Ni suala la ujirani mwema tu hakuna namna tuwapokee kama ilivyo desturi yetu kwa wageni. Tukiwapokea na kuwapa nafasi washiriki Ligi yetu hii itaendelea kutoa funzo kwa wengine kwani ujio wa Al Hilal ya Sudan katika Ligi Kuu ya NBC itaenda kuongeza kitu ingawa haitaathiri chochote kwenye kupoteza alama tatu kwa timu pinzani itakayocheza nayo siku hiyo.
Hakuna asiyeujua ukubwa wa Al Hilal na ubora wao lakini pia hakuna timu isiyotamani kucheza dhidi yao ili kuijitengeneza na kuendelea kujiimarisha zaidi.
Nafiriki hii itakuwa njema sana kwa zile timu ambazo zitakazoenda kucheza michuano ya kimataifa kwa msimu ujao. Hapa itaenda kuongeza kitu na kuwapa nafasi zaidi wachezaji ambao watakuwa katika timu shiriki.
Katika maisha ya kawaida hakuna asiyepitia matatizo na ikitokea imekuwa hivyo mpe nafasi kwani kwako haikupunguzii chochote. Tuseme karibuni Al Hilal SC katika Ligi shindani Afrika Mashariki.
Hilo suala la nani atazidiwa alama na Al Hilal wala kwao siyo kesi na haitaondoa chochote kuhusu hilo. Tanzania ya amani tunawapenda majirani. Kuna wakati niliwahi kuwaza hili jambo nilipoona wakati ule wanatanga tanga, nikataka kushauri hili kufanyika na nimefurahi kujua kumbe pale TFF kuna watu wana uwezo wa kufikiria mambo yenye tija kwa ligi yetu.
Nakumbuka mwezi January nilishangaa kwa nini hawakujumuishwa katika mashindano yaliyopita ya Kombe la Mapinduzi wakati walikuwepo hapa hapa.
SOMA ZAIDI: Barua Kwako Pacome Zouzoua Profesa Wa Boli
1 Comment
Pingback: Hii Ndio Mbavu Ya Kushoto Ya Azam Fc Yenye Balaa Zaidi - Kijiweni