Ilipoishia “Alisimama huku akielekea chumbani Kwake! Muda huo alikuwa amefura hasira! Lakini Esau ni mtu mkubwa alielewa kipi kinamsumbua mdogo Wake, aliwaza namna ya kumsaidia japo itakuwa ngumu Gorii, akamuelewa kwa akili yake ya kitoto kitoto kazi ipo.”

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA TATU

Wakati kaondoka tu, Anelisa alitia timu nyumbani alikuja kumuona Jolvin.

   “” Aa Shemeji! Mbona leo usiku sana! Itakuwa umemumisi rafiki yako!?”

   “” Nimempigia simu.. nimeona mazungumzo yake Kama hayupo vizuri! Nikaona nije kumuona! Vipi Bibi yupo sebuleni!?”

  “” Atakuwa kalala..! Wewe Nenda tu ukamuone!”

Esau ilibidi amuache huku akiendelea kupangilia mambo yake make karibia anarudi kazini, huku Joely na Jolvin wao walikuwa bado wanasoma! Essau yeye alikuwa akifanya kazi kwenye shilika la chakula.

Anelisa aliingia Chumbani moja kwa moja alimkuta Jolvin kalala kwenye sofa huku akiwa na Mawazo Sana.

  “” Nilijua tu lazima utakuja ! Make huwezagi kuvumilia ukimuona rafiki yako hayupo vizuri! Vipi umeniletea mihogo!?”

   “” Nimehangaika kweli kuipata! Yaani mpaka nimeenda mtaani kuitafuta!”

“” Nashukuru kwa kuwa unajali Sana! Vipi Mama, Baba wazima!?”

“” Of course Wazima! si hutaki kuwaona!”

“” Nitakuja, Chuo waenda lini!?”

“” Ilitakiwa nikareport leo lakini nilihofia utajisikia vibaya sijakuaga, nikaona nikusubili urudi.”

“” Muda mwingine usifanye hivyoo! Waweza ukapoteza kila kitu! Mimi nipo tu.””

Jolvin alimaliza kula Kisha alijilaza miguuni kwa Anelisa, ni kitu alikizoea make ni rafiki tu.

“” Anelisa wewe si rafiki yangu tu? Kuna kitu nataka nikwambie huenda wewe ni mzoefu wa vitu hivyo sijui utanishangaa! Make hata Mimi najishangaa!”

“” Aaah.. Jolvin kitu gani hicho tenaa!? ” Ila kabla hujasema Mimi nataka niseme kitu kwako nahisi sitapata muda wa kusema ukileta ajenda yako!?”

“” Basi semaa…!”

“” Nataka urafiki wetu upige hatua… Make imekuwa muda kweli urafiki wetu umebakia sehemu moja!”

“” Hatua ipi tenaa Anelisa? Mimi napenda hivi hivi tunavyoishi! kwani kunashida?”

“” Hamna shida, ila Mimi naona ndani ya urafiki wetu Mimi na wewe, moyoni kwangu kumezaliwa kitu kingine!! Nahisi kukupenda Sana Jolvin, mpaka Kuna vitu natamani nivifanye zaidi ya urafiki.”

Jolvin alishituka Kwanza, alikaa vizuri huku akikumbuka maneno ya Gorii kuwa Anelisa anamchukulia zaidi ya rafiki, halafu leo ndio anasikia live bila chenga, hata hivyo na yeye alilifahamu hilo Mwanzoni alitaka kumuwahi amwambie kunae mtu pia anampenda. 

Alimjibu;-

   “” Lakini Anelisa… Ni ghafra sana! Mimi napenda hiyo nafasi ya urafiki niliyokupatia hiyo nafasi nyingine hapana!!”

   “” Jov..!! im sure!! nakupenda wewe! Ingekuwa kunae nafasi ya mtu mwingine moyoni kwangu nisingesema kwako!?”

Jolvin alishusha Pumnzi Kwanza huku akipepesa macho akiangalia pembeni, unaambiwa siku zote hakuna kitu kinachozoeleka machoni Kama kubadilisha hatima, Jolvin baada ya kuambiwa hivyo na Anelisa alianza kumuogopa Kwanza hata yale mazoea yakaanza kukata taratibu.

   “” Lakini Anelisa.. Mimi sipo vizuri kwasasa, bado Nina uchovu wa Safari tutaongea siku nyingine! Nahitaji kupumnzika.. sijui umekuja na usafiri wako? Au nimpigie dreva aje kukuchukua!?”

   “” Hauwezi ukanisindikiza? Halafu ulitaka kuniambia Nini labda, kabla sijaondoka?”

   “” Aaa! Nilitaka nikushukuru kwa kuniletea chakula nikipendacho!”

“” Okay byee! Tayari nimeshaongea na dreva tax ananiijia! Nahisi atakuwa getini sahii! Kama nitaondoka kesho nitakujulisha.

“” Okay! usiku mwema! pia Ufike salama!?”

Wakati Anelisa anaondoka, alipishana na Esau bila kujua! Esau alimwangalia Kisha alirudi Chumbani kwake.

“” Huyu Jolvin sijui anashida gani? Nashidwa kuelewa yupo upande gani ni Anelisa au Gorii? Anyway atajua kuchagua yeye kipi moyo unataka!?”

Huku Chumbani kwa Jolvin akili yake ilizidi kuvurugika, Anelisa alizidi kumsumbua kichwa, bado Gorii nae kaanza kuchukua nafasi! Aliangalia picha ya Anelisa, ni rafiki yake wametoka mbali wamezoeana, kila mtu anayajua mapungufu ya mwenzake Kama ni kuoana