IlipoishiaJolvin alimwangalia, mtu anaeshukuru na anaeomba msamaha kampea mgongo!

” Gorii mtoto mwenye heshima, anae nidhamu, anaheshimu watu wadogo kwa wakubwa! Hii kuongea amekupea mgongo tuiweke upande ganii!?”

Gorii alimgeukia alikumbuka Yale maneno aliwahi kuyaongea Jolvin, siku wakutane kwenye chumba Cha Rich na leo kayarudia japo kayabadilisha kidogo, ilibidi amuulize;?

 ” Kaka White…. Huwa ninakukosea Sana mpaka uanze kunielezea tabia kupitia mafumbo pale ninapokuuzi!?” 

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA SITA

 ” Kwasababu ndivyo ulivyo!”

Kisha aliinuka akitoka chumbani kwa Gorii.

Gorii aliinuka kufunga mlango! Akakaa kwanza kitandani huku akitizama picha ya Mamake ukutani.

   “” Ee Mungu! Mlinde mamangu awe mzima huko aliko haijalishi nitachelewa kumpata ila hakikisha anaishi!”

Asubuhi kulipokucha Gorii alijiandaa kwenda chuoni! Siku hiyo hakutaka kumsubilia Kaka White. Alichukua usafiri wa bus hadi chuoni.

Wakati akiwa njiani Mawazo yake yalikuwa mbali alihisi Kama  mamake anamuita! Alisimama kuchungulia dirishani! Kuna abiria alikuwa akishuka ilibidi aunge nae akachukua.

Alianza kuangaza huku nakule Kama ndie mama kweli kamwita kumbe ni akili yake tu! Ile anatuliza akili bus tayari lishaondoka aliangalia mfukoni Kama anae pesa hakuwa nayo.

   “” Ooh! Kaka White sijui atapita hii njia!! Halafu mbona kule Kuna watu wengi wanakimbilia.

Ilibidi aliunge, lilikuwa ni gari la matangazo limepaki pembeni kidogo na barabara, walikuwa ni watu wa Tecno wakitangaza biashara zao huku wakiuza simu! Gori Alisimama akawa amejisahau kabisa! Alianza kuangalia vijana wanavyocheza pale! Akawa amevutiwa nao! Mtangazaji alitangaza anahitaji watu watatu watakaoweza kushindanishwa kucheza na akishinda atapewa zawadi ya Simu.

Gorii alitabasamu Kwanza! Aliangalia jinsi alivyovaa akaona Kama akienda pale atajulikana  ni mwanachuo! Aliangalia kwenye begi lake huwa anatembea na prova! Pamoja na viatu vya wazi akitoka chuo hupitiliza navyo dukani.

Akaona wee! Hawezi kupitwa hivihivi na hiyo Simu, alibadilisha Ghafra akabaki kwenye suruali ya chuoni kwa juu akajazia prouva kuficha ile sale, akawa hatambuliki tena Kama mwanachuo!

Alizamia mbele, ile anakuja kuangalia kawa mtu wa tano! Dj alimwambia arudi lakini muda huo ndio alizidi kusogea kunako mziki! Watu ikawa ni oya! oya! Abaki… Abaki..!

Dj alimwachia acheze! Mziki ukawa umewekwa! Round ya kwanza mtu mmoja akaishia, Hadi ilipofika Round ya mwisho Gorii alikuwa bado akiongoza! Walibaki mabinti wawili washindaniehwe na atakae shinda ndio atapatiwa simu!

Gorii alimtiza mwenzake akaona kamnunia kweli! Yeye Tena! Aliamua kucheka kwanza huku akinyosha kiuno, kushoto kulia, hayo yalikuwa ni maandalizi tu!”

Mziki ulivyoachiwa Gorii alicheza Kama hatocheza tena, baadae Dj alisimamisha mziki kwanza angalau awahoji majina yao, binti wa kwanza alijitambulisha Amina! Alipofikia upande wa Gorii alifikikilia Kama atataja jina lake itakuwa kesi Tena, aliwaza baadae akasema

 ” Kaka White” watu wote walibaki wakicheka DJ ilibidi aachie mziki huku kila mtu akimshangilia na ndio akaibuka mshindi wa kwanza na Amina akiwa ni mshindi wa pili ilibidi na yeye pia apatiwe T-shirt na kotia.

Gorii alikabiziwa tshert ya Tecno, kofia na Simu! Aliziweka kwenye begi lake Kisha alipewa maiki neno moja aongee, alichofanya ni kusema “” Thank you” akarudisha maiki kwa bahati mbaya ile anarudishia maiki ule waya wa maiki ukafunua prouva, T-shirt ya ndani ikaonekana watu wakaanza kumjadili huyo si mwanachuo kabisa! 

