Yeyote aliyekujua ukiwa mtoto mdogo hatakuheshimu ukiwa mkubwa.Ni methali ya kiarabu,Kwa ufupi mazoea huleta dharau,mazoea huzaa hata wivu.

Wagiriki wa zamani walizungumzia mtu mwenye shamba la ngano lenye ukamilifu.Watu walilistaajabia shamba lake.Mabua yote yalikuwa na urefu sawa.Walipomuuliza ni namna gani mabua yote ya ngano yalikuwa na urefu sawa alijibu.”Rahisi.Kila mbegu inayotokeza kichwa chake kuzidi nyingine nakata kichwa”.

Hapo awali kulikuwa kuna historia moja tu kubwa katika klabu ya Young Africans sports club nayo ni kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1935 nyingine zote ambazo zilifata zilikuwa ni ndogo ambazo pia zinatajwa kuwa historia.

July 9,2022 wanachama wa Young Africans Sports club waliongeza historia nyingine kwa kupata uongozi mpya uongozi ambao uliingia kwa kishindo cha kura zote ama kwa lugha nyepesi bila kupingwa hii ni baada ya mgombea Hersi Said kuwa peke yake kwenye kiti cha urais wa klabu.

Aliingia Young Africans kukiwa tayari kuna mataji mengi sana ya ligi kuu kuliko timu nyingine yoyote Tanzania.

Tangu kuingia kwa Eng. Hersi Said klabu hiyo imepata mafanikio makubwa zaidi mojawapo ikiwa ni kufika fainali ya kombe la shirikisho, kuingia makundi ya klabu bingwa na hatimae kufika robo kitu ambacho hakikufanyika kwa miaka mingi sana.

Mafanikio hayo hayajatokea kwa bahati mbaya bali ni amani na utawala bora ndani ya klabu hiyo.

Kalamu yangu leo ngoja ikupitishe katika maeneo machache ambayo ndio imekua chachu kubwa ya mafanikio ya uongozi wa Hersi Said.

Kama kuna kitu kiliweza  kuathiri akili za Wanayanga ni jina la tajiri Yusuf Manji kwa muda mrefu, licha ya uwepo wa kiongozi  Dr Mshindo Musola bado kulikuwa na makundi mawili wanaoamini Yanga Sc bila Manji haitasimama na wanaoamini inawezekana.

Katika uongozi wake Eng Hersi Said amehakikisha makundi haya mawili yanaamini kitu kimoja tu nacho ni Young Africans sports club.

Kama mkulima wa ngano alivyoweza kukata vichwa vya mbegu zilizotaka kuwa juu ya nyingine ndicho amekwenda kufanya Hersi Said.

Nyakati zimeenda sana na mambo pamoja na mitazamo ya kuifanya klabu itulie Kwa kuwa na watu makini.

Timu ya Digital waliporecruit na kuibuka na Priva ilikuwa ni Moja kati ushindi mkubwa katika kujenga Yanga katika ushindani huko mitandaoni.

Idara hii imewatumia sana Alwatan Abdulaziz vizuri. Kila mwanayanga hupata taarifa zake kupenda kufuatilia Yanga Tv.

Idara ya digital imefanya nchi isimame imara katika kuitangaza Yanga.

Kama kuna jambo ambalo kilikua kilio kikubwa sana kwa baadhi ya mashabiki basi ni klabu kutokuwa na mpangilio wa mauzo ya jezi za timu. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa klabu kongwe kukosa mpangilio mzuri wa kuona ni jinsi gani inanufaika na mauzo hayo.

Kuna Wanayanga walishajiapia hawatanunua jezi za timu yao kwa sababu kama klabu haipati chochote zaidi ya kunufaisha watu wa mipango yao.Katika hili amekwenda kujenga mfumo bora ikiwemo kuingia ubia na makampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo pamoja na kuwa na duka lao  pale makao makuu ili kuweza kuambulia chochote.

Natambua ugumu ambao ulikuwepo lakini chini ya uongozi wake hili wameamua kwa pamoja na imewezekana.

