Utangulizi: 

Katika dunia hii kila mtu amekuwa akiuchukia umaskini, na familia zisizokuwa na uwezo nazo zimekuwa zikifedheheshwa na watu matajiri wakiamini katika jamii hawana mchango wowote! Leo tunakutana na binti aitwae GORYANAH kwa kifupi muite (GORII )ni binti shupavu mwenye umri wa miaka kumi na saba anaishi na mamake mzazi pekee kwani Babake alipoteza maisha ikiwa bado ni binti mdogo.

Mamake huwa anauza mbongambonga analangua kwa wakulima kisha anampatia binti yake kutembeza mtaani huku yeye akiendelea kuchoma vitumbua nyumbani kwake ilimradi wazidi kuzichanga shilingi. Ndoto kubwa ya binti Goryanah aliamini ipo siku atauepuka umaskini katika familia yake kama ataongeza nguvu katika kupambana, fedhea kwa mamake kuitwa “msimbe” zitaisha endapo watapata pesa nzuri!

 

SONGA NAYO… SEHEMU YA KWANZA

Huku mtaani Goryanah alikuwa akizidi kutembeza mboga mboga! Jua nalo halikuangalia kuwa binti huyu anapitia wakati mgumu liliweza kuangaza zaidi misiri ya Moto uwakao.

Goryanah alifika kwenye mti mkubwa uliokuwa na kimvuli aliamua kutua hapo, huku akichukua chupa yake ya maji angalau anywe! Wakati akiwa anamalizia kunywa alisikia sauti ikimuita kwa nyuma ilibidi ageuke.

“” Mudy! Ulijuaje kuwa nipo hapa!

“”Dada Gorii!!” Siku ya leo naona biashara ni ngumu! Nimejaribu kutembeza matunda hutaamini watu hawanunui! Hapa nawaza labda twende stand angalau tutauza!?” Goryanah Alibaki akimtizama, Kisha alimpatia chupa ya maji anywe.

“” Utakuwa na kiu Sana mudy! Ila na wewe unisaidie, Mimi na njaa huwezi kunipatia hata ndizi mbili tu nikapunguza njaa?

“” Aaah! Dada Gorii” unajua huwa wanisaidia sana! Mimi nikikutana na wewe naomba uchukue tu! Kuhusu mama nitamwambia ziliharibika!”

 

Goryanah aliishia kucheka huku akichukua zile ndizi na kuanza kula, baada ya kumaliza kula ilibidi amgeukie.

“” Lakini mudy! Mi kwenda stand haitowezekana! Mimi nauza mboga mboga! Stand wamejaa wasafiri hawawezi kununua! Fanya hivi wewe nenda ukatembeze stand, Mimi naingia mtaani! Jioni tukutane hapa ili tuaangalie mahesabu Kama tutakuwa tumefanikiwa!

“” Sawaa! Kuwa makini Dada” halafu usipite zile chocho unazopitaga Kuna wahuni huwa wanakuwinda!”

“” Usijali, Goryanah ni binti jasiri! Anapambana na watu waovu siku zote! Kuwa makini hata wewe wasikunyanganye matunda pamoja na pesa.

Huku mtaani Goryanah alikuwa akizidi kutembeza mboga mboga! Kuna wamama walikuwa wakisukana walimuita akawa ameenda.

“” Wewe Binti wa Ma’ Goryanah! Naona unamsaidia mamako mlipe Kodi! Kazana make hii mabibo mtazidi kuhama hama muda wote!

Ni mama mmoja aliongea huku akizidi kuchagua mboga mboga, upande wa pili kulikuwa kunae kina mama wawili wakizidi sukana, walimtizama Goryanah Kisha walinong’onezana.

“” Huyu ndie binti yake! Mamake anatoka na mzee rajab Yule! Naskia ameungua! Daaah! Maskini binti wa watu atabaki yatima sahii tu! Sijui maisha ndio yalimfanya mamake amchukue Yule mzee apate kula!?”

Wakati wakizidi kuzungumza Goryanah hakuwasikia, muda wote alikuwa akihesabu pesa alizoziuza Kisha aliweka kwenye kimkoba alichokuwa akitunzia pesa!

Baada ya kumaliza mboga zote ilibidi arudi kwenye ule mti waliokubaliana watakutana! Alikaa huku akimsubili Mudy Kisha alitoa pesa huku akizihesabu, siku hiyo alikuwa amekusanya Kama elfu kumi na moja na Mia mbili, wakati akizidi kuhesabu Kuna kikaratasi kilianguka ilibidi akiokote Kisha alikikunjua akisome.

“” Huyu nae Kila siku haishi kuniletea vibarua! Eti anioe ili niepukane na kuungua jua! Ani ananionea huruma Mimi! Sa akifanya vile ndio ataniepusha umaskini vipi kuhusu mamangu!?”

 

Goryanah ilibidi acheke kwanza, huku akiichana ile karatasi! Kwa mbali ndio anamuona Mudy akija na beseni lake likiwa tupu huku akicheza cheza njiani.

“” Ooh! Afadhari hata Mudy nae kamaliza! Muone anavyocheza kwa furaha! Barabara kaifanya yake!”

