Meneja wa Barcelona, Xavi Hernandez amemtaka Gavi kubaki na klabu hiyo zaidi ya msimu huu.

Gavi amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Premier League, huku Chelsea ikiaminika kumtaka mchezaji huyo.

Inakisiwa kuwa Mhispania huyo amekerwa na Barca kwa kushindwa kumsajili kama mchezaji wa kikosi cha kwanza mwezi Januari.

Hata hivyo, Xavi amemshauri mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kusalia na wababe hao wa LaLiga.

“Hangekuwa na furaha katika timu nyingine kama alivyo hapa.

“Ni mwanasoka anayenisisimua. Mustakabali wake upo kwa Barca,” Xavi alisema.

Leave A Reply


Exit mobile version