Ligi kuu ya Tanzania ni moja ya Ligi bora na kubwa sana barani Afrika ni Ligi ya sita kwa ukubwa Afrika, Wacha ni kurejeshe miaka 10 nyuma nikimaanisha mwaka 2010, ukirejesha Kumbukumbu nyuma moja ya Ligi ambayo haikuwa maarufu sana ni ya Tanzania.

Nikusogeze tena miaka mitatu mbele mwaka 2013 vilabu vyetu havikuwa maarufu na hata walipojaribu kutoka nje ya Tanzania na kushiriki michuano mikubwa waliishia hatua za awali mapema tu, miaka minne mbele yaani 2017 njia na mwamba kwa Ligi yetu ilianza kuonekana kama ni safari basi tulianza kufika kwenye vituo maarufu nchini.

Kumbukumbu ni kuwa mpaka 2017 tulikuwa na timu moja tu iliyofanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya moja ya Ligi kubwa Afrika ambapo hawakufanya vizuri sana na kuishia makundi, baada ya Mwaka 2017 kuelekea miaka minne mbele ilianza kuwa historia huku Kumbukumbu mbalimbali zikaanza kuwekwa na vilabu kutokea Tanzania.

Haikutosha na Wala haikuishia hapo wachezaji na makocha mbalimbali wakaanza kuvutiwa na Ligi yetu, wengine wakifanya Ligi yetu kama daraja kwao kuvuka mipaka na kupata nafasi kwa vilabu vikubwa Afrika na wengine kwenda nje ya Afrika.

Ukiendelea tena miaka minne mbele, nje ya umaarufu sasa ni sehemu ambayo umaarufu wa vilabu vyetu umezidi kukua, kwa sasa nje ya Tanzania ni Simba SC na Yanga SC vinavyozungumzwa sana, siyo kwa bahati mbaya hapana bali ni kutokana na ubora tuliyonao kwa sasa.

Kelele na Afrika inatikisika kwa sasa pale ambapo vilabu vyetu hivyo vikishindwa kufuzu hatua ya makundi na hata kushindwa kucheza Robo Fainali jambo ambalo linaongeza hamasa na ubora wa Ligi yetu barani Afrika.

Yanga SC na Simba SC ndiyo kioo cha Ligi yetu ndani ya miaka mitano tumeshuhudia Robo fainali sita ambapo Yanga SC akifuzu mara mbili na Simba SC mara matano huku tukishuhudia Fainali moja kutoka kwa Yanga SC. Ni kukumbushe tu kuwa Robo Fainali hizo ni za Ligi ya Mabingwa Afrika Mara nne Simba SC mara tatu na Yanga SC mara moja na Robo fainali mbili za Shirikisho ambapo wote kwa pamoja wamecheza mara moja moja na moja ya Yanga SC iliwapeleka na kuishia Fainali ya Kombe ilo la Shirikisho.

Sitoshangaa kwa sasa moja ya klabu yetu au zote kwa msimu ujao kufuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho Afrika, ila tu nitasononeka kama zitaishia hatua ya Robo Fainali kwani ni wakati sasa Afrika iheshimu na kuwa na tahadhari na vilabu kutoka Tanzania.

SOMA ZAIDI: Ni Ngumu Kuamini Kamwe Unaondoka Jangwani

4 Comments

  1. Pingback: Sio Vibaya Kuwaiga Simba Kwa Jambo Hili Ambalo Walilianzisha

Leave A Reply


Exit mobile version