Ilipoishia ”  Wasimbe nyie! Mamako amebaki kula pesa za Mume wangu halafu unakuja kumtafuta Mamako kwangu! Nakwambia na huyo mamako anaendeleza umalaya na waume za watu! Chakula chenyewe ni ugali mboga mboga! Jumlisha hivo Virus sahii tu unaitwa yatima kwa umalaya wa mamako, tena nakupa pole!”

Gorii” alikuwa akikimbia baada ya kusikia Maneno ya Mke wa Mzee Rajab ilibidi asimame huku akiamini kumbe kweli mamake ni Muathirika, hapo hapo alianguka chini akazima.”

Endelea 
SEHEMU YA TATU

 

Mke wa Mzee Rajab alibaki akimtizama baada ya kuona kazima, aliamua kumuacha palepale.

Asubuhi yake ndio kunapambanzuka Gorii” aliinuka pale, aliangalia sehemu ile ndio anakumbuka tukio la Jana lilivokuwa, aliinuka taratibu akijikongoja kuelekea Nyumbani!

Baada ya kufika Nyumbani alikuta mlango umeegeshwa ilibidi aingie ndani akimtafuta mamake baada ya kufika alikuta Kila kitu kipo vururuvuru aliangaza upande wa pili ndio anashituka begi la mamake halipo, ilibidi aanze kukagua kila eneo vizuri lakini nguo hazikuwepo.

Alitoka nje huku akimwangaza mamake Kama atamuona lakini hakuwepo, alirudi tena ndani alitazama mezani ndipo anaona barua imewekwa pale ilibidi aisome.

  “” Binti yangu Gorii” naomba unisamehe kwa maamuzi niliyochukua, najua unapambana ili Mimi mamako niishi vizuri, ninachokuomba binti yangu olewa na Hammad make familia yao wanayo pesa itakufanya uepukane na umaskini hata hilo jua halitakuunguza tenaa!”

Aliweka kituo kwanza huku akifikilia neno kuungua na jua ndio lililizidi kumchanganya zaidi, yeye alilichukulia Kama anaonewa huruma na wakati hapendi, Kuna maswali alikuwa akijiuliza mamake atakuwa wapi sahii.

Majibu aliona yatakuwa kwenye barua make alikuwa hajamalizia kusoma.

   ”’ Kuhusu Mimi mamako nimeamua kwenda mjini kutafuta kazi! Hata Mimi bado Nina nguvu za kupambana!”

Gorii” aliishia kusoma mwisho pale, akili yake iliwaza ni sawa kaenda kutafuta kazi jijini Dar! Na vipi Kuhusu hivo vidonge na afya yake itakuwaje? 

Alianza kupaki nguo kwenye begi lake la mgongoni alikuwa ameliandaa muda mrefu atatumia kusafilia akienda mjini.

   “” Mama nitakutafuta muda wote popote utakapoenda nami nitakufuata!”

Alifungusha Kila kitu kilicho ndani akifunga mafurushi, Kisha alifunga mlango kuelekea kwa kina Muddy.

   “Gorii” mbona mapema hivi umebebelea  begi! Leo unasafiri?”

Mamake Muddy Alihoji huku Muddy nae akitokeza nje. 

   “” Gorii” ndio wakimbia kuolewa na Hammad?”

Goryanah ilibidi amvute Kisha alimsogeza kunako banda la kuku aongee nae!

   “” Muddy sikia!! Mama kaenda mjini kutafuta maisha, kaondoka na nguo zake! Ninachotaka kumwambia hii hapa funguo utakuwa waenda kupaangalia Nyumbani, naenda kumtafuta mama mjini ila nitawahi kurudi.”

   “‘ Aaa a! Gorii” we baki uendelee na biashara mama atarudi tu! Kwani lazima umfuate!?”

  “” Hapana Muddy! Wewe niamini Mimi nahisi mama bado hajafika mbali kwasasa! Halafu nahisi mamangu anae ugonjwa mkubwa huwa anameza dawa nyingi!”

Muddy alibaki akimtizama kwa mara ya kwanza alimkumbatia Gorii” alimkumbatia pia huku wote wakibaki kulia! Muddy alimuachia Kisha aliingia ndani alirudi na kiasi Cha pesa Kama elfu kumi.

   “” Hii hapa itakusaidia kumtafuta Mama! Najua mjini bila hela huwezi kuishi!”

Goryanah alipokea ile pesa Kisha aliweka kwenye begi, alimuaga tena ili aondoke lakini alisikia sauti ya Mamake Muddy ilibidi ageuke kumtizama

Alimfuata na kumkumbatia, kumbe maongezi yote mama aliwasikia, Mama alifungua kitenge chake kwenye pindo alikuwa Kama na elfu Saba alimpatia huku akimtakia Kila la kheri katika Safari yake.

Huruma ya mama Kama mama ilimuuma Sana hasa akimtizama Gorii” ni binti mdogo hajui ataendesha vipi maisha akiwa mjini.

   ‘”‘ Mama unauhakika kweli Gorii” atampata Mamake”  Lile ni jiji kubwa anaweza kutana na wahuni wakamlagai!”

