IlipoishiaMama alisogea pale Kisha alimkumbatia kwa furaha.

   “” Leo ni sherehe yenu! Tumewaandalia part kubwa ya kufurahia afya zenu! Ingia chumbani kwako ujiandae kila kitu utakachokikuta utakitumia! Halafu ndio utaenda kumuona huyo Kaka White! Na yeye katoka kwenye matibabu Pamoja na wengineo ambao hawapo hapa!”   

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA TISA 

Gori alifika chumbani alikuta Kuna nguo zimeandaliwa pale pamoja na viatu vyake alifanya kujiandaa, wakati huo Mama aliingia chumbani kumtengenezea nywele zake.

   “” Waooo! Hapo umekaa vizuri sio Kama unavyochanaga wewe!”

Baadae walitoka ndani kuelekea nje make wenzao walikuwa wakiwasubili, kila mtu aliyemuona Gorii alimsifiwa kwa kupendeza!.

Safari ilianza walikuwa wakielekea kwenye Hoteli moja haikuwa ngeni machoni kwa Gorii! Ni siku moja kabla halijatokea tukio la kumpoteza Mamake walienda kufanya tangazo wakiwa na Doreen!

Gori baada ya kufika pale alianza kujishuku! Wakati wamefika pale taa zilizimwa Gorii akaambiwa aingie Kisha aelekee mbele! Ile anafika mbele anaanza kushangaa shangaa zile taa alibaki kukenua ovyo! Si unajua Kuna vitu vingine vinastaajabu machoni lazima vikuduwaishe kwanza!

Ile bado anashangaa kunae mziki wa taratibu uliachiwa! Aliona Kuna mtu anamnyooshea mkono acheze nae! Hutaamini alikuwa ni Kaka White! Siku hiyo alipendeza kuliko! 

Gori alikuwa bado anamushangaa kwanza! Kama miguu imekaa vizuri lakini hata Kaka White nae alikuwa akistaajabu vile vilevile! Akaona wee! Atashangaa mpaka sangapi mziki ni wao! Na macho ya watu yote yanawatazama! Isitoshe sehemu waliyokuwa wakichezea ndie inayo mwanga pekee hivo walionekana vizuri! 

Jolvin alimsogelea kwa ukaribu Kisha mkono mmoja alimshika kiunoni huku mkono mmoja wa Gorii aliuweka begani na kuanza kucheza nae taratibu pasina pupa yeyote wakizidi kutizamana.

Gori alikuwaa bado haelewi somo! Muda wote alikuwa akimtazama Kaka White akisitaajabu kwa muonekano wake mpya.

Jolvin alifanya kumkonyeza kwa ishara awe huru kucheza, alifunga macho kwa hisia huku akitafuta matamshi ya wimbo wenyewe unavyosikika ndani ya moyo Wake. Gori nae alikuwa bado akimshangaa Kaka White jinsi anavyovuta hisia na yeye akaamua kuzama mazima kwa ile song. 

Mashairi mazuri yalisikika kutoka kwa mwimbaji maarufu aliyejibebea tuzo za uiambaji wa nyimbo zilizojaa hisia, sio mwingine alikuwa ni Westlife, wimbo wake uliachiwa masikioni kwa watu ulikuwa ukisikika taratibu huku ukivuta hisia zilizo ndani ya nyonyo za watu, anakwambia ” My love” Kisha ala za music zinafatisha zikiwa zimetulia kabisa! Baadae mashairi ya Mwandishi yanaanza, anakwambia…. 

   “” An empty street

     An embty house

     An hole inside my heart.

    I’m all alone the rooms are getting smaller.

   I try to read,

   I go to work

   I’m laughing my friend.

  But I can stop to keep myself         from thinking o. no! 

Nimejaribu kujisomea, nimeenda kazini ili nifurahi na rafiki zangu lakini nimeshindwa kujizuia kwa kila kitu. 

   I wonder how,

   I wonder why, 

   I wonder where there are! 

Hakuishia hapo alimalizia mashairi tena anakwambia

“the days we had the songs we sang together”

   To hold you in my arms

   To promise you my Love

   To Tell you from the heart

   Your all thinking of..

Mwisho kabisa maneno ya mwishoni mwishoni alimalizia kuyaongea.

