Kuna mtu aliishi mlimani,alikuwa na sanamu kwa kawaida aliicha mbele ya nyumba yake.Siku moja mtu kutoka mjini alipitia eneo hilo na kuona sanamu.Aliuliza kama ilikuwa ya kuuzwa.Mtu wa mlimani akajibu: “Nani atanunua sanamu hii mbaya?”.Mtu wa mjini akatoa sarafu mfukoni na kumuuliza upo tayari kuniuzia kwa sarafu hii?.Mtu wa mlimani akakubali kuuza.

Baada ya miezi michache mtu wa mlimani alienda mjini.Aliona mstari mrefu wa watu wamejipanga mbele ya duka.Alisikia mtu akitangaza: ” Njoo muone sanamu nzuri duniani. Gharama ya kuiona ni sarafu mbili.”Yule mtu wa mlimani alilipa sarafu mbili ili aweze kuona sanamu ambayo aliuza kwa sarafu moja.

Kama kuna mambo ya kushangaza katika soka la Tanzania ni jinsi mashabiki wanvyoshindwa kuvithamini vilabu vyao vya nyumbani. Mashabiki wengi wanahusudu zaidi uwepo wa Simba sports club na Young Africans sports club kuliko timu zao za mikoa husika.

Ni mara chache kuona mashabiki wanajaa uwanjani kuzipa hamasa timu zao za mikoa kama hazichezi na Yanga Sc au Simba Sc ilitokea hivyo kwa Mbeya City pekee miaka kadhaa nyuma.

Katika msingi wa kawaida ili mgeni wa mbali aje ni lazima umkaribishe hawezi kutoka Dar es Salaam kuja kwako Mbeya,Mwanza au Kigoma bila kuwa na malengo na sehemu hizo ila unapomkaribisa atakuja kwa sababu yako. Maana yangu Simba Sc na Yanga Sc haziwezi kwenda Kigoma bila kuwa na timu huko ya ligi,haziwezi kwenda kirahisi Sumbawanga bila kuwa na timu huko za kufanya waende.

Mashabiki wa soka hasa nje ya Dar es Salaam mnatakiwa kuvipa nguvu vilabu vyenu ili viendelee kuwaletea hao mapacha wawili kutoka Dar Es Salaam. Kuna mikoa hadi leo inatamani kuziona moja kwa moja uwanjani lakini haiwezekani kwa sababu hawana misingi ya kufanya wakongwe hao kwenda huko.

Sina maana ya kutozipenda Simba Sc na Yanga Sc mioyoni mwenu lakini mnatakiwa kukumbuka na nyumbani mfano mdogo Lipuli ikicheza na Mtibwa mnapaswa kujaa,Alliance ikicheza na Ndanda vivyo hivyo,kusalia kwa vilabu hivyo ni pamoja na nguvu ya mkoa husika vyama vya soka hadi mashabiki.

Hili la mwisho kwa upande wa vilabu, viongozi wa vilabu vya nje ya Dar Es Salaam mnatakiwa kujenga ushawishi kwa mashabiki toka mikoa yenu hakuna shabiki wa Dar es Salaam ambae atasema ahangaikie Stand United ama klabu nyingine nje ya jiji alilopo ni mpenda mpira tu ndio anaweza.

Wasimamizi mnatakiwa kujenga timu ambazo zitawafanya wazawa waipende, ushujaa wa Mbeya City wa kuwa na wadau wengi ulitokana na ushindani waliokuwa nao. Baada ya kuyumba wote tuliona kilichotokea,anguko la African Lyon ni ukosefu wa mashabiki hata ikicheza hakuna mapato ya kufanya wajiendeshe ipasavyo.

Hakuna Simba na Yanga mikoani bila msingi wa uwepo wao watakuja kucheza na timu sio nyie watazamaji. Hata Ulaya mambo ya kupenda timu kubwa yapo lakini suala la nyumbani tunaona jinsi wanavyojaa kila mechi timu zao zikicheza.

Ni mtazamo wangu ikiwapendeza ishini nao lakini isipowapendeza chagueni maisha ya kawaida.

SOMA PIA: Bisris Norte Inahitajika Kwa Timu Zetu Kimataifa

3 Comments

  1. Pingback: Huu Ni Mtazamo Wangu Kuhusu Soka Letu

Leave A Reply


Exit mobile version