Mama Muddy aliamua kumshika mkono kijana wake huku wakiingia ndani, ukimya ulitawala walibaki wakitazamana kwanza huku Kila mtu akionesha kukosa furaha Ghafra!

 

   “” Mamaa! Hivi Mama’ke Gorii” anae magonjwa mengi, make kanambia anazo dawa nyingi anatumia.”

Mama alishituka Kwanza inaonesha alikuwa akifahamu maradhi ya Mamake Gorii”.

     “” Wewe Nani kakwambia haya yote!?

“” Ni Gorii”

“” Gorii…!!?”

“” Kaniambia kipindi kaniita kule nyuma! Nahisi hizo dawa aliziona!

Mama alipata kikohozi kwanza, Muddy alimletea maji ya kunywa Kisha aliondoka kuelekea nyumbani kwa Gorii make alikuwa haamini kama kweli kaondoka.

Huku kwa Goryanah alikuwa tayari yupo kwenye Basi akielekea jijini Dar es salaam, siku hiyo alipata siti ya dirishani ilikuwa ni kukenua kutizama mazingira muda wote.

Majira ya jioni ndio wanaingia ubungo, baada ya kufika stand walishuka, kimbembe kilianza kwa Gorii” wapi ataenda? Alitizama vijana waliokuwa wakiuza vinywaji ilibidi awaulize sehemu ya kulala Kuna wakaka wawili walijitokeza huku wakimuomba wampeleke nyumba za wageni.

Gorii” aliwashukuru kwanza Kisha aliondoka nao walipita Kama mitaa miwili, walipofika kule mbele ilibidi wasimame kwanza huku wale vijana walirudi nyuma baadae walipeana ishara, muda huo huo wakamgeuka Gorii” mmoja alikwapua begi Kisha mwingine alichukua Simu wakaishia mtaani, Gorii” alianza kuwakimbiza lakini wapi, mwisho kabisa alichoka aliamua kukaa chini nakuanza kulia.

   “” Haya yote ni kwaaajili yako Mamaa! Upo wapi kwani ona Mimi binti yako nazidi kuhangaika peke yangu!

Wakati amekaa alisikia king’ola kinapita ilibidi akimbie huenda Kuna msaada, ili kutokeza tu alikamatwa na police kwa uzururaji ovyo akawa amebebwa kwenye tenga. Walifikishwa police walipatiwa kichapo Cha nguvu kilimfanya azidi kuumia zaidi.

Kesho yake asubuhi walitolewa selo Kisha walianza kuhojiwa, wale wenzake wote walitolewa na ndugu zao ikabakiwa yeye akihojiwa.

   “” Binti unaitwa Nani?

   “” Gorii!!!”

   “” Kwa kilefu nanii!!?”

   “” Gorii Goryanah!””

   “” Babako Goryanah ndie Baba?”

   “” Ndie Mimi!”

Askari aliahirisha kumhoji kwanza make alijua binti hakunemo, Kuna Askari mmoja alimuuliza.

   “” Unaishi kwa Nani au upo mtaa gani!?”

   “” Sina makazi maalumu, siku nikimpata mama ndio nitajua naweka wapi makazi!

Kuna mama mmoja kati ya wale Askari aliamua kumchukua Gorii” ili amhoji vizuri, Gorii” na yeye alimwelezea Kila kitu, mama Yule alimuonea huruma alimuahidi atamsaidia kumtafuta Mamake.

Siku hiyo Gorii alichukuliwa kupelekwa kwa Yule mama, alimpatia hifadhi alikuwa akiishi kwenye jumba zuri la kisasa!

Ilipita Kama mwezi mmoja Gorii” alikuwa ameanza kubadilika rangi yake ya asili ilionekana vizuri make alikuwa ni maji ya kunde.

Kwaujumla alianza kuzoea kazi za pale Nyumbani huku akisaidiana na mabinti wenzake pamoja na mdada wa kazi, baada ya kumaliza majukumu yake aliomba ruhusa angalau akamtafute mamake tenaa make mji alikuwa tayari kauelewa, siku hiyo alitafuta Kila sehemu hakufanikiwa mwisho kabisa alirudi Nyumbani akiwa ni mnyonge.

Wakati anaingia ndani alikuta familia imechangamka, kumbe ni baba wa familia amerudi, siku hiyo aliwaletea binti zake zawadi, Gorii” alipofika sebuleni ilibidi asalimie kwanza Kisha alielekea kunako chumba chake, angalau akapumzike!

  ‘We wee wee! Ni Nani Wewe unaingia kwenye nyumba yangu halafu huna wasiwasi kabisa unazama tu, hebu njoo hapa haraka!”

Ilikuwa ni sauti ya Baba iliyomfanya asimame make ilikuwa Kama inamfokea, aligeuka ili amjibu lakini alikumbuka Kuna Maneno alikuwa akimwambia mamake.

   “” Hupaswi kuzungumza na wakubwa pale wanapokukosea angalia kwanza chanzo ni Nini ndio ufungue kinywa chako.”

   .. .. Itaendelea Usikose Sehemu ya Nne ….. 

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

 

14 Comments

  1. Kijiwe kimechangamka Sana uuwhiiiii good job 💕💕💕💕💕.
    Mwenzioooo nimekupenda bureeee💜🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Leave A Reply


Exit mobile version