   “” natamani nikushike kwa mikono yangu, nikuahidi mpedwa wangu ni kiasi gani navyojisikia ndani ya moyo wangu! Wewe ni kila kitu kwangu”

Hatimae wimbo ulienda kumalizika Jolvin alishika kidole Cha Gorii kisha akamvalisha Pete ya uchumba huku akibaki kumtizama akishuhudia uzuri wa Gorii ulivyomchanganya, Upepo nao ulikaa karibu yao uliamua kutumia ile fursa ya kupeperusha nywele ya Gorii kuhakikisha Jolvin anachanganyikiwa zaidi.

 Walibaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa, baadae Jolvin alimalizia kumkiss kwenye paji la uso huku  Gorii alikuwa bado anashangaa na asiamini kitu anachokiona.

Alijitoa mikononi kwa Jolvin, lakini Jolvin alifanya kumvuta taratibu Kisha akamkumbatia tena, Ile Gorii anataka kuongea alimuwahi akamwambia huku akimziba mdomo kwa kidole chake.

       “” Because I love you” 

Kisha alimshika mkono wakielekea kunako viti vyao maalumu viliandaliwa pale! Wakati wakiwa wanashuka taratibu Gorii alikuwa akikakamaza mkono hataki kushikwa, Jolvin aliishia kucheka lakini alianza kuchukua tahadhari mapema make hachelewagi kusanua jambo.

Wakati wamekaa Pale Gorii alikuwa akitafuta nafasi ya kuzungumza na Jolvin lakini Jolvin akawa anamkwepa, Gorii baada ya kuona anamkwepa ilibidi aanze kuunda stori.

   “” Kaka White… Yaani Unajua kucheza ulivyokuwa umenikamatia mkono kiunoni! Nikahisi Kama nipo ulaya! Ila wao wanakuwaga romantic sio Kama wewe!?”

Jolvin alimtizama chinichini Kisha alimsogelea karibu kabisa ili amusikie vizuri.

   “” Sio hivyo bhana…! Bibi anatuona” Halafu nilitaka urudie vile ulivyoniambia kwa kingeleza wakati tunatoka pale!”

   “” Ooh! Kumbe ulitaka usikie vizuri.. “” Gorii Nakupenda Sana! Natamani nikufanye uwe mkewangu wa Ndoa! Muda mrefu nimeanza kuvutiwa nawe japo mara ya kwanza vituko vyako vilikuwa vinanifanya nishidwe kukuelewa vizuri! Umuhimu wako niliona tangu siku ile ulivyotoka nyumbani nilianza kujisikia vibaya kwanza nilianza kukumisi bila sababu! Ndipo nikajua nimejitenga mbali na mtu muhimu kwangu!

Jolvin alianza kusema ya moyoni lakini alikuja kukatiswa na Rich aliomba acheze na Gorii! Gorii akaona ndio nafasi ya kumuepuka make alimtoa jasho.

Wakati anataka kuondoka Jolvin alimshika mkono Rich! Kisha alimuonesha aangalie pembeni, alikuwa ni Sophia akimtizama.

   “” Aaah Unabahati yako! Make nilitaka kumuonesha Broo kuwa Mimi ni zaidi yake kwenye kucheza.”

Rich alifanya kumuachia Gorii, akamshika mkono Sophia wacheze wote.

Gorii alikasirika kwanza huku akimtizama Sophia aliekuja kumharibia tgeti zake, Alijua kabisa Kama atakaa pale maada inaendelea tenaa! Alikaa kwa unyonge huku akisogea pembeni ajitenge na Jolvin! Make tayari ashaanza kumuogopa!

Muda kidogo familia ya Mama Doreen iliingia ikiwa imeaandaa zawadi ya kuwapongeza na kuwapa pole kwa nyakati walizozipitia! Hawajakaa sawa mama Muddy aliingia akiwa na Muddy na wao walikuja kuwaona.

Siku hiyo ilikaa vizuri Sana baina ya watu wawili! Na siku hiyo ndio walitumia nafasi ya kutambulisha Duka lao kwa mara nyingine! Kwani Gorii ndie atakuwa akilisimamia tena.

Muda ulizidi kwenda Sherehe ilimalizika walirudi nyumbani kupumnzika!

