Ilipoishia

Goryanah ilibidi amsine mguuni kwanza Kisha walianza kurushiana majani wakikimbizana, lakini kwa bahati mbaya wakati Gorii” anarusha yalimuangukia Jolvin kichwani na mengine usoni. 

Jolvin ilibidi asimame kwanza make alikuwa haoni, alinyanyua mkono wake kwanza ili afute kwa bahati mbaya tenaa Simu yake ilianguka chini, Rich baada ya kuona vile ilibidi akimbie huku msala ukibakia kwa Gorii’

Endelea 
SEHEMU YA SABA 

Gorii” alitizama pembeni alimuona Esau, Joely wapo busy kusoma, yeye akazani hawajaona kumbe walivunga ili waone kinachoendelea pale.

    “” I’m sorry Kaka White! Ni mis understanding tu! Hata hivyo Simu haijapasuka.

Jolvin alikaa kimya huku akiwa amefura hasira! Akifikilia mambo anavyoyafanya kitoto kitoto halafu analeta kuongea kingeleza.

Gorii” hata hakujali alinyanyua mkono ili aendelee kumfuta lakini Jolvin aliurudisha ule mkono akiukunja. Gorii” ambavyo hasikiagi alirudia tena kuweka huku akimtolea, Kisha mkono wake wa pili alimshika akimsogeza sehemu nzuri amkalishe huku akiendelea kumtolea majani, baada ya kumaliza alijipigia makofi huku akimuomba afungue macho.

   “” Kaka White! Ila Mimi ni Bora kuliko hata Rich aliyesababisha matatizo, halafu sahii kakukimbia!

Huku kwa Esau na Joely! Walibaki wakicheka kimya kimya, Rich nae hakuwa mbali alikuja kuungana nao.

  “” Yaani leo nilikuwa nakula Kofi moja mpaka kuanguka! Najua Gorii” akitoka hapo atakuwa na hasira na Mimi! Lakini angalau kalisovu hilo!”

Esau na Joely walicheka Kisha walimpatia Ishara Rich ajifiche make Jolvin anamuangaza muda wote!

   “” Daaah! Nimekwisha kumbe bado natafutwa tu!?”

Jolvin alimuona Rich anavokimbia alimuita kwa sauti Kali arudi.

 

Ilibidi Rich aje taratibu huku mikono kaiweka nyuma alikuwa mnyonge kweli, Gorii” alimtizama akawa amegundua hilo! Jolvin alinyanyua mkono wake ampatie Kofi lakini Gorii” aliudaka Kisha aliuelekeza shavuni kwake.

   “” Kaka White…!! Wewe huwa hujui bahati mbaya!? Unazani Mimi na Rich tulipanga tuje tukumwagie majani usoni? Tulikuwa kwenye michezo wewe Ndio ukatokea ukapita mbele yetu! Hiyo si bahati mbaya tu!? Basi nipige Mimi make mikono yangu ndio ilikumwagia nyasi!”

Jolvin ilibidi atoe mkono Kisha alishusha pumzi ndefu akiwa ameshikilia meza waliokuwa wakiitumia Rich na Gorii”

Esau na Joely baada ya kuona imekuwa msala ilibidi wasogee karibu, walimruhusu Rich na Gorii” waondoke Kisha wao walibakia na Jolvin.

“” Hapana amezidi huyu Mjukuu wa Bibi! Muda wote hasira! Sijui Nani kumuuzisha kiasi hicho!

Gorii” alikuwa akilalamika huku akiwa na Rich, ilibidi kila mtu aingie chumbani Kwake! 

Kitendo Cha Rich kukoswa Kofi na kakake kilimuuma Sana! Aliamua kuchukua nguo zake akapaki kwenye begi dogo la mgongoni Kisha alilala.

Asubuhi kulipokucha alienda kumgongea mamake chumbani Kisha alimuaga, huku akiaga kuwa anaenda kwa rafiki yake anae birthday! Mama alimruhusu.

Huku Chumbani kwa Jolvin alikuwa akichungulia dirishani! Kwa mbali alimuona Gorii” akiruka kamba ilibidi acheke kwanza.

