Ilipoishia Ilikuwa ni sauti ya Baba iliyomfanya asimame kwani ilikuwa Kama inamfokea, aligeuka ili amjibu lakini alikumbuka Kuna Maneno alikuwa akimwambia mamake.

   “Hupaswi kuzungumza na wakubwa pale wanapokukosea angalia kwanza chanzo ni Nini ndio ufungue kinywa chako.”

Endelea

SEHEMU YA NNE – 04

 

“” Baba! Huyu anaitwa Gorii” ni Dada yetu kaletwa na Mama aje kuishi hapa! 

Doreen aliongea na kumfanya Babake amtizame Kisha alimwangalia tena Gorii”

   “” Basi nenda nitaongea na mama yenu, ataniambia ukweli!”

Gorii aliingia Chumbani Kwake yeye muda wote alikuwa akimuwazia mamake atakuwa wapi! Hata Yale maneno ya Baba alichukulia kawaida tu! 

Majira ya usiku akiwa amelala mamake mlezi alifika kumgongea Ilibidi afungue.

   “” Mama mbona usiku Sana upo hapa?

Gorii” Alihoji lakini mama aliishia kumshika kichwani akimtoa wasiwasi.

   “” Kama utaendelea kukaa hapa! Hutampata mamako kwa uharaka, nimepanga kesho utaenda kukaa kwa rafiki yangu huwa anaishi yeye na binti yake mmoja watoto wengine huwa wapo shule! Nishamweleza Kila kitu nahisi atakusaidia kumtafuta Mamako hata Mimi nitakuwa muda wote nipo na wewe!”

   “” Lakini Mama… Mimi Yule sijamzoea nimezoea familia hii, sijajua hata atanichukuliaje kwa hizi akili zangu!”

Mama aliishia kucheka kwanza, kweli binti yake akili yake anaijua vizuri anae wenge la nguvu aliamua kuondoka tu.

Gorii alikuwa na akili nyingi Sana alianza kuhoji kimya kimya mbona imekuwa ghafra Sana aambiwe ahame, alijiongeza Huku akijua chanzo ni mapokezi ya Baba mwenye nyumba ndiyo kaamua vile, aliplan siku ya kesho yake ataenda kuongea nae ili asiondoke tu.

Asubuhi kulipopambazuka Gorii” aliamka asubuhi Sana, alifanya kazi zote Kisha aliweka chai mezani, ile familia inakuja kuamka asubuhi wanashangaa kazi zote zimefanyika na chai ipo mezani.

Mama Ilibidi aingie Chumbani kwa Gorii” angalau ampongeze, baada ya kuchungulia kwanza Ilibidi abaki akimtizama Gorii anavyofanya maigizo akitembea tembea chumba kizima.

   “” Aaa! Hapana, hapo nimekosea.. nitamsalimia kwanza Kisha nitamletea jusi anywe,,, aaa…  Hapana! Nitamsalimia Kisha nitamwambia, “” Baba I’m sorry! Jana nilikuwa na mawazo nilipokuwa napita sikukuona vizuri! Ndio maana nikakupita pasi pasipo kukuongelesha! Kwahiyo nisamehe sitarudia halafu nipe adhabu yeyote na sio nikakakae kwingine! Nivumilie nimpate mama kwanza!”

Goryanah alimaliza kuongea Kisha alijipigia makofi akiamini mtihani kaufaulu! Lakini alisikia upande wa pili Mama akimpigia makofi, upande mwingine tena ni Doreen alikuwa akichungulia dirishani alicheka na yeye, Kisha alizunguka akaingia ndani.

   “” Mama lakini kwanini usimuache Gorii” akae tu hapa Nyumbani unajua tumemzoea Sana! Halafu leo kafanya kazi zote mwenyewe, nyumba inavutia ujue! Si baba ndio kasema Gorii” hamuamini lakini sisi tunamwamini mama, acha akae tu.”

Kwa maelezo ya Doreen ndio yalimfungua macho Gorii” alijua kabisa kumbe shida ni kutokumuamini tu, kwanza alishuka kitandani kama karushwa na remote, huyo nduki Hadi sebuleni baada ya kufika alimuakia Babake kwa heshima, muda huo alikuwa ananyanyua kikombe anywe chai, Gorii” alimsitopisha kwanza Kisha alichukua kile kikombe akanywa chai iliyokuwemo,  baada ya Hapo alishusha tenaa huku akimpatia Mzee anywe..

