Baada ya mapumziko ya siku kadhaa ni wazi sasa macho na masikio ya wengi ni kuhusiana na michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) ambapo kuanzia hatua ya makundi mpaka hatua ya robo fainali yamekua na mvuto mkubwa sana kwa mashabiki wa soka barani Afrika haswa kutokana na matokeo ya kustaajabisha na vigogo kutolewa.

Kumbuka kuwa katika hatua hii ya nusu fainali timu zilizofuzu ni wenyeji Ivory Coast, South Africa, DR Congo na Nigeria na wote tayari walishawahi kuwa mabingwa wa michuano hii ya AFCON hivyo ni nusu fainali ambayo sio ya kinyonge sana kwani inawakutanisha mabingwa wa mara kadhaa wa michuano hii mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya timu za taifa na hapa tutazame timu na idadi ya makombe waliyochukua katika michuano hii.

  1. Nigeria

Amefuzu hatua hii baada ya kumtoa Angola kwa bao 1:0 katika hatua hii ya nusu fainali ndio ambaye anaongoza kwa kuchukua ubingwa mara nyingi zaidi kwa timu zilizofuzu hatua hii ya nusu fainali. Amechukua ubingwa huu mara 3 ambapo ni mwaka 1980, 1994 na mwaka 2013.

  1. Ivory Coast

Huyu ni mwenyeji wa michuano hii ya mataifa barani Afrika kwa mwaka huu na ameingia hatua hii baada ya kumtoa Mali. Sio mnyonge kwani amechukua michuano hii ya mataifa barani Afria mara 2 ambapo ni mwaka 1992 na mwaka 2015.

  1. DR Congo

Timu hii ya taifa ambayo ndani yake kuna wachezaji wengi sana kutoka ligi mbalimbali kubwa barani Ulaya wamewahi kuchukua ubingwa huu wa AFCON mara 2 ambapo waliutwaa mwaka 1968 na mwaka 1974 hivyo wana kiu kubwa ya kuweka rekodi ya kuchukua mara ya 3 michuano hii.

  1. South Africa

Hawa ndio unaweza kusema vibonde ila pia waliwahi kuwa mabingwa wa michuano hii mara moja pekee na swali kubwa ni wataweza kutinga fainali? Kwani hatua hii ya nusu fainali anakutana na Nigeria ambaye ndio mkongwe zaidi katika hatua hii akiwa na ubingwa mara 3.

Bila shaka tumeona namna ambavyo nusu fainali hii ilivyokua sio ya kinyonge kwa kuona ambavyo wote waliotinga nusu fainali washawahi kuwa mabingwa , kumbuka kuwa Nigeria dhidi ya South Africa huku Ivory Coast dhidi ya DR Congo.

SOMA ZAIDI: Walioleta VAR AFCON Wana Nafasi Yao Moyoni Mwangu

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Ivory Coast vs DR Congo Suka Hivi Mkeka Wako - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version