Chumbani kwa Gorii ilikuwa ni kelele muda wote hasa akikumbuka jinsi Jolvin alivyokuwa akicheza nae mbele ya watu, maneno ya Jolvin yalijirudia masikioni kwake. “” Because I love you” ndio lilizidi kumchanganya kabisa! Aliangalia ile Pete ikamfanya atabasamu kwanza.

Alianza kuzunguka mle ndani ndipo akamkumbuka Anelisa, alishusha pumnzi kwanza Kisha alicheka.

   “” Because I love you!? Vipi huyu Mama wa kulalamika Jovii… Miss u… Jovii.. nikuletee Nini? Jovii.. Jovii….  ” Ngoja nimfuate nikamwambie!”

Huku kwa Jolvin alikuwa amekaa na Wenzake huku wakipiga stori, Esau alimpongeza kwanza.

“” Hongera kwa kuwa jasiri siku ya leo umeongea yamoyoni kwako! Niligundua zamani unampenda Gorii! Hata kumtizama kwako ulimtizama tofauti kuliko hata unavyomtizama Anelisa.”

Jolvin Alibaki kucheka cheka, ilionesha kabisa anae furaha kwa kitu kilichotokea.

Rich ilibidi alale miguuni kwake huku akimtizama.

   “” Ila Gorii ilitakiwa Mimi niwe nae! Unajua ana akili Kama zangu! Isitoshe wewe bado hakupendi! Unajua wapenzi huitana majina mazuri ila Wewe Kaka White! Bora niwe Mimi!”

   “” Na Sophia…!!?”

   “” Wote bhana! Mimi nitaishi nao si wote wananipenda!”

Huku kwa Gorii alikuja kasi akiwa na furaha akiamini amepata majibu ya kumjibu Jolvin! Alifika akagonga mlango kutokana na ile spidi aliyokuwa nayo mlango uliegesha, akawa ameingia nao mpaka ndani.

Ile anatua macho anawakuta wapo wote alibaki ameduwaa, huku Esau, Joely na Rich walianza kumtania   wakimuita ” Shemeji, Shemeji” Gorii akakosa ujasiri alitoka  mbio huku akiwaacha watu hawana mbavu.. 

   “” Hapa hamna mwanamke!!!”

Joely aliongea huku akizidi kucheka.

   “” Nyie nyote ondokeni Mimi nilale.

Ilibidi wamuache make Kama ni chaguo kachagua yeye mwenyewe. Wakati akiwa amelala alikuwa anawaza ni namna gani atafanya kumbadilisha Gorii! Muda mwingine huwa anaboa.

“” Hapana hapana! Mbona nataka kuwa kichaa! Nimeenda kumwambia Kaka white kuhusu Anelisa, nawakuta hawa nao wamo halafu wananiita mi Shemeji yao! Usikute wao wanachukulia serious wakati Mimi natania!”

Ni mojawapo ya Pilika alizokuwa nazo Gorii chumbani katika kuwazua mpaka kunapambanzuka . 

Asubuhi yake Familia kwa ujumla waliamka kusaidiana kazi mpaka mida ya mchana kila kazi ilikaa sehemu yake! Mama Muddy pamoja na familia aliyokuwa kaambatana nayo waliaga kutoka na familia ikabakia Kama hapo awali.

Gorii alikuwa Chumbani kwake akipanga panga baadhi ya vitu vyake make tangu apate ajari hakupata muda! Ile katika kukagua ndio anakutana na picha ya Mamake! Ilimfanya akumbuke maisha ya nyuma aliyokuwa akiishi na Mamake kwa furaha leo hii hayupo tena, aliamua kuzihifadhi vizuri kama kumbukumbu!

Baadae alitoka nje ili kutizama mazingira kwanza ya familia ya Mishoki! Siku hiyo alianza kukumbuka maneno ya Mamake kipindi kile wamepata ajari wakiwa wote Kuna maneno aliyoongea, ilibidi amtafute kwanza Jolvin aongee nae.

Alifika Chumbani kwa Jolvin lakini alikuta kumerudishiwa Aligonga mlango kupo kimya mwisho aliingia akichungulia lakini hakunae mtu.