   “” Samahani Baba! Wewe kunywa tu! Najua huniamini ndio maana nimefanya kunywa chai yako kabla usije ukanisema nimeweka sumu!”

Doreen na mamake walibaki kucheka tu, make vituko vya Gorii” Kila kukicha vilikuwa haviishi.

Lakini Baba Yule alibaki akikitizama kile kikombe, kwa roho mbaya alikitamiza chini Kisha alisimama aondoke lakini Gorii” aliwahi akamshika mkono huku wakimtizama jicho kwa jicho.

   “” Lakini Baba!! Nimekosea Mimi na sio kikombe hiki! Hata kyenyewe kimeumia ndio maana kimepasuka! Halafu ulipokitupia sio sehemu salama muda wote kinaweza kukuchoma wewe kwa hasira kilichonacho.”

Baba alimtiza tena Gorii” Kisha alimtoa mkono uliokuwa umeshikilia mkono wake, alimpatia ishara huku akimsontea kichwa chake kwamba hamnemo.

Gorii hakujali, aliinama akawa ameokota vile vipande vilivonjika na kwenda kuvitupa kwenye ndoo ya uchafu!

Mama alimuonea huruma Sana huenda anapitia wakati mgumu, kuliko hata yeye lakini binti wa watu hajali kuhusu hilo, Ilibidi amfuate Kisha aongee nae.

   “” Gorii jiandae basi tukamtafute mamako! Kuna taarifa zimetoka Kuna wamama wajane wanahitaji msaada!

Gorii kwa mamake tena! Dakika tano ni nyingi alienda kubadilisha nguo siku hiyo alivaa gauni lake Zuri kweli Kisha waliondoka.

   “” Huenda Mamangu anapitia wakati mgumu kwasasa! Atakuwa kaenda kuomba msaada kwa watu wenye roho nzuri!” Gorii alimuuliza Ma Doreen!

   “” Usijali siku tukimpata ataishi vizuri!”

Walielekea sehemu Kunae tajiri mmoja alikuwa maarufu Sana, alijitolea kugawa msaada kwa watu wasiojiweza! Gorii baada ya kufika pale aliuliza wale walinzi Kama Kuna usajili wa jina la mamake.

  “” Mamako anaitwa Nani?

  “” Nelisha Magai!”

Muda kidogo mlinzi alimwangalizia kwenye orodha Kisha alirudi  na majibu kwamba hakunae jina hilo.

Gorii alivunjika moyo Alibaki amekaa huku akijawa na wasiwasi Sana huenda hata mamake alikufa muda mrefu! Ma Doreen alimfuata Kisha alimshika mkono huku akimpeleka kwenye gari, siku hiyo hakutaka kumpeleka nyumbani make nako hakukaliki. Aliondoa gari yake kuelekea kwa huyo rafiki yake( Mama Rich ) angalau wapate chakula kule.

Baada ya kufika Gorii” alibaki kwenye gari akiamini mamake anaenda kuonana na mtu Kisha angemkuta kwenye gari, lakini mama alimuomba ashuke kwenye gari Kisha waondoke wote!

Baada ya kushuka Gorii” alibaki akitizama jumba lilivokuwa kubwa halafu linae wafanyakazi wengi alibaki kushangaa, walipitiliza moja kwa moja Hadi sebuleni.

Kuna mama aliingia sebuleni, kwa muonekano ilionesha ndie mama mwenye nyumba, lakini alikuja ameambatana na Bibi mmoja akiongozana nae walikaa kwa pamoja, Gorii ilibidi awasalimie Kisha alikaa kimya, waliletewa kinywaji huku msosi ukizidi kuandaliwa.

Kwa Gorii muda wote alikuwa akimtizama Yule Bibi Kisha anampatia ishara kupitia mkono baadae anacheka, Ma Doreen alimuona Bibi anacheka ilibidi amtizame anaecheka nae, ile kumtizama Gorii” akavunga Kama hakuna kinachoendelea.

Ghafra Kuna kijana aliingia huku akipiga makofi kuelekea kwa Bibi yake aliongea.

   “” Naona Bibi amepata mjukuu wa kufanana nae! Muda wote anacheka nae!”

Wote walimtizama Bibi lakini Bibi alibaki kufurahia zaidi, Gorii” ndio akauchuna maziwa. 

   “” Rich wamaanisha Nini? Mjukuu yupi huyo!?”

Mama Rich ndio Alihoji, make Rich pia ni mwanae.

Rich alifanya kumsonta Gorii” kwa kidole.

