Pascal Gaundence Msindo Mchezaji kijana kutoka Azam Fc anaeyetokea mji kasoro bahari kwenye milima Ya Uluguru yaani Morogoro, alizaliwa mwezi wa nane tarehe 15 ya Mwaka 2003, Morogoro mjini.

Alianza maisha yake ya soka yalitangazwa kwenye kikosi cha vijana cha Azam FC baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari kwenye Shule ya Lupanga, alianza maisha yake Ya kabumbu kwenye “Academy” maarufu nchini na mkoa wa Morogoro Moro Kids tokea akiwa kijana mdogo lakini ilipofika mwaka 2012 alijiunga na Azam FC Academy na hapo ndipo maisha yake ya soka yalipoanzia na amefanikiwa kucheza michuano mbalimbali mpaka sasa kuanzia ngazi ya klabu hadi ya taifa.

Mpaka sasa amefanikiwa kuichezea timu ya vijana ya Azam kuanzia U-17 na U-20 na michuano ambayo amefanikiwa kucheza ngazi ya timu ya taifa na klabu ni pamoja na Ferwafa cup iliyofanyika mwaka 2019 nchini Rwanda, michuano ya AFCON U-17 mwaka 2019, East Africa cup Arusha ambayo ilifanyika nchini Tanzania mkoani Arusha, michuano ya Uefa Assist aliyoshiriki nchini Uturuki, Michuano ya Cecafa nchini Botswana, michuano ya Cecafa iliyofanyika mkoani Dar es Salaam mwaka 2018, michuano ya Cecafa iliyofanyika nchini Burundi, michuano ya Afcon U-20 pamoja na Ligi ya vijana ya U-20.

Pascal Msindo alikuwa akivaa jezi namba 50 akiwa anahitumikia timu yake ya Azam FC kwenye ngazi ya vijana huku akiwa timu za taifa za vijana akivaa jezi namba 22. Ni moja ya vijana waliyoonyesha kiwango kizuri na utulivu wa hali ya juu hawapo na mpira mguuni na mpaka sasa amefanikiwa kuonyesha kiwango kikubwa sana akiwa na timu kubwa ya Azam FC na kupelekea kumuweka benchi Cheikh Sidibe ambaye ni raia wa Senegal.

Ikumbukwe kuwa Pascal Msindo alisaini mkataba wake wa kwanza na kikosi cha Azam FC mwaka 2021 baada ya kuonyesha kiwango kikubwa akiwa na timu za vijana za taifa na klabu yake, mchezo wake wa kwanza akiwa na timu Ya wakubwa ilikuwa ni msimu wa 2021/2022 ambapo ulikuwa mchezo wa Ligi kuu wakiwa ugenini dhidi ya Dodoma jiji katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Hata hivyo mpaka sasa amefanikiwa kuchukua tuzo ya Mchezaji bora wa Michuano ya Cecafa iliyofanyika Tanzania na timu Ya taifa ya Uganda “The Cranes” kufanikiwa kuibuka bingwa wa michuano hiyo kwa kuwafunga Tanzania 4-1 kwenye mchezo wa fainali, huku mshambuliaji mwenzake wanayecheza naye Azam FC kwa sasa Abdul Selemani akiibuka mfungaji bora, huku akiwa hajatumikia timu yeyote kwenye Ligi kuu soka Tanzania bara zaidi ya Azam FC na amefanikiwa kusaini mkataba wa kwanza wa soka la kulipwa.

Pascal Msindo ameonyesha kuwa wachezaji wa Kitanzania wanaweza na wanavipaji vikubwa sana jitihada za kijana hiyo zimemfanya apate nafasi ya kuaminika kikosini mbele ya Mchezaji wa Kimataifa (mgeni) Cheikh Sidibe ambaye alionyesha kiwango kiasi ambacho ilikuwa ngumu kuamini kuwa anaweza kuwa chaguo la kwanza ila kwa sasa ndiyo chaguo la kwanza na Mchezaji muhimu kwenye nafasi hiyo.

Moja ya sifa yake kubwa ni kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu mawili ya kukaba na kushambulia kwa usahihi, amekuwa akitumika vizuri pale ambapo timu itahitaji kushambulia basi ataonekana kwenye kutengeneza mashambulizi na kumfanya kuwa na “Assist” nne mpaka sasa akiwa ni Mchezaji wa tatu mwenye “Assist”nyingi kikosini akizidiwa na Kipre Junior pamoja na Feisal Salum huku akiwa amefunga goli moja.

Tofauti ni kuwa kijana huyu mpaka sasa hajapata nafasi Ya kucheza kwenye kikosi cha timu kubwa Ya Taifa maarufu Taifa Stars licha ya kutumikia timu mbalimbali za taifa za vijana kuanzia U-17 pamoja na U-20, huu ndiyo wakati wa kumpa thamani kijana huyu wakati wa kutia moyo vijana wengine wa kuona ukipambana basi utapewa nafasi ya kulitumikia taifa lako.

SOMA ZAIDI: Hili La AL HILAL Kucheza Ligi Kuu Ya Tanzania Limenitafakarisha

 

1 Comment

  1. Pingback: Kambi Ya Simba Zanzibar Itaongeza Kitu Kikosini - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version