Kocha  Mkuu mpya Benchika ni sababu moja tu kati ya zile 10 za Simba Sports, Ni Kocha mkubwa ambaye ambaye amefanya makubwa sana ila Simba narudia kwa misimu zaidi ya minne haijawahi kuwa na shida ya Makocha, always inaleta Makocha wakubwa tena wenye CV kubwa sana, lakini kuna sababu nyingine nyingi hazijawekwa sawa ili Mwalimu afanye makubwa.

 Mchukue Benchika na alipopita kote anza tu na USMA pale je una wachezaji wenye profile kama wale? Mchukue tu Benchika mtazame alipokuwa RS Berkane alikuwa na squad gani na watu gani kikosini je una watu kama wale ama profile angalau ya kufanana? Simba imetoka kwa Robertinho ambaye alikuwa Muumini wa soka la Vijana pale Vipers maana yake alikuwa anaidai timu msingi mzuri wa soka la Vijana na angechukua Wahitimu kadhaa wazuri kuchanganya na wazoefu ili timu iondoke, haikuwezekana akastuck kwenye mfumo uliopo ambao umemfelisha ijapo kwangu hakufeli alifelishwa.

Sasa timu ipo kwa BENCHIKA, mapema hii kabla bahari haijakorogeka, anzeni kuweka sawa na mambo mengine! Wachezaji wapya wa kuongezeka ukubwa wa kikosi kuendana na mbinu zake pia Rotation, kabla ya kuanza kelele za Fitness njia ya asili ya Mchezaji kuwa fit ni kugawana dakika! Mmeona Jude Bellingham ameumia? Mmeona Vini ameumia? Unaweza kuwa na Fitness Coach wa viwango na kila kitu ila kama hakuna Rotation kwa baadhi ya Wachezaji wakitumika sana ni eidha majeraha ama wachoke na wasikupe kile unachotarajia! TAFADHALI TUMIENI VYEMA DIRISHA LA USAJILI HILI.

Leave A Reply


Exit mobile version