Soka ni mchezo wenye misingi yake ya kiutawala katika taifa hadi kidunia. Soka limekosa majeshi tu na mwisho kuwa kama mataifa mengine yalivyo na kuendeshwa.Katika takwimu iliyopo pale Zurich Uswisi,kuna idadi kubwa ya wanachama wa mashirikisho ya soka kuliko hata wanachama wa umoja waataifa.

Yawezekana ikawa dhahiri shahiri mataifa kama Tuvalu, Micronesia, Visiwa vya Dominic, jamhuri ya sahara Magharibi ikawa sio wanachama wa Umoja wa mataifa. Lakini wakati huo wakawa na uanachama wa FIFA vyema kabisa. Mnaikumbuka Tahiti ile timu ya kutoka kule Oceanic.

Sasa hapa nchini Tanzania kuna maeneo tunakosa umakini na kuamua nini kifanyike. Vilabu vingi duniani vimekuwa na salamu zake kwa mashabiki wake .

Ni Ulaya unakuta klabu ikiwa na utaratibu wa hashtag matata ambayo inakuwa kama salamu kwa klabu yao.GGMU ni kati ya salamu au utambulisho wa klabu.

Ni mshangao mkubwa kuona kiongozi wa klabu ana salimu mashabiki kwa salamu ya chama cha Siasa. Kama klabu wana aina yao ya kuitana na kujinasibu mbele ya mashabiki. Ni ngumu kueleweka kama unakuta kiongozi anasema ” Namungo oyeeeee” au ikawa “Simba oyee” utadhani ni chama cha siasa.

Moja ya salamu ambazo zinaweza kuwa maarufu ni kwa kutumia kauli mbiu kama vile “Simbaaaaaaa”, halafu wapenzi wake wakajibu “Nguvu mojaaa”, hii inaleta hamasa kwa wenye timu zao.

Klabu kama ya Yanga haiwezi kuingia akilini kama kiongozi akataka kuwasalimia mashabiki wake na akaita Yanga oyee oyee. Hizo ni salamu za kisiasa. Tunapojisahaulisha tunakuwa kama vile ni utamaduni kuitana hivyo.

Kiongozi kama Wa Yanga lazima ataita “Yangaaaa”,wananchi wakajibu “Daima mbele nyuma mwiko”. Huo ndo unakuwa mwitikio wa kiuananchi.

Sio kwa Simba tu hata Azam,Mtibwa na timu nyinginezo. Kiitikio cha oyeeeee sio sehemu ya slogan za vilabu vyetu. Ukifika kwa klabu kama ya Biashara United ya Musoma. Klabu inapaswa kuitikia kama wanavyo jinasibu wanajeshi wa mpakani.

Viongozi wa timu zote lazima wajenge utamaduni huo hata vijana ambao wanakuwa wakisikia kaulimbiu hizo wajiulize na kuuliza kwa nini hawa wanasema hivi,wachezaji nao wakisikia viitikio hivyo vya salamu kuna picha ambayo wataijenga katika akili zao na utendaji wao uwanjani.

SOMA PIA : Fahamu Yote Kuhusu Muundo Mpya Wa Ligi Ya Mabingwa Ulaya

1 Comment

  1. Pingback: Ifahamu Timu Ya Kanisa Iliyoizaa Liverpool Baada Ya Muungano Na Everton

Leave A Reply


Exit mobile version