Alitoka kumuulizia Kwa Bibi, majibu aliyoyapata ni Jolvin karudi chuoni kufanya mitihani kaondoka asubuhi, na kuhusu simu kaziacha mpaka atakaporudi.

   “” Sasa Bibi… Mjukuu wako yupoje lakini, akipata shida huko itakuwaje!?”

Gorii alitoka akilalamika akiingia Chumbani kwake lakini alirudi tena kwa Bibi.

   “” Sasa ndio kaacha chumba wazi!?”

Bibi alimrushia funguo.

   “” Kasema ubaki nayo! Atakuwa akikutafuta kwa namba za wanafunzi wenzake!”

Ilipita wiki moja tangu Jolvin aende chuoni pasina kupiga simu yoyote Nyumbani! Esau, Joely, Rich na wao warudi kwenye Pilika zao! Nyumba ikawa ni kimya! Kwa  Gorii ilimpatia Mawazo Sana, alianza kukumbuka ukaribu wa Jolvin, furaha aliyomuoneshea kwa muda mfupi ilitengeneza kumbukumbu kubwa, muda mwingine aliwaka hasira  akikumbuka Yale maneno aliyoyasema anampenda hakuyaamini Tena alichukulia ni vile alimdanganya! Ilifikia hatua zile fikra zote za kumkumbuka Jolvin alizihamishia  kwa Mamake siku akionana na Jolvin alitaka ajue ni kipi alimwambia siku ile anapata ajari.

Majira ya jioni akiwa Chumbani kwake, alikuwa akipitia picha walizopiga hivi karibuni akiwa na Jolvin alibaki kuzitizama! Siku hiyo Mamake Rich! Alifika kumtizama Gorii baada ya kumuona muda mrefu kajifungua.

Mama Alifika akamshika begani huku akitizama picha zilizokuwa pembeni Gorii alizificha na nguo yake, alitambua kabisa Gorii kaanza kumkumbuka Jolvin! 

   “” Utakaa ndani mpaka lini!? Leo hujaenda chuo umejifungia humu! Bibi yako anakuhitaji Chumbani kwake na wewe upo huku!”

    “” Hapana Mama! Nilikuwa nasoma tu! Unajua mitihani ipo karibu kwahiyo muda mwingi nautumia kusoma!”

Mama ilibidi amuache Gorii make alikuwa akielekea kazini! 

Baada ya Mama kuondoka Gorii aliingia kwenye chumba Cha Jolvin kwa mara nyingine, alianza kukagua kila kitu kilichokuwa pale, Kuna nguo baadhi alizoea kuzivaa…. Gorii alibaki amezikumbatia! 

“” Kaka White..  Nimekumisi kweli!! Leo nimekumbuka maneno yako uliyoniambia siku ile ya party! Nakumbuka siku yenyewe ulivyokuwa ukicheza na Mimi! Nakumbuka siku ile tulivoenda kule kijijini tukaenda kutembea shambani! lakini  ni lini utarudi?

Ni siku tatu zilisogea Gorii alikuwa ameanza mitihani ya kumaliza chuo ilichukua Kama siku tano akawa amemaliza mitihani yake! Akawa yupo Nyumbani akisubili matokeo.

Huku kwa Jolvin siku hiyo alikuwa akifungasha mizigo yake kurudi Nyumbani baada ya kumaliza mitihani yake alitizama muda kwanza, aliona bado unatosha alipita Mjini ili aangalie mazaga yoyote Yale ya kupeleka Nyumbani.

Majira ya jioni Jolvin ndio anaingia Nyumbani alikuta nyumba nzima imetulia kila mtu alikuwa amejizoelea ni kumaliza kula na kulala!

Alikaa sebuleni kwa muda wa dakika kadhaa Kisha alienda kumgongea Bibi yake! 

   “” Gorii haulali na leo tenaa!? Nishakwambia Jolvin atarudi tu!”

Bibi ile anafungua anashangaa kumuona Jolvin yupo pale, alifanya kumkumbatia huku wakikaa.

   “” Mjukuu wangu hata simu hupigi Jamanii! Huku mwenzako umemuacha ana khari mbaya! Yaani muda wote anashinda hana furaha akikufikilia!”

   ‘” Usijali Bibi nitaongea nae tu! Funguo yangu iko wapi lakini!?”