   “” Yule pale mjukuu!”

wote waligeuka kumtizama Gorii”

   “” Hapana sio Mimi! “Mjukuu wa Bibi kakosea”

Ilibidi wacheke kwa pamoja huku wakizidi kumtizama Gorii”.

   “” Mama Rich.. nilikwambia Gorii” ninaekaa nae ndio huyu! Yaani muda wote haishiwii vituko! Huwa ni mcheshi Sanaa!”

   “” A aaa!! Lakini mama Mimi sitakaa hapa! Lazima turudi wote Nyumbani!”

   “” Gorii” familia niliyokwambia utakaa nayo ndio hii, huoni wanavyokupenda!”

   “” Haikuwa makubaliano yetu..! Uliniambia ninae mama mmoja na binti mmoja mbona ni wengi hivyoo!?”

   “” Nilikwambia vilee lakini nilitaka kukuondolea hofu ila ndio hii!”

Bibi Alisimama huku akimfuata Gorii aseme nae, ile kusimama mguu wake ulikuwa umekufa ganzi, alitaka kuaanguka lakini Gorii” aliwahi kumdaka, mpaka watu wote wakabaki kushangaa, “” mbona ni binti wa ajabu Sana!”

   “” Sorry Bibi!!” Huku akimkalisha taratibu kwenye kiti.

   “” Mama twaweza kuondoka sahii! Itakuwa Doreen anatuulizia Sana!

   “” Lakini Wewe mjukuu wa Bibi! Si ubaki tu! Tulisikia Kuna binti ataletwa hapa! Angalau awe anakaa na Bibi kumliwaza make Bibi yangu ni mgonjwa.

Rich aliongea, alimfanya Gorii” amtizame kwanza huku akifikilia.

   “” Kumbe  kukaa hapa ni kwaajili ya Bibi na si kumtafuta Mamangu!? Wanaleta utani hawa.

   “” Gorii” mwelewe Basi kakako! Hii familia ndio itakusaidia kuitafuta familia yako pamoja na Mama.

Gorii” Alisimama kwanza Kisha alizunguka huku akitizama mazingira ya pale Kama Kuna usalama kwanza, Kisha alimsogelea Mamake Rich akamuuliza.

   “” Je, utanichukulia Kama Mtoto wako Kama Ma Doreen anavyonichukulia Mimi!?”

Mama Rich aliishia kumshika shavu Kisha alimkumbatia.

   “” Ninajua thamani ya kuwa mama!”

Aliongea maneno machache tu, lakini ndani yake yalikuwa na maana nzito.

   “” Kwahiyo utabaki na familia hii?  Familia yetu inajulikana Kama familia ya Mishoki house! Je upo tayari kuishi na hii familia?”

Gorii alikuwa Kama haelewi alimtizama Bibi upande wa pili muda wote alikuwa akimpatia ishara akubali, akikataa atajiua.

Kabla hajakubali alimsogelea Bibi kwanza Kisha alimshika mkono huku akipaza sauti.

“” Kwaajili ya Bibi nitakaa hapa!”

Wote walipiga makofi kumpongeza kwa maamuzi aliyochukua.

Mama Doreen ilibidi akae nae pembeni angalau amuachie maneno kadhaa yatakayomjenga.

   “” Gorii! Najua Wewe huwa una moyo safi, naimani kupitia Wewe familia hii utaifanya iwe na furaha Kama ulivyotufanyia sisi! Sina maneno mengi ya kuongea make najua nidhamu huwa unayo! Pia ni mtu wa kujiongeza! Kuhusu mama tutampata tu, kikubwa makazi kwanza ndio kitu muhimu, hata mama naamini yupo anatafuta makazi ya kukaa, kana Wewe umepata hifadhi hata mama nae kashapata hifadhi amebakiza jambo moja tu, nikukutafuta Wewe!”

Gorii” alibaki akidondosha chozi Kisha alimkumbatia mamake kwa furaha kabisa! Ni mama mwenye upendo wa dhati, alihisi hata huo moyo utakuwa ni Mamake.

Baada ya kumaliza maongezi walirudi sebuleni, Gorii” alitembezwa nyumba nzima ajue mazingira pia alipatiwa chumba chake kwaaajili ya mapumnziko.

Mwisho kabisa walikaa mezani wapate chakula Cha pamoja. Mama Doreen aliomba kuondoka huku akimwahidi Gorii atamletea nguo zake. 

  .. .. Itaendelea Usikose Sehemu ya Tano ….. 

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

 

21 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version