   “” Zoezi la kuruka kamba ndio uuzuie mkono wangu kweli! Ayaa… Ngoja tuone Hadi mwisho, Nani mshindi?”

“” Ooyo Jolvin..!!”

Esau alibisha hodi.

   “” Wewe ingia bhana! 

 

   “” Tunaogopa kuingia kiholela humu chumbani, make hupendagi mtu aingie.. !”

 

“” Wewe sema wataka Nini!?”

“” Sabuni.. naona nimeishiwa kwangu!”

“” Huwa si shei..!”. Au Ngoja kwanza kumbe Kuna hii mpya sijaitumia! Usinirudishie.”

Esau aliondoka, lakini Jolvin aliendelea kukumbuka siku ya Jana kidogo amshushie Kofi mdogo wake! Asingekuwa Gorii” lingemfika.

Alitoka ndani huku akiwa amevaa pensi na singled akielekea chumbani kwa Rich! Alifika akagonga mlango lakini kimya aliamua kuingia huku akikagua chumba chote kilikuwa kimya! Mwisho kabisa aliingia bafuni kumuangalia hakukuwa na mtu pia.

Huku kwa Gorii” baada ya kumaliza kazi aliamua kuja chumbani kwa Rich! Make kwenye mazoezi hakumuona! Alijua itakuwa kaumizwa na hasira za kakake, akaona budi amjulie khari yake.

Alifika Mlangoni akaita kimya mwisho kabisa aliingia ili ajidhihilishie Kama hamnae mtu ndani! Muda huo Jolvin anatoka bafuni huku kaweka singled yake nyeupe  begani, nahii ni baada yakugusa uchafu toka bafuni akaamua kuivua kabisa make alihisi Kama inazidi kumchafua.

Ile anafungua anamuona Gorii” yupo busy na kioo akijitizama huku akibana nywele yake, Jolvin ilibidi amsogelee Hadi Karibu na mgongoni Kisha alishika mkono mmoja ukutani.

    “” Hivi ndivyo ulivyosifiwa kuwa Gorii” ana nidhamu, ana akili, ana heshima! “” Sijui hii kuingia kwenye chumba Cha wanaume bila ridhaa yao hii tuiweke upande ganii!?”

Gorii” ndio anageuka vizuri amtizame huenda alihisi, kile kioo ukijitizama Sana kinakuvua nguo ilibidi ahakikishe kwanza make Kuna taswira ya mtu, na mtu kamili! 

Ile anageuka ndio wanakutana uso kwa uso na Jolvin! Alichofanya ni kufunga macho yake na mikono huku akimwambia avae ndio afungue.

Jolvin alimwangalia Kisha alicheka Sana, akaona ili kumkomesha nikumchezesha akili yake ili awaogope wanaume hasa upande wake! Make kamzoe kweli hata hamuogopi!

“” Nipe Dakika tano nivae! Ndio ufungue macho yako!!”

 

Alirudi Hadi kunako mlango Kisha aliurudishia ndio akarudi Hadi kwa Gorii”

   “” Fanya ukae kwanza! Make ukifunga macho muda mrefu utaanza ona kizunguzungu! Ukaanguka!

Alimshika mkono Kisha alimkalisha kwenye sofa! 

   “” Kaka White! Bado tu..! Mama ananitafuta niende jikoni sahiii!”

Muda huo alisikia sauti ikimuita kweli alikuwa ni Dada wa kazi akimuita! Gorii” alitaka kuitika lakini Jolvin alimuonya Kisha yeye alijibu.

   “” Mbona kelele! Asubuhi asubuhi watu wamepumzika kamtizame garden!”

Dada ilibidi aondoke japo aliona Kama Gorii” kaelekea kwenye hiko chumba, akahisi ni wenge lake tu.

Gorii” baada ya kushiba tu, alianza maneno yake.

   “” Hivi Rich wewe ndie umesema nisiende kusema kuwa ulikuwa out na mwanamke! Vipi lakini anaitwa Nani? Na unae mpango wa kumuoa!? Isiwe unamchezea tu.

