Ni wazi kuwa historia imeandikwa vyema na klabu zetu za Simba na Yanga baada ya timu zote mbili kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa barani Afrika lakini kamwe tusiache kuwapa maua yao wawekezaji wa klabu hizi mbili kwa jinsi wanavyopambana.

Tanzania ndio shirikisho pekee iliyopeleka timu mbili robo fainali klabu bingwa na hii inaonesha kukuwa kwa vilabu vyetu. La pili naona utawala wa timu za kiarabu zinaanza kutokomea kwenye michuano ya bara la Afrika kuanzia zile za timu za Taifa ambapo tuliona katika michuano ya mataifa barani Afrika kwa ngazi ya taifa yakiwa hayajafanya vyema.

Baada ya kuona katika AFCON ni wazi sasa kama timu zetu zikipambana basi tunaona kabisa jambo hili likijirudia katika michuano ya mabingwa ngazi ya klabu kwa bara la Afrika.

Ni timu mbili pekee za kiarabu zilizofanikiwa kutoboa kucheza robo fainali, kwasasa timu ambayo Simba na Yanga hawatamani kukutana nayo ni Mamelod, na kwa nafasi waliokuwa nayo Simba na Yanga ni bahati tu iamue kikombe hiki kikiwaepusha nacho timu hizi za Kariakoo.

Mamelod ndio iliyokamilika kwasasa tofauti na Al Ahly ambayo kwasasa kule mbele imekuwa timu inayokosa umakini kabisa katika kumalizia mipira. Mechi zao zote wamekuwa watengenezaji wa nafasi nyingi ila kuzitumia wanashindwa.

Wananchi na wekundu wa Msimbazi safari zenu za nusu fainali zipo mkononi mwa kikombe cha Mamelod. Atakaye pangwa na Mamelod hiyo baba Jeni baibai. Tukutane kwenye draw ila upande wangu natabiri timu moja ya Tanzania itapewa Mamelod.

SOMA ZAIDI: Simba vs Jwaneng Galaxy Wachezaji Hatari Ni Hawa

1 Comment

  1. Pingback: Kama Ni Ufalme Wa Mbinguni, Chama Ameubeba Wa Duniani - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version