Baada ya michuano ya mataifa barani Afrika kutamatika rasmi kwa fainali ya kibabe ambayo wenyeji Ivory Coast walikua wanakipiga na Nigeria na tembo wa Ivory Coast kuondoka na ubingwa baada ya kuwafunga Nigera bao 2:1. Kama utakua ni mmoja kati ya wale ambao wanajiuliza kuhusu tuzo lakini hapa tumekuandalia vipengele vyote na washindi wa tuzo hizo.

Mchezaji Bora wa michuano

Nahodha wa Nigeria William Troost Ekong nayecheza nafasi ya beki wa kati ana miaka 30 tu akiwa anakitumikia kikosi cha PAOK FC ya Ugiriki.AFCON hii amevaa jezi namba 15 ndiyo mchezaji bora wa Mashindano haya amecheza jjmla ya mechi sita na amefunga magoli 3 kwenye mashindano.

Kipa Bora

Nahodha wa Bafana Bafana Ronwen Williams akiwa na miaka 32 ndiyo amechaguliwa kuwa kipa bora wa mashindano haya toleo la 34. Amecheza michezo yote 7 ya AFCON kwa kikosi chake cha South Afrika akifungwa jumla ya goli 4 akiondoka na “Clean sheet” 4 kwenye mashindano haya na kuiwezesha Bafana Bafana kumaliza nafasi ya tatu.

Huyu ndiyo kipa aliyeweka historia ya kudaka mikwaju 4 ya penalti kati ya mikwaju 5 kwenye mchezo wa Robo fainali dhidi ya Cape Verde.

Mchezaji Bora Kijana

Kijana anayekipiga Brighton ya England pamoja na kikosi cha Ivory Coast akiwa na miaka 22 tu Simon Adingra anachaguliwa kuwa Mchezaji bora kijana na AFCON nchini Ivory Coast. Amecheza jumla ya michezo5 akifanikiwa kufunga goli moja dhidi ya Mali huku akitengeneza magoli “Assist” 2 kwenye fainali dhidi ya Nigeria na alikuwa akivaa jezi namba 24.

Mfungaji Bora

Akiwa na miaka 34 mshambuliaji na nahodha wa Equatorial Guniea Emilio Nsue anaibuka Mfungaji bora wa AFCON toleo la 34 akiwa amefunga jumla ya magoli 5.

Hata hivyo magoli hayo amefunga kwenye michezo miwili tu akifunga hat trick dhidi ya Guinea Bissau pamoja na mawili dhidi ya Ivory Coast huku akiweka historia ya kufunga hat trick ya kwanza ya AFCON msimu huu.

Kocha Bora

Kocha mzawa Emerse Fae amechaguliwa kuwa Kocha bora wa AFCON, alianza michuano hii kama Kocha msaidizi wa Ivory Coast baada ya hatua ya makundi kutamatika akakabidhiwa mikoba ya Kocha mkuu.

Ameiongoza Ivory Coast kwenye michezo 4 kama Kocha mkuu na amefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yote 4 huku mchezo mmoja wa hatua ya 16 dhidi ya Senegal akiibuka na ushindi kwa mikwaju ya Penalti.

Fair Play Team

Timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana imechaguliwa kuwa timu iliyoonyesha mchezo wa Kiungwana zaidi maarufu “Fair Play” kwenye michuano hii ya 34 ya AFCON iliyofanyika Ivory Coast. Hata hivyo Bafana Bafana ndiyo washindi 3 wa michuano wakiishia hatua ya Nusu Fainali baada ya kutolewa na Nigeria kwa mikwaju ya Penalti.

SOMA ZAIDI: Wachezaji Watano Muhimu wa kuwapa ubingwa Ivory Coast.

2 Comments

  1. Pingback: Takwimu Na Rekodi Zote AFCON Unazopaswa Kuzifahamu - Kijiweni

  2. Pingback: Hiki Hapa Kikosi Bora Cha AFCON 2023 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version