Gorii akashangaa watu wote wanamnyoshea kidole ilibidi ajikague kwanza ndio akaona T-shirt imeonekana.

“” Daaah!! Nini tena hiki? nisije nikawa sinema Tena hapa!”

Alichukua begi lake huku akitizama upenyo wa kutokea! Dj pia aliiona  ile T-shirt ile anataka kumuita Gorii tayari kasharuka jukwaani akajichanganya katikati ya watu huku akiishia.

Baada ya kutoka sehemu ile ilibidi asimame kwanza kutafuta pumnzi! Aliingia hotelini akaomba maji ya kunywa! Kisha alianza kutafuta ramani ya kwenda chuoni aliangalia muda kwenye Simu yake tayari ilikuwa ni saa sita mchana ndio anakumbuka ni muda wa lunch karibia Jolvin atafika pale chuoni.

Alisimama barabarani huku akiwaza anafika vipi chuoni, aliingiza mkono mfukoni wakati yupo anacheza Kuna watu walikuwa wakimletea zawadi alikuta Kama kunae buku buku nyingi alizihesabu ni Kama elfu tisa! Kama kawaida yake alijipigia makofi kujipongeza kwa kazi aliyoifanya huku akipanda hiace za kuunga unga hadi chuoni.

Alifika Getini alikuta kumtulia ilibidi aingie kwa kujificha.

   “” Wewe Gorii!!”

   “” Daaah! Nani tena huyu!?”

   “” Geuka huku! Unavunga husikii!”

Ilibidi ageuke ndipo anakutana na Mwalimu wake alimpokea siku ile darasani.

“” Sir Jacob! Aaa.. haupo darasani leo!?”

“” Mhuu! Sahii ndio waingia chuo! Halafu umevaaje hivyoo!?”

Gorii ndio anakumbuka muda ule atoke kule hakubadilisha ilibidi ajitetee.

“” Sir.. viatu vyangu nilifua Jana havikukauka ndio maana nimevaa hivi! Kuhusu prouva ni baridi tu!”

“” Na sweta la shule nalo bichi!!?”

“” Nililisahau Ofsini kwa Bibi'”

“” Unajua kujitetea Wewe.. haya nenda darasani!?”

Gorii alimtizama kwanza baada ya kuona yupo busy alikimbilia nyuma ya hostel akabadilisha mavazi Kisha aliingia darasani.

Ile anafika darasani alikuta Meza yake imekaliwa na kikosi Cha Ali gang” Aliwatizama kwanza! Alichofanya ni kukaa mezani akawapea mgongo!

Mmojawapo kutoka kwenye kile kikosi alimsukuma Gorii, akawa ameanguka chini. Gorii alinyanyuka akafuta kwanza mikono yake Kisha akatunisha kifua! Aliangalia mkono wake kwenye kiwiko unatoa damu aliifuta ile damu Kisha alimshika mmojawapo ambae kakaa mezani kwake! Akamuinamisha kwenye meza kwa kumgongesha.

Kama unavyojua wanafunzi huwa wanapenda fujo za aina hii! Ikawa kapigwa, apigwe ni kelele mtupu! 

Wale wenzake baada ya kuona mwenzao kagogezwa hasira zikahamia kwao! Japo Gorii alijitahidi kupambana wao walimzidi walikuwa watatu!

Kuna wanafunzi walienda kuripoti Mwalimu akawa amekuja! Bahati nzuri au mbaya ndie Yule Yule aliyekutana na Gorii! Alivyomuona Gorii kabadilisha na mavazi wakati hakuwa vile akajua huyu ndie mkorofi! Walichukuliwa kwa pamoja wakawa wamepewa adhabu toka mchana Hadi jioni wanahangaika nayo.

Waliambiwa kuchimba Dampo la uchafu maana walionesha wanae nguvu za kupambana bora wakapambane na jembe.

Baada ya  muda mfupi kila mtu alikuwa kachoka, Ilibidi stori zianze kupunguza uchovu.

   “” Lakini Ally! Nyie ndie wakorofi mlikaa kwenye kiti changu! Kama msingekaa…. tusingekuwa tunahenyeka hivi.””

Gorii aliongea.

   “” Sasa Wewe Binti gani unapambana na wanaume! Haya yote ni kwasababu yako.

