Rais wa Klabu ya Young Africans SC na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris Nchini Ufaransa, jana Januari 3, 2024.

Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka Kwa ndugu Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya Vilabu Wanachama.

Vilevile, Ndugu Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Eng Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambapo PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa Toulouse kwa magoli 2-0.

Baadhi ni picha za Hersi alivokutana na baadhi ya wachezaji wa PSG baada ya kutwaa ubingwa wa Trophies des Champions kwa kumfunga Toulouse.

Endelea kusoma zaidi kuhusu taarifa mbalimbali kwa kugusa hapa.

 

1 Comment

  1. Pingback: Zanzibar: Simba Wapeleka Jezi Ikulu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version