Nchini Uingereza Ligi kuu ya nchi hiyo imekuwa maarufu sana duniani kwa sasa na hiyo  inajaziwa na namna Ligi yao ilivyo na ushindani uliyopo ndani yake, lakini jambo kubwa zaidi linalosifika ni kuwa moja ya Ligi kubwa Duniani ambayo imekuwa ikipamba sana wachezaji wake wa ndani yaani wachezaji wazawa wa Kiingereza pale ambapo wanaonyesha ubora hata kama ni chipukizi bila kujali klabu anayocheza.

Ni miaka mingi sasa tumekuwa tukiwalaumu sana wachezaji wetu wazawa, ni muda mwingi tumekuwa tukipambana kuona nafasi za wachezaji wa kigeni kupunguzwa na kuwa nafasi chache kwao kuja kusakata kabumbu nchini na hiyo ni kutokana na kuona ubora wa wazawa kupata nafasi mbele ya wageni ni ngumu jambo ambalo limekuwa na mjadala mkubwa kila iitwapo leo.

Wakati sasa umefika tunapaswa kukubali kuwa wageni wana nafasi kubwa sana ya maendeleo ya mpira wetu kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja. Uwepo wa nafasi nyingi za usajili wa wwachezaji wa kigeni ndiyo Kumbukumbu bora ya mwanzo mzuri wa mafanikio ya vilabu vyetu kwenye Ligi ya Mabingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.

Nani asiyeikumbuka Simba SC iliyofanya vyema ? Kumbukumbu inanikumbusha kuwa hata Yanga SC iliyoingia fainali Shirikisho chache ni wageni.

Jambo ilo limenifanya kutupa jicho langu kama mwewe na kuona kuwa nafasi ya wageni imesaidia sana kupandisha ubora wa Wachezaji wetu wa kizawa kwa kiasi kikubwa sana, wachezaji wetu wengi wamekuwa na vipaji na uwezo mkubwa ila ilikosekana hamasa ya kupambana na ilo kwa sasa ni tofauti.

Wazawa wengi wanapambana hata wale ambao wapo Simba SC na Yanga SC pamoja na Azam FC wamekuwa wakionyesha jitihada na wengine wakiwaweka benchi wageni Mfano halisi unapizungumzia Mohamed Hussein, Pascal Msindo, Lusajo Mwaikenda, Feisal Salum, Mzamiru Yassin, Clement Mzize, Mudathiri Yahya, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Nickson Kibabage, Adolf Mtasigwa na wengine wamekuwa wakiongeza kujituma na kuonyesha ubora wao na kupambania namba na wageni.

Ni msimu wa tatu sasa wazawa wamekuwa wakijituma hata wakiwa kwenye vilabu vya kati hapa nchini unapozungumzia msimu uliyopita kiwango cha wazawa kupambana na kuonyesha ubora wao kiliongezeka na walionekana, unapomzungumzia Najimu Mussa akiwa na Tabora Utd, Waziri Junior, Valentino MASHAKA akiwa na Geita Gold FC, Zabona Mayombya na Tanzania Prisons, Rahim Shomary pamoja na Yona Amos.

Wageni njooni na sisi wenyeji tuwaonyeshe ubora wetu huu ndiyo wakati wa wazawa kuondoa dhana ya kuwa wazawa hawapambani na hawajitumi, yaliyotokea nyuma wakati huu siyo wa kuendelea kutembea nayo ni wakati sasa kuamini wanaweza. Hakuna haja ya idadi ya wageni ipunguzwe hapo hapo panatosha hiyo ndiyo silaha nzuri ya kuongeza ubora wao.

SOMA PIA:  Hii Ndio Sheria Tata Zaidi Kwenye Mpira Wa Miguu

1 Comment

Leave A Reply


Exit mobile version