Kijana wa pili aliongea, huku kijana wa tatu yeye aliendelea kuchimba baadae alimuita Gorii.

   “” Wewe si unajifanya mwanaume bhana! Njoo uchimbe si mnataka haki sawa kwa wote!?”

  “” Nimechoka bhana Kaka wa tatu! Halafu Wewe si ulinisukuma Lakini!?”

   “” Hukupaswa unirudishie Sasa!”

   “” Aa.. wee! Nisirudishe wakati umeniumiza. 

Gorii aliamua kulala kabisa make alikuwa hoi taabani, ile kalala pale alianza kuwaza ndio anakumbuka ile Simu ilibidi anyanyuke haraka huku akiwaaga.

“” Nyie “Ali gang” kesho bhana tuonane! Hata hivyo nyie wa kiume!

Ali aliwahi kumrudisha Kisha alimkalisha.

“” Wewe mjanja mjanja Sana! Umesahau tunakuja kukaguliwa! Huoni ukikutwa haupo ni Adhabu nyingine!”

“” Aaa powa bhana! Muwe na huruma muda mwingine Mimi ni wakike hata hivyoo!  Malizieni Chapu tuondoke! 

“” Bora nyie mkitoka hapa Adhabu yenu imeisha.. Mimi ninae Kaka mkorofi huko Nyumbani! Sijui hata nitaenda mweleza Nini leo!?”

“” Gorii njoo uongee na Simu yako hapa!?”

Mwalimu wake alifika pale! Ilibidi achukue Simu! Alisikia Hello! Akajua moja kwa moja ni Jolvin. Aliwaangalia kwanza wenzake Kama wanamtizama akaona wako busy ilibidi asogee mbali kidogo aongee.

“” Samahani leo mchana nilikuwa busy! Sikukuletea chakula! Nilikutumia ujumbe ukaonane na Mwalimu wa darasa nimemwachia maigizo! Ulimuona!?”

Gorii alifikilia jibu kwanza, akagundua kumbe mchana hakuja ilibidi ajibu!

“” Leo tulikuwa busy na masomo sijashika simu!?”

“” Kwahiyo umekula!?”

“” Alitabasamu Kwanza make kala mandazi na jamaa zake muda si mrefu.”

“” Nimekula.!”

“” Okay! Njoo getini nakusubili wanafunzi wenzako wameanza kutawanyika wewe bado tu!?”

“” Nakuja!!”. Kisha alikata Simu.

Mwalimu alimuita ilibidi arudishe simu! 

   ” Adhabu yenu imeisha! Ole wenu mrudie tenaa! Tutawafukuza chuo!”

Gori aliwatizama wenzake, aliwaona wanaelekea bombani kunawa ilibidi awafuate!”

“” Alii… Nywele zangu zimekaa vizuri lakini!?”

“” Wewe sitaki mazoea!! Muulize Khamisi.

“” Mhuu! Sasa ndo umenuna wakati Adhabu imeisha nijibu basi! Unajua sahii tushakuwa marafiki.

“” Na wewe…!?”

“” Ee Mimi.. si tunashilikiana.

Ali ilibidi amtizame vizuri Kisha alimpangusa kulikuwa Kuna mchanga!

“” Upo vizuri.. kakako ndio alipiga? Muwahi bhana..”

“” Khamisi.. mbona wewe husemi nisaidie hata wazo la kuzungumza na Kaka.

“” Kaseme ukweli.”

Khamisi alimjibu mpaka wenzake walianza kucheka. 

     “” Muulize Hussein!? Ali alijibu kwa kumjaribu make aliona Hussein haziivi kabisa na Gorii tayari kamtoa ngeu.

Alimtizama Hussein ambae alikuwa akipikicha majani ya mgomba akiweka kwenye paji la uso, akaona isiwe noma alimfuata.

“” Sisi wote ndio tulitakiwa tupatiwe Adhabu! Make ndio tulileta vurugu! Hapa tumeumia wote! Kesho asubuhi nikumbushe nikupatie dawa ya hicho kidonda!”

Gorii alichukua begi lake huku akiwaaga wenzake akaondoka, alifika Hadi Jolvin alipo! alionekana yupo busy akisikiliza mziki.

   “” Kaka White!!! 

Jolvin ndio anasituka, alimtizama kwanza Gorii huku akimkagua hata yeye alikuwa amemmisi kwa vituko vyake.

   “” Ndio umetoka hivo Nyumbani!?”

Gori alianza kujikagua kwanza akijiweka sawa, Kisha alimkubalia kwa ishara.

“” Hizo nywele hizo…!!?”