Katika uongozi wake ambao unakwenda kutimia miaka miwili sasa amehakikisha klabu inakuwa na wanachama wapya ambao ni hai sio bora wanakadi, klabu imeanza kuwa na takwimu sahihi za idadi ya wanachama wake tofauti na awali ambapo walikuwa wakitajwa kwa kujumlisha mashabiki ambao hawana kadi.

Chini ya uongozi wake Eng Hersi Said amekaribisha makampuni mengi kuingia kuidhamini klabu hii kongwe nchini katika maeneo tofauti tofauti miongoni ni wale ambao waliingia kwaajili ya ukarabati wa jengo lao pale Jangwani, uwepo wa makampuni mengi kumefanya klabu hiyo kukusanya pesa nyingi za kuweza kuendesha timu kiujumla.

Haya ambayo tunayaona kwa sasa hayaji bahati mbaya bali ni utawala bora ambao ni lazima tuupongeze kabla ya mengine kutokea(Hatuombei iwe hivyo), hatuwezi kupindisha mafanikio ya watu kwa kumpa mtu kwenye dhana ya matani.

Lakini nitakuwa mchoyo ikiwa sitaweza kuendelea kuukumbusha uongozi huu juu ya jambo hili muhimu, historia zote zipo lakini Wanayanga na wadau wa soka wanasubiri historia moja kubwa sana nayo ni klabu kumiliki uwanja wake.

Hayo ni machache ambayo nimewaza kama mdau wa michezo kwa leo kazi ni kwenu kuyachambua na kufanyia kazi.

SOMA ZAIDI: Ligi Kuu Inakaribia Hivi Ndivyo Wazawa Wanatakiwa Kufanya

6 Comments

  1. Nikwery sana inabid club kubwa tuwe na wanja wetu pale jagwani maan haiwezekani club kubwa tuwe atuna uwanji. Tunakosa hela nying sana katika mech zetu za nyumban kwa sababu ya kukodi uwanja kila march

    • Nakubaliana na wewe mdau kwa asilimia zote, kwani katika ahadi zake hilo swala la uwanja lilikua moja ya ahadi zake na ameiongea mara nyingi sana akimaanisha kuwa lipo kwenye mipango yake.

  2. Ndaskoykileta on

    Nafikiri mchakato wa kuujenga uwanja wa jangwani ulikua unasubiri kuondolewa kwa utata wa kimazingira uliokuwepo baina ya eneo la kuujenga uwanja wa jangwani wa yanga na bonde la mto msimbazi.
    Kama nipo sawa utata huo umeshaondolewa nafikiri kilabu kingeanza mchakato wa kuanza kulifanikisha hilo jamba ila kama utata huo bado upo naishauri kilabu ya yanga iangalie ustaarabu mwingine wa kupata eneo sehemu nyingine na kujenga uwanja maana uwezo wanao, nguvu wanayo na mahitaji poa wanayo. Hata kama ndoto yao ya kumiliki uwanja ni eneo la jangwani haitabadilisha mtazamo na matamanio yao bali itawaongezea nguvu na upana wa ndoto yao pia
    Naamaanisha mfano yanga ikaanza ujenzi wa uwanja nje kidogo ya kijiji cha mzizima ukakamilika kisha baada ya muda wakaruhusiwa kuujenga uwanja wa jangwani itakua ni kilabu ya kwanza ama miongoni mwa vilabu vinavyomiliki viwanja viwili vya mpira kama ntakua mtafiti mzuri
    Kumiliki viwanja viwili pia itawaongezea uwezo kama sio upana wa kuamua game ipi ichezewe jangwani na ipi iwe nje ya jangwani
    Pia ikumbukwe kuna timu ya vijana na timu ya wasichana wanahitaji uwanja wa mazoezi pia kuna wakati timu zote zitahitajika kuingia mazoezini ama mchezoni zikiwa nyumbani kwahiyo itakua ni faida pia kwa yanga

  3. Pingback: Chama Clatous Na Kumbukizi Ya Kurasa Za Ajibu

  4. kweli kilicho baking ni kuleta kombe la Africa championships ambala linatakiwa Liambatane
    na uwanjaaaa
    haiwezekani time kubwa nyingi duniani zinc viqanja vyao half sisi bado
    ila engineer bigup ✊👍👍👍👍👍👍👊

Leave A Reply


Exit mobile version