Kifo kipo katika miguu tunatembea nacho,Siyo kwamba tunatembea nacho tu katika miguu tu pengine tunasafiri nacho katika vyombo vya majini,angani na barabarani.

Hadithi inapokuwa tamu kwenye gazeti , kitabu au runinga hukatizwa na chini yake utakutana na maneno “Itaendelea toleo lijalo”.Lazima utakuwa na hamu ya kuendelea kutaka kuisoma ama kuitazama.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Young Africans (Yanga Sc) kutoka nchini Congo,Heritier Makambo aliikacha klabu hiyo na kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia klabu ya Horoya ya nchini Guinea misimu kadhaa iliyopita.

Kitendawili kilichozungumzwa na baadhi ya wadau wa soka pamoja na mashabiki ilikua ni je Makambo ameuzwa au kaondoka bure?. Maswali hayo yalikuja baada ya mwenyekiti wa Yanga  kusema watafanya mazungumzo angali tayari alikua amesaini,wasiwasi huo ikawa ni siri iliyowekwa hasa katika wakati huu wa utandawazi wa habari.

Lakini lengo langu haswa sio kutazama aliondokaje Yanga Sc na kujiunga Horoya Fc. Makambo alikuja Yanga Sc kwa bei rahisi sana huku wengine wakitupia dongo usajili wake lakini alifanikiwa kujibu kwa vitendo.

Katika takwimu Makambo alicheza mechi 40 na kufanikiwa kufumania nyavu takribani mara 21 ni wastani mzuri kwa mshambuliaji hasa katika msimu wa kwanza tu kwenye klabu tena klabu yenye iliyokua na ukata na uhaba wa wachezaji wenye ubora wakati ule.

Katika muda mfupi ambao alikuwa na Yanga Sc miguu yake  na kichwa chake alivitumia kuwaachia simulizi tamu  Wanayanga ikichagizwa na aina yake ya ushangiliaji. Akili na kalamu za wachambuzi vilikuwa vinaandaa maneno mapya kila siku.

Makambo hakuwa na kashifa ya Donald Ngoma au Obrey Chirwa kusikia amegomea mazoezi au kukuta anatajwa kwa lolote baya juu ya klabu yake jambo ambalo hata wazawa kama Kelvin Yondani au Ajibu liliwashinda,jambo ambalo Haruna Niyozima licha ya ufundi wake lilimshinda, ni jambo dogo tu “Nidhamu”.

Achana na simulizi tamu ya Makambo, kama kuna jambo linaumiza kichwa changu ukiacha changamoto za maisha binafsi basi ni kuona hawa vijana wetu wanashindwa kuwa na viwango endelevu,ukitazama wachezaji wengi wazawa wanapotea muda mfupi tu baada ya kuibuka kwenye soka wachezaji kama Habib Kiyombo,Jofrey Mwashiuya mchezaji aliyenifanya niandike Choga 19 katika jezi yangu kuna wengine kama Abrahaman Musa Salim Aiyee, Crispin Ngushi na wengine wengi wamepotea haraka.

Unakaa unajiuliza inakuwaje Makambo wa msimu mmoja aliwaacha hapa hapa Tanzania?,Ni maswali magumu yenye matundu madogo ya kupitisha maji.

Vijana wetu wanatakiwa kujitambua kuwa na nidhamu ya kutosha naposema nidhamu sio kuwaheshimu wanajamii inaokuzunguka tu hata kuheshimu vipaji vyao ni nidhamu ya hali ya juu sana.

Makambo alikuwa anajielewa pengine hata mwalimu wake Zahera Mwinyi alimwambia hapa Yanga Sc fanya njia ya kupita tu,Fanya kama barabara ya vumbi huku ukiitafuta lami kwa haraka zaidi,amefanikiwa.

Makambo aliacha simulizi tamu inayoendelea hadi sasa lakini Aiyee,Mwashiuya,Ajibu,Paul Godfrey,Rashidi Juma,Said Ndemla na wengine wengi simulizi zao zimeishia nyumbani kwao.

Watanzania ni watu wa matukio hasa kwa waliofanya vizuri na huwa na heshima sana  pitia kurasa mbalimbali utakutana na maneno haya “TBT” wakiwa na maana ya kumbukumbu, wanajali sana.

Wachezaji wetu wanatakiwa kujitambua wao ni akina nani katika soka la Tanzania, wajue wanataka nini kwenye ramani ya soka letu.

Amkeni vijana chipukizi Mbwana Samata hakufika Ulaya kwa bahati mbaya bali ni kujitambua yeye ni nani.

SOMA PIA: Mashabiki Na Wachezaji Wana Nguvu Kubwa Ya Uchumi

 

7 Comments

  1. Gachy Mr money on

    Ama kweli kipaji ni Kam mshumaa kaka ukiweka katikati ya upépó basi hàkuna mda mrefu wa kuwaka🥺🥺🥺

  2. Pingback: Ni Wakati Wa Vilabu Kula Matunda Ya Timu Za Vijana

  3. Pingback: MVP Wa Ligi Mbalimbali Kuja Kucheza NBCPL Ina Maana Gani?

Leave A Reply


Exit mobile version