Gori akaona isiwe tabu alifungua mlango wa nyuma akakaa.

     “” Kaka white sorry! Nipeleke Nyumbani kwanza leo sitapita dukani nimechoka kweli!”

“” Hapo ndio unakomaa akili! Na wiki kesho hakikisha unaweka ratiba ya kujisomea! Nikiwa nasoma Mimi na Wewe unajisomea!”

Jolvin aliongea pasina kujua Gori huyo! Leo kashinda na pilika pilika hata daftari hajashika.

Baada ya kufika Nyumbani Gorii alipitiliza chumbani kwake! Alifanya usafi wa mwili Kisha alitoka kuanika nguo nje, inaonesha hata kufua alifulia ndani!

Siku hiyo Gorii aliwahi kulala kutokana na uchovu! Jolvin Kama kawaida yake yeye huwa anasoma kwanza! Baada ya kumaliza kusoma aliingia mtandaoni achati na marafiki zake wa chuoni, alikokuwa akisomea walikuwa wamemumisi sana! Waliongea mengi huku wakimuomba kwenye graduation asikose make Huku alikuwa kajiegesha tu hata mitihani alikuwa akifanyia chuoni kwake kwa mara ya kwanza.

Wakati akiendelea kuchati Rich alimtumia video What’sup, alizifungua ndio anakutana na Gorii akicheza, aliangalia Hadi mwisho ndio anaona hata jina kasema ni la Kwake! Hapo ndio alichoka baada ya kuona na zile zawadi alizopewa, wakati anamalizia kuangalia video ile Kuna nyingine tenaa inaingia ni ile aliokuwa shuleni akipigana pamoja na ile akichimba dampoo.

Aliamua kumpigia Rich ambae alipokea simu huku akicheka.

   “” Yaani Broo! Nyumbani tunae Mandoga, mtu kazi! Unaona alivyopambana ulingoni akapigwa na mtu tatu! Bado akaomba pambano na wale jamaa achimbe dampoo! Nakwambia Kaka, Gorii  ni wa kiume, siku ile alipigana na Hammad na leo tena! Mara acheze mziki wa promotion na Tecno! Hivi kunae mwanaume atakaemuoa kweli, au tu akampenda labda nae awe na akili Kama zake ila Hammad waliendana!”

Muda huo Jolvin  alikuwa hata bado hajazungumza, ilibidi amuulize;

   “” Umetoa wapi hizi video!?”

   “” Mimi si mzaliwa wa hapa” ninao jamaa wengi! Si huwa wananiona nipo karibu na Gorii wamenitupia picha nioshe macho! Halafu mwambie Gorii awashe simu! Alijua nitamtafuta Nini!!?”

Jolvin aliamua akate simu Kisha aliiweka pembeni, akimfikilia Gorii”.

   “” Sijui tumuachishe shule.. aanze kunengua kwenye makasino! Make kawa too much kwa kila kitu!”

Aliamua kulala huku akimsubilia asubuhi! Video zote azituma kwenye group la familia What’sup kila mtu akaziona.

Asubuhi yake Bibi na mama pamoja na Jolvin walikuwa mezani wakimsubili Gorii afike.

   “” Bibi muamshe Mjukuu wako! Naona bado anaota michezo ya jana!

Jolvin aliongea huku akimtazama Bibi.

Bibi ilibidi aende chumbani kwa Gorii alimgongea mlango ndio anakurupuka, alikuja kufungua huko akijinyosha mwili auweke sawa’

   “” Ooh! Good morning Bibi’ nimechelewa chuo! Ngoja nijimwagie haraka!”

   “” Usijali Jolvin kakuombea ruhusa upumnzike make Jana ulichoka sanaa!”

Gorii ndio anakumbuka tayari Jolvin kajua ni msala tenaa!

“” Yupo wapi yeye!?”

“” Katoka!!”

“” Hadi mama!?”

“” Eee! Hawapo..!”

“” Hapo sawa..!””

“” Njoo tunywe chai mezani.

Bibi alitoka huku akimsikitikia, sijui hata watamaliza vipi? Gorii alijiandaa haraka akawa amevaa peans jinsi, alipendelea kuivaa Nyumbani na t-shirt.

Ile anafika mezani anakuta watu wote wakimgoja. Alishituka kwanza Kisha aliwasalimia, aliangalia sehemu ya kukaa ilikuwa ni seat imebaki Karibu na Jolvin.