   “” Gorii kairudisha Jana kwa hasira kweli analamika kachoka kutunza chumba Cha mtu aliekimbia chumba chake!”

   “” Kana matatizo haka! Hebu nisaidie funguo kwanza angalau nitue mizigo ndio nimtafute Goryanah! Wewe Bibi tutaongea kesho pumnzika kwanza.

Jolvin alielekea chumbani Kwake alikikuta chumba chake kimependeza kweli!

   “” Waoo Gori mi nakujuaga Wewe ni msafi sana, sema ni akili yako inavokuwa na wenge ndio maana huwa wajisahaulisha!”

Aliingia bafuni kuoga baada ya kumaliza alichukua simu yake akawasha siku hiyo akague baadhi ya jumbe zilizoingia alikutana na ujumbe wa Anelisa akilalamika baadae alimtumia ujumbe wa kumtakia mtihani mwema, kwa Gorii alikuta jumbe zinazomuuliza kurudi kwake aliamua kumtumia ujumbe. “” Leo nimerudi”

Hutaamini Gorii kumbe alikuwa hajalala! Alikuwa akichezea simu yake huku akisubili kutafutwa na namba ngeni, baada ya kuona message imetoka kwa Jolvin ilibidi amjibu” Sitaki matani Bibi’

Akili ilimtuma atakuwa ni Bibi kachukua simu ya Jolvin akimchezea akili, lakini ujumbe uliingia tena “” By Jolvin ( Kaka white) njoo chumbani kwangu.

Aliinuka taratibu huku akiwa kashikilia simu yake! Akijua ni Bibi ndie atakuwa chumbani kwa Jolvin make hata funguo alimrudishia. Aligonga mlango lakini alianza kuhisi Yale marashi ya Jolvin nakubaki kusema huenda ni kweli Jolvin karudi.

Jolvin alikuja kufungua mlango, huku Shauku yake ilikuwa ni kumuona Gorii! Walikutana uso kwa uso huku kila mtu akibaki kumtizama mwenzake akionesha kumkumbuka.

Gorii alimtizama mpaka machozi yakimtoka alionesha ni kweli kamumisi mtaaramu! Jolvin pia alijisikia huruma Sana hata yeye alimumisi sivyo kawaida alimkumbatia kwa sekunde kadhaa! Akawa amemsogeza Hadi kwenye sofa alibaki akimtizama huku macho yake hayaishi hamu.

Alimtizama vidole vyake vya mkononi Kama anae Pete! Kisha alinyanyua mkono wake akashika ile Pete na kumtizama Gorii usoni, alihisi furaha ya ajabu! Alimsogelea karibu Gorii ambae alikuwa ameduwaa kila akizidi kumtizama Jolvin alimuona wa tofauti Sana machoni kwake tofauti na siku nyingine.

Jolvin aliona ile midomo aliyokuwa akiitolea tofauti na ya Anelisa kipindi kile leo ndio ataenda kugundua utofauti ulioshidwa kuamini kuwa ile yote ni midomo! Aliamua kujirizisha mazima isiwe kuona tu pasina kugusa akawa amepata deep kiss! Lililojibu majibu ya maswali yake!”

Hatimae kunapambanzuka! Jolvin aliwahi kuamka asubuhi kabla ya Gorii hajaamka alibaki akimtizama zaidi na zaidi huku akitabasamu tu! Aliamua kumfunika shuka huku akiamka kuelekea bafuni! Baada ya kumaliza kujiandaa aliwahi kukifunga chumba Cha Gorii ili wasimsitukie na Kama watamuuliza itabidi awadanganye kaitwa chuoni Kuna form ya kujaza.

Alirudi chumbani kwake ndio anamkuta Gorii kaamka akijaribu kushuka kitandani, Alibaki akimtizama kumuonea huruma Sana! Aliamua atoe msaada alifika akambeba kumpeleka bafuni Kisha alimutaka radhi.

“” Nisamehe kwa yote yaliyotokea! Lakini hakutaharibika kitu! Najua unagopa Bibi atakutafuta! Ila nimewaambia umeenda chuoni utarudi jioni! Na leo utashinda chumbani kwangu halafu jioni nitakutoa naimani utakuwa sawa!” 

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya 20

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

 

 

18 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version