Mudy baada ya kufika ilibidi akae kwanza chini Kisha alijilaza kwenye mchanga chali akibaki kutizama mti ule, alimuita Goryanah kwa kifupi.

“” Gorii! Unajua leo umeninenea vizuri! Hutaamini nimefika pale stand! Kuna wasukuwa watatu wamenunua ndizi zote!”

Goryanah baada ya kusikia vile ilibidi alale nae kifudifudi huku akikaa sitaili fulani ya kumsikiliza mtu kwa umakini.

“” Ni wasukuma watatu ndio wamenunua!?” Kwanini wawe wasukuma tu!?” Mudy alicheka huku akigeuka kumtizama Goryanah! Kisha aliongea..

“” Mamangu anaumwa ujue! Nimemuacha akikohoa muda wote! Sijui ni vumbi la shambani, majuzi kati tulienda kupalilia mihogo nahisi ni hili vumbi ndio limemuathili.”

Goryanah ilibidi akae huku akikumbuka kipindi yupo anauza mboga alisikia kwa mbali wale wamama wakimuita Msimbe(mwanamke aliyeachika au asiye na mme) mamake” Ilibidi ajikaze japo hapendi kusikia mamake akiitwa vile.

“” Tuondoke kwanza! Hata Mimi mamangu atakuwa akinisubili kwa hamu!”

Mudy aliinuka taratibu, walianza kutembea huku sitori zikiendelea njiani, lakini kwa Mudy alikuwa akitembea Kama akichechemea Gorii alimuona ilibidi amsimamishe Kisha alichuchumaa chini.

“” Ayaa! Nyanyua mguu wako nijue umekuwaje? Make watembea ukichechemea.”

Mudy baada ya kuinua mguu, alikuwa kajeruhiwa na chupa, Gorii ilibidi amkalishe chini Kisha alitizama upande wa pili aliona Kuna mgomba, alitabasamu Kwanza huku akikimbia kuchukua jani la mgomba akija nalo taratibu akilipikicha.

 

“” Hii inakata sumu! Baada ya siku tatu mguu wako utakuwa vizuri! Tutaendelea kufanya biashara tenaa!”

Mudy alibaki akimtizama Goryanah! Alimchukulia Kama Dadake na yeye alimchukulia Kama Kaka japo umri wao ulikuwa sawa! Mudy nae alikuwa akiishi na mamake pamoja na wadogo zake wawili wao walikuwa Darasa la tatu! Mamake ni mtu mwenye khari ya chini, anae genge anauza mboga mboga Nyumbani kwake, na muda mwingi alimtegemea Mudy. kwa ujumla maisha yake na Goryanah ni Kama yalifanana kutokana na kipato chao.

Baada ya Goryanah kumaliza kumhudumia alimwambia akanyagie mguu wake chini, ili dawa ifanye kazi vizuri. Goryanah Alibaki akimtizama Mudy jinsi dawa inavyozidi kumuingia, aliona uso ukianza kukunjamana ilibidi acheke kwanza.

“” Hivo hivo! Piga hatua ndio unazidi kupona! Kama vile unaumia ee!?”

“” Naumia “Gorii” siyo Kama natania hapa!”

“” Basi kaa tena!”

Ilibidi akae huku akizidi kuunyosha mguu wake misuri ikae vizuri, baadae alijisikia unafuu ilibidi amtizame kwanza Goryanah.

“” Goriii…!”‘

“” Vipi? Bado inauma!?”

“” Hapana..!”

“” Ilaa…!”

“” Wewe ni mzuri!”

Goryanah ilibidi asitishe kwanza zoezi lake make alikuwa akimchua taratibu kwenye mishipa ya miguu.

“”Aaah! Twende bhana! Unanitizama Sana! Au wataka nikuonee huruma! Mimi kwenye maisha ya mtu huwa naangalia afya yake tu.

Walianza kutembea taratibu huku Goryanah akipiga hatua ndefu, akifika mbele kidogo ilibidi asimame kumsubilia Mudy, make mwendo wake ulikuwa ni wa taratibu

“” Aaah! Mudy nawee! Unakuwa Kama sio mwanaume tu! Wewe huwezi ukatembea kwa uharaka tukawahi!?” Harafu tupo maeneo siyo!”

Mudy baada ya kumfikia ilibidi asimame nyuma yake make alikuwa amenuna. Goryanah ndio anageuka huku akipaza sauti, ndipo anakutana na Mudy uso kwa uso ilibidi hasira zishuke Kisha alicheka tu.

“” Hapo sawa’ make nilikuwa naenda kukufokea vibaya! Harafu leta hizo pesa ulizokusanya make Kuna vijana hapa nimeona mtu mmoja akirusha jiwe upande wa pili naona Kama wanashituana hivi! Hawa wanahitaji pesa, fanya hivi wewe kaa utulie.”  Itaendelea…….

 

Usikose kufatilia simulizi yetu mpya! Na huu ndio mwanzo wa simulizi yetu, ushirikiano wenu ndio utatufikisha tamati wa simulizi yetu pendwa. Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

 

30 Comments

  1. Stori km hizi ndo zenyewe, ziko na maudhui na mandhari za asilimia kubwa ya Watanzania. Big up admin 💪

Leave A Reply


Exit mobile version