Alivuta kiti akawa amekaa kwa kuogopa ogopa! Muda huo Jolvin alichukua chupa ya chai akamumiminia ni kitu ambacho huwa hafanyi vile! Waliendelea kunywa chai huku stori zikiendelea tofauti na Gorii alivyofikilia sangapi asijisahau akaanza kudakia maada huku akikoleza kicheko.

Walibaki wakimuenjoy kabisa ili asijisikie vibaya! Baada ya kumaliza kunywa chai walitaka ashibe kwanza maada ikaanza.

 Jolvin alishika simu yake akawasha Kisha aliplay video zote akamuonesha Gorii ambae hakuzishangaa ila aliwaza kazipataje Jolvin! 

Hapo hapo alianza kulia Kisha alipiga magoti akiomba msamaha kwa Jolvin.

   “” Gorii sitaki maigizo! Ni hivi nikirudia ule msemo wangu huwa unaniuliza kwanini napenda kusema vile! Tulikabiziwa kuwa wewe ni binti, msitaarabu, unae nidhamu, unaheshimu watu ila Wewe hujiheshimu! Leo unarudi kwenye familia yako ukakae kwanza huko utulie huenda utajifunza!? Ayaa!! Mama ingia…

Gori aligeuka kuangalia Mlangoni alikuwa ni Mama Doreen akiwa na Doreen wamemuijia.

 Bibi ilibidi aingilie kati.

  “” Lakini Jolvin! Mtu huwa anaonywa na sio kumuondoa hivi hivi! Anajisikia vibaya!”

Muda huo Mama Doreen alimuinua Gorii Kisha alimshika mkono huku akimuomba akusanye nguo zake waondoke.

“‘ Jamaniii naombeni mnisamehe kwa hiki kilichotokea! Nashukuru hata kwa muda mliokubali kukaa nae! Leo nitamchukua kwakuwa Mimi ndie nilimchukua kumlea nitaenda kukaa nae mmewangu kaenda kikazi atakaa muda wa nusu mwaka! Nitakua Nishajua jinsi ya kukaa nae nitamrudisha hosteli ikiwezekana!”

Jolvin Alisimama Kisha alimkumbatia mama Doreen!

   “” Afadhari Mama! Wewe mchukue tu! Angalau nitasoma make sio kwa vituko humu ndani! Inatosha hata kwa huu muda tuliokaa nae! Watoto wasiojulikana huwa hawajulikani tu! Ukute kweli hata mamake aliiba zile pesa!”

Jolvin aliongea maneno mengi hata ambayo hakuyastahili ayazungumze! Muda huo Gorii alikuwa pale aliyasikia vizuri! Yalimfanya aanze kulia huku akiichukia familia kwa ujumla aliweka ahadi moyoni mwake hatakanyaga tena katika familia ile!

Alichukua begi lake akirivuta kutoka nje! Bibi alimuwahi amzuie lakini Jolvin aliwahi akamshika mkono akampeleka chumbani kwake”

Huku Mama Rich na Mama Doreen walitoka nje huku wakizungumza.

   “” Ni hasira tu! Naomba mjisikie vizuri, Jolvin anae hasira! Zikimuisha yeye ndio atakuja kumuomba Gorii amrudushe ndio maana nimekaa kimya! Jolvin mwanangu kafata tabia za Babake kweli! Ila Kuna siku zitamuumiza vibaya! Huwa anafanya kitu bila kufikilia lakini baadae hujutia maamuzi yake!”

Gori baada ya kufika nje ya Geti alibaki akitizama ile nyumba! Alikumbuka mambo mengi jinsi alivyopokelewa, furaha waliyompatia lakini leo hii imetoweka ghafra! Alilia Sana huku akimlaumu mamake yote  yanayotokea  yeye ndio chanzo!.

Muda huo Mama Rich alifika pale alitaka kumkumbatia Gorii amuage, lakini Gorii alimgeuzia mgongo hii ikamuumiza Sana! Alijua tayari chuki aliyoisababisha mwanae Sasa imehamia familia nzima kwaaajili ya mtu mmoja leo furaha haipo tenaa!

Gorii siyo haipendi ile familia ila aliamua aisahau kabisa! Alihisi ni kwasababu ya umaskini wake ndio chanzo hata hawamuani Tena, Alimtizama jinsi mama Rich akiwa anarudi ndani kwa unyonge ilimpelekea hata yeye azidi kulia.  Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya 17

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

16 Comments

  1. 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

  2. Henderson Didas on

    Admin uliniahid utaachia mbili leo Ila naona moja tu 💁🏾‍♂️…anyway ila story ni 🔥🔥🔥

Leave A Reply


Exit mobile version