Klabu ya Azam FC ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa chini ya uongozi wa kampuni ya Bakharesa ambapo Azam FC ilianza kushiriki michuano ya bonanza ambayo ilkuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Bakharesa, Azam FC ilikuwa ikishiriki michuano hiyo kwa kupitia wafanyakazi wa kampuni ya Bakharesa na klabu hiyo iliweza kuibuka na ushindi kwa kila mechi waliokuwa wakicheza, Azam ilianza kushiriki ligi daraja la kwanza baada tu ya kuweza kufanikiwa kushiriki michuano ya bonanza na kuweza kufanikiwa kushinda mabonanza hayo yaliyokuwa yakiandaliwa.
Azam FC ilianza kushiriki ligi daraja la kwanza mwaka 2007 na kuweza kufanikiwa kuweza kushiriki ligi kuu bala ya Tanzania (Vodacom Premier League) ambapo waliingia katika ushiriki wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa mwaka 2008/2009 na kuweza kumaliza msimu wa ligi katika nafasi ya tisa (9) katika msimamo wa ligi.
Azam Fc haikushia hapo kwani msimu uliofuata waliweza kufanikiwa kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu kwa mwaka wa 2010/2011. Baada ya kuweza kushika moja ya nafasi za juu Azam Fc ilianza kusajili wachezaji wa kimataifa, ambapo wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa na Azam Fc waliikuwa ni Kipre Cheche na Michael Balou wote hao wakiwa ni raia wa Ivory Coast ambapo walikuja kushiriki michuano ya CECAFA kwa nchi za Afrika mashariki na Kati lakini Ivory Coast walishiriki kama wageni waalikwa katika michuano hiyo na baada ya kumalizika kwa michua hiyo ndipo Azam Fc ilipoona fursa ya kuwasajili wachezaji hao ambao walionesha kiwango kizuri na kuweza kusajiliwa na Azam FC huku ikiwa ndio usajili wa kwanza wa klabu ya Azam kusajili wachezaji wa kimataifa.
Baada ya kuweza kushika moja kati ya nafasi za juu za msimamo wa ligi kuu bala Azam Fc ilweza kumalisha nguvu kubwa katika kikosi chake kwa kutaka kuchukua ubingwa wa ligi kuu bara na hapo ndipo wakamsajili mchezaji Mrisho Ngassa akitokea Yanga SC, lakini bahati haikuwa kwao na waliweza kumaliza ligi wakishika nafasi ya pili kitu ambacho kiliwawezesha kushiriki michuano ya kimataifa ambapo walishiriki michuano ya kombe shirikishi la Afrika kwa mwaka wa 2012/2013, ambapo Azam FC ilweza kutolewa katika mechi yao ya tatu katika hatua ya mzunguko wa kuingia katika makundi.
Mafanikioa ya Azam FC
Klabu ya Azam Fc imekuwa moja ya vilabu vyenye mafanikio makubwa katika soka la Tanzania ikilinganisha na vilabu vya Simba SC na Yanga SC ambavyo ni vilabu vikongwe katika soka la Tanzania, Ama kwa hakika mafanikio ya Azam Fc ni makubwa kiasi kwamba ni mfano wa kuigwa kwa vilabu vingine.
Azam Fc iliweza kufanikiwa kuweza kujenga uwanja wake wa nyumbani ambao upo katika maeneo ya Chamanzi nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, uwanja huo wa Azam Fc ulizinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya .M. Kikwete ambaye alialikwa kuzindua uwanja huo wa klabu ya Azam, mafanikio ya kwanza ya Azam Fc yalikuwa ni kuweza kujenga uwanja wake wa chamazi.
Mafanikio mengine ya klabu ya Azam Fc yalikuwa ni kuweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu bara kwa msimu wa 2013/2014.
Na baadae ubingwa huo walioupata mwaka 2014, Azam FC imeweza kufanikiwa kuingia ushirika na bank ya National Microfinance Bank (NMB) ambapo Azam Fc imeingia Ushirika (Partenership) na NMB ushirika ambao una muuingizia pato la shilingi bilioni 1-2 kwa mwaka mmoja
Licha ya Mafanikio hayo yaliyopatikana katika klabu ya Azam FC imetangazwa kuwa moja kati ya vilabu bora Afrika huku Azam FC ikivipita vilabu kongwe Simba SC na Yanga SC ambavyo ni vilabu vya muda mrefu sana katika Ligi kuu ya Tanzania