Kama wewe ni mtu wa mpira ambaye mara nyingi huwa unaenda viwanjani katika baadhi ya mechi haswa zile ambazo huzikutanisha klabu za Simba na Yanga basi utakua unajiuliza maswali ambayo pia huwa niko nayo kichwani kwangu na kubwa ni kuhusu hawa makomando wa timu hizi.

Ngoja nikupe stori moja kuhusu makomandoo hawa, wiki moja kabla ya mchezo kati ya Simba na Yanga mimi ni miongoni mwa wale ambao katika pitapita zangu nilipita nje ya uwanja wa Benjamin Mkapa na kuwakuta watu katika makundi wakiwa wanaviziana akiamka mmoja wa klabu hii kwenda getini basi ujue kuna mwingine naye ataamka kwenda kuona au kutazama nini kinaendelea.

Mara nyingi kinachonichanganya zaidi wengine hukesha kabisa nje ya viwanja hivyo wakilinda lakini pia wapo ambao husafiri hadi mikoani kwa kazi hiyo kwani huwa wanalinda nini? Na kuna wakati unakuta kabisa viwanja hivyo vina walinzi kabisa mfano uwanja wa Mkapa kuna walinzi lakini wao henda nao kulinda.

Mfano katika mchezo wa Simba sc vs Al ahly siku tatu kabla kuna kikosi kinachojiita Makomandoo wa Simba sc kilikwenda kuweka kambi kwa dhumuni la kulinda uwanja wa Mkapa lakini juhudi ziligonga mwamba baada ya Maofisa wa CAF kuwazuia hao makomandoo kulinda uwanja.

Hii siyo kwa Simba tu hata kwa Yanga nao huwa wanautamaduni huo wa kulinda uwanja haswa kipindi Cha Dabi ya Kariakoo na mechi za kimataifa. Swali la kujiuliza Hawa makomandoo huwa wanalinda Nini? Na wakati uwanja una security guards ambao wanalipwa kwa mwezi Sasa hao makomandoo wanakua hawana Imani na hao walinzi kuwa uwanja utaibiwa na timu zao zisicheze?

Jibu ni hakuna bali kinachoendelea hapo kwenye ulinzi wa makomandoo ni Imani za kishirikina na uchimbaji wa uwanja (uharibifu) hakuna kingine zaidi ya hilo tukubali tukatae na nadhani TFF na mameneja wa uwanja wapige marufuku timu kuingiza makomandoo wao kabla ya mechi na ni wakati wa kubadilika.

SOMA ZAIDI: Yanga Sc Kutinga Robo Fainali Imekuwa Nongwa?

Leave A Reply


Exit mobile version