Baada ya kupitia njia ngumu kabisa mpaka kuwa mabingwa ni wazi kuwa ilikua njia ambayo hakuna ambaye alitegemea kuwa watakua mabingwa wa michuano ya AFCON kwa mwaka 2023 nchi ya Ivory Coast ambayo walipata nafasi ya kupita kama Best Looser baada ya Morocco kumfunga Zambia huku Tanzania dhidi ya Congo ikiisha kwa suluhu na hii leo tukitazame kwa undani kikosi bora ca michuano ya mataifa barani Afrika kwa mwaka 2023 ambaco kimetoka CAF.

Ronwen William

Golikipa wa Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana amechaguliwa kwenye kikosi bora cha AFCON baada ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo japo kuwa kikosi chao kiliishia hatua ya Nusu fainali huku kwenye michuano hiyo akifanya save 20 za hatari akiokoa penalti 6 huku akiondoka na jumla ya Clean sheet 5 kwenye michezo 7 pia huyu ndiyo Kipa Bora wa AFCON.

Ola Aina

Ana miaka 27 na anacheza klabu ya Nottingham Forest akiwa na Nigeria amekuwa akicheza kama beki wa kushoto amekiwasha sana kwenye AFCON hii na aliiwezesha Nigeria kufika Fainali ya michuano hiyo.

Aina amecheza michezo 7 ya AFCON akiisaidia timu hiyo kupata clean sheet 4 huku akipata kadi ya njano 2 kwenye mchezo 16 bora dhidi ya Cameroon na Ivory Coast, akitengeneza nafasi 8 za magoli akifanya recover mara 30 na akipiga mashuti 3 na moja likiwa on target.

Ghislain Konan

Ana miaka 28 na anakipiga Al Fahya huku akitumikia kikosi cha Ivory Coast kwenye AFCON hii na ndiyo namba tatu bora ya michuano, amecheza michezo 7 ikiwa ni sawa na michezo yote ya Ivory Coast huku akiwa Hana kadi yoyote ile, akifanya recover mara 45, huku akipiga jumla ya pasi 266.

Chancel Mbemba

Ana miaka 29 na anahitumikia Marseille ya Ufaransa, alikuwa beki tegemeo kwenye kikosi cha DR Congo kwenye AFCON hii na amecheza michezo yote kuanzia hatua ya makundi hadi mshindi wa tatu. Amepiga mashuti 5 na amefanikiwa kufunga goli moja akishinda tackling 3 mipira ya juu 25, recover mara 26 huku akiingilia mipira ya mpinzani mara 6 na amepata kadi 2 za njano kwenye michuano hii.

William Troost

Ana miaka 30 na ni beki wa kati wa PAOK FC ya Ugiriki, alikuwa nahodha wa Nigeria kwenye AFCON hii na ndiyo Mchezaji bora wa michuano kwa ujumla. Amecheza michezo 7 ikiwa ni sawa na michezo yote ya Nigeria kwenye AFCON hii huku akipiga mashuti 5 “On target” na amefunga magoli 3 ndiyo beki mwenye magoli mengi pia ameshinda mipira ya juu mara 19 ameingia mpinzani mara 5 akifanya recover mara 17 na amepata kadi moja tu ya njano dhidi ya Afrika Kusini.

Teboho Mokoena

Kiungo wa Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini ana miaka 27, alikuwa Mchezaji muhimu wa Bafana Bafana akiwa amecheza michezo yote ya kikosi hicho cha Afrika Kusini huku akipiga mashuti 19 yaliyolenga lango 9 na amefanikiwa kufunga magoli 2 na ametengeneza goli “Assist” moja tu. Amepiga pasi 330 akipiga mipira mirefu 31, huku akitengeneza nafasi 12, akicheza mipira 34 ya juu akiingilia mipira mara 6 akiblock mipira 2 na akifanya recover mara 41.

Jean Michael

Ni kiungo mkabaji wa Hull City akiwa na miaka 32 na Mchezaji wa Ivory Coast kwenye AFCON hii amecheza michezo saba ya kikosi hicho amepiga pasi 192 kwa usahihi pasi za juu mara 13 huku akitengeneza nafasi 4 na amegusa mara 261, akishinda tackling 4, akifanya interception mara 5 recover mara 20 na amepata kadi moja ya njano kwenye michuano mizima.

Franck Kessie

Kiungo wa Al Ahli ya Saudi Arabia mwenye miaka 27 na Kiungo tegemezi wa Ivory Coast, amecheza michezo 7 ya AFCON akipiga jumla ya mashuti 10 huku mashuti 6 yakipenga lango akiwa na magoli 2 na ametengeneza goli “Assist” mara moja, amefanikiwa kupiga pasi 206 kwa usahihi baada ya kupiga pasi 352 kwenye michezo yote aliyocheza, akipiga mipira ya juu 12 kwa usahihi na ametengeneza nafasi 7, akishinda tackling 7 na mipira ya juu 38 huku akifanya interception mara 8 na akiblock mpira mmoja huku akifanya recover mara 31 na Hana kadi yoyote ile.

Yoane Wissa

Winga wa Brentford akiwa na miaka 27 anakitumikia timu ya taifa ya DR Congo amecheza michezo 7 huku mmoja akitokea benchi, amehusika kwenye 2 akipiga mashuti 19 yaliyolenga lango yakiwa 5 na amefunga magoli 2, akipiga pasi 86 kwa usahihi akishinda mipira 4 ya juu akitengeneza nafasi 3 huku akipiga krosi 5 kwa usahihi akichezewa faulo mara 16 na amemiliki mpira kwenye lango la mpinzani mara 32.

Ademola Lookman

Winga wa klabu ya Atalanta mwenye miaka 26 na Mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, amecheza michezo saba ya AFCON, amepiga mashuti 8 huku 4 yakipenga lango na amefunga magoli 3 na ametengeneza goli “Assist” moja tu huku akipiga pasi 90 kwa usahihi akishinda mpira mmoja wa juu na ametengeneza nafasi 14 na amepiga krosi 8 kwa usahihi.

Emilio Nsue

Mshambuliaji huyu Akiwa na miaka 34 anacheza klabu ya CF Intercity na anaicheza timu ya taifa ya Equatorial Guinea amecheza michezo 4 ya AFCON na Taifa Lao lilitolewa kwenye hatua ya 16 bora, amepiga mashuti 9 huku 5 yakilenga lango na amefunga magoli 5 huku akiwa na hat trick moja akifunga dhidi ya Guinea Bissau pia huyu ndiyo Mfungaji Bora wa AFCON akiwa na magoli 5.

Kocha: Emerse Fae

Kocha huyu alikinoa kikosi cha Ivory Coast akianza kama Kocha msaidizi kwenye AFCON na akawa Kocha mkuu kuanzia hatua ya 16 hivyo ameongoza michezo 4 kama Kocha mkuu na amefanikiwa kushinda michezo yote 4 huku mchezo mmoja tu dhidi ya Senegal akishinda kwa mikwaju ya Penalti, huyu ndiyo Kocha Bora wa AFCON.

SOMA ZAIDI: Washindi wa tuzo za AFCON 

Leave A Reply


Exit mobile version