu,kijana mmoja alikuwa akimweleza mkufuzi kuhusu mipango yake ya siku zijazo. Alimwambia ataenda kusoma awe wakili, atasoma digrii ya udaktari lengo lake aziweze kesi ngumu ngumu na awe tajiri. Haya yalikuwa ni malengo kwake

Tumekuwa tukilaumu juu ya mwenendo wa Soka letu  kukosa ubora na kwenda mbali kutaka uwekezaji kwa vijana ni kweli hili la msingi lakini tunajua misingi ya uwekezaju huu?. Ni wachache watakao kwambia uwekezaji upi unatakiwa hii nayo ni taaluma ambayo bila kujua huwezi kufanya,timu zetu zimekosa hili kutokana na usimamizi kutokuwa na nia,ili ufanye hili lazima kwanza uwe na lengo pili nia na tatu vifaa haya yote yamekosekana hapa kwetu.

Unapozungumzia Soka la vijana unalenga usimamizi imara hapa ndipo unapoweza kuona tofauti ya timu B na academic hapa ndipo unaweza kuona tofauti ya vijana wa simba sport, Young Africans,Mtubwa Sugar, na timu nyingine za hapa kwetu na wale wa Barcelona,timu zimekosa mwendelezo wa timu B angali hata academic hakuna. Timu za vijana tunazosema hazina hadhi ya vijana maana zimejaza vijeba na 2/100 ndio wanaweza kuonekana timu za wakubwa japo nao ni over 20.

Kama ilivyolenga maana halisi basi uwekezaji katika Soka ni lazima tuwe na haya,walimu wa kufundisha vijana,viongozi wawe na nia zaidi,kuwe na mahitaji muhimu kwa maana ya viwanja na vifaa vya michezo kiujumla,ili hili lifanikiwe kipato kijitoshereze kwa dhima zima kama ni young players account mfano mfuko wa ukuzaji vijana kimichezo.

Ikiwa tu haya yatafanikiwa ufujaji wa pesa utapungua,usiulize kwa nini Ajax wanakikosi bora tafakari wanafanye kufika huko. Tumekuwa wepesi pia wa kutoa tathimini na ushauri lakini huenda tukawa tunapiga kelele tu bila kujua maana halisi ya kile tunacho zungumzia.

Ndani ya makala hii pia nakuletea mpenzi msomaji wa habari za michezo mantiki zima ya ukuaji wa Soka letu unaposema kutengeneza vipaji au kukuza kwanza tambua dhima zima na maana halisi sasa tutazame namna ya kutengeneza vipaji.

KUTENGENEZA KIPAJI NI NINI NA KUINUA KIPAJI.?

Kutengeneza kipaji katika soka ni kumkuza Mtoto asiejua hata maana ya kupiga pasi, krosi shuti na kuanza kumfundisha moja baada ya moja mpaka kufikia kugeuka na mpira na kupiga chenga. Kwa upande wa kuinua kipaji ni kufanya mwendelezo wa kile alichonacho baada ya kutengeneza.

Kumtumia Mtoto wa umri wa miaka 12,13,14,15,16 mpaka 17 na kuendelea akiwa anajua nini maana ya kupiga pasi,krosi,kugeuka na mpira na mpaka kupiga chenga kutamfanya awe na hali ya kujiamini na kukua hivyo siku zote hata akiwa mkubwa.

Kwa maana hiyo sasa ukifatilia vilabu vyetu havina malengo na watoto wenye umri wa miaka 8,9,10,11,12,13,14 na 15 kuwaandaa ambao hawa unaweza kuwapa msingi wowote wa soka unaoutaka bali tunaanza na watoto wa umri wa miaka 17,18,19 na 20 na kuendelea ambao washapitia kwenye misingi ya kizamani ambayo ya mitaani kwenye hali ngumu sana. Wamepita katika misingi ya kupiga pasi,krosi na chenga wajuavyo wao kutokana na uwezo wao binafsi, katika umri huo ukitazama  kwa walio  endelea kisoka umri huo wa miaka 17 hadi 20 unawakuta wakiwa tayari  wanacheza timu kubwa pamoja na timu ya taifa kwa mafanikio sio kwa kupata uzoefu.

Tuamke watanzania pamoja na shirikisho letu na vilabu vyetu tusitake mafanikio ya haraka ambayo yanazidi kutupotezea muda kumchukua mchezaji wa umri wa miaka 20 nakuendelea aliepitia misingi mibovu ya mpira ndio ukataka umbadilishe na kocha wa kisasa sawa na kumpa mafunzo mbwa aliyechoka.

MAMBO YANAYOTAKIWA ILI KUFANYA HAYA.

Lakini hayo yote yanafanikiwa chini ya miundo bora endelevu timu iwe na kocha mzoefu na mambo muhimu ya mafunzo kama uwanja na mengine. Katika suala zima la makocha kimsingi kuna makocha ambao wanakuwa wamefundishwa kulea vijana tofauti na wale ambao wanafundisha wachezaji wakubwa. Hawa ni makocha ambao ukimpa tu kijana anajua huyu amjenge vipi.

Miundo mbinu hapa unazungumzia vifaa vya mazoezi na uwanja kijumla. Ni vigumu sana kuwa na academic katika misingi ambayo inakosa mambo hayo yote,Unaweza ukawa na kocha lakini kama huna miundo mbinu bora ni kazi bure tu kwani itampa shida kubwa katika kazi yake.

Jambo la mwisho ni kuzingatia kuhusu mlo wa mchezaji kijana,hapa ndipo kuna shida sana tunakosa watu wa kufundisha masuala ya milo kwa wachezaji ili wawe katika uimara mkubwa. Unakuta mchezaji kaumia anachelewa kupona hii inatokana na kukosa mlo wa kufanya yeye aweze kurudi katika uimara wake ipasavyo.

Viongozi wa soka kuweni kama huyo kijana wa chuo kikuu tutafika kwa pamoja na katika furaha daima na kuacha kutumia pesa kwa kupoteza tu. Sina shule ya soka Ipo siku nitaenda darasani kuchukua Elimu ya soka niwaeleze vizuri faida ya academy.

SOMA ZAIDI: Hakuna Simba Na Yanga Bila Msingi Wa Uwepo Wao

4 Comments

  1. Pingback: Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

Leave A Reply


Exit mobile version