   “” Ushaanza maneno yako ee! Anaitwa Sophia! tuna malengo ya kuoana!”

Gorii” ilibidi acheke kwanza Kisha alimsogelea kwa ukaribu.

   “” Hapo ulipo upo mnadanganya Dada wa watu unamuoa! Hivi inakuja kweli hiyoo! Bado hujaenda chuo, huna kazi na pesa hujapata bado! Hivi itawezekanaje kwanza!!?”

   “” Wee! Kama anakupenda kweli lazima akusubili! Siku zote kwenye upendo wa kweli, kusikilizana, kuaminiana, kuvumiliana hiki ndio kiunganishi!”

“” Sawa’ mwalimu wa Mahusiano japo bado mdogo Sana!”

“” Hivi Gorii” wewe huwa unanichukuliaje Mimi! Mimi sahii naweza kuwa na familia! Hata Wewe naweza kukuoa na kukuzalisha pia!”””

“” Basi… Basi… Make unaleta maada za kijinga hapa!

 

Wakati wakiwa wamekaa Kuna vijana watatu walifika pale! Ile Gorii” anatizama vizuri alimuona Hammad ilibidi ashituke kwanza.

“” Hammad! Wewe tenaa!!?”

“” Yaah! Mimi Ndio! Umenikimbia kule kijijini! Nilikuulizia  kwao Muddy, na ndie kanambia upo mjini! Kuna siku nilikuona ukiwa na familia ya Mishoki nikajua kabisa waishi pale! Ila umepiga hatua kuondokana na umaskini.”

Gorii” alishusha pumzi kwanza hakuna kitu kinamuuma kusikia kakaa kwa mtu ili aepuke umaskini na hiki ndio kitu kinampatia ujasiri wa kupambana zaidi.

   “” Kipi wakitaka kwangu!!?”

   “” Mamako anadeni kwetu, alikuwa akikopa pesaa kwaaajili ya mtaji! Hapa katoweka kijijini akiwa na deni! Kama tumekupata wewe Basi utalilipa, na ukishidwa kulilipa kubali nikufanye mke wangu Ili tuishane.”

   “” Mama alikopa lini tenaa!? Wakati hakuwa na Deni au alirudi tena kijijini kukopa!?”

  “” Mamako alirudi Kijijini Kama wiki moja baada ya kuondoka, alichukua laki mbili akidai ni pesa ya matibabu! Baba akamuonea huruma kutokana na khari yake aliokuja nayo! Na Mimi nilimpigia debe apewe kwasababu yako tu, Nakupenda”

Neno Nakupenda likamfanya Rich acheke kwanza, kumbe Gorii” huwa anavunga kumbe anae bwana.

   “” Nawewe unacheka Nini!!? Wazani huyu ni Bwanangu’ make akili yako na yeye ni kitu kimoja!”

   “” Ushaanza kunilinganisha na hii level ya poli Mimi! Ila nimeamini Mungu humpa wakufanana nae! Ila kwasasa haufanani nae make wewe kwasasa ni familia ya Mishoki! Ndio maana upo na Mimi!”

Rich alimtetea mpaka Gorii” alifurahia na kujipa kiburi, 

“atafanya Nini huyo Hammad?”

 

Alimsogelea Karibu Kisha alimnong’oneza sikioni.

   “” Ukinigusa Mimi ndio umegusa familia nzima ya Mishoki! Kwahiyo kuwa makini!”

Hammad alisogea nyuma kidogo Kisha aliwapatia Ishara wenzake kilichofuata hapo ni kelele tupu huku wakipeana vipigo vya kufa mtu, baadae Hammad aliwanong’oneza wenzake wakatoka haraka haraka . Nini Kitaendelea Usikose Sehemu Ya Nane

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

7 Comments

  1. Samahan nilikuwa naomba tu 😁 hauwez weka stry in audio maana daahnakuwaga kavivu kusoma lkn nazipenda kinyama

Leave A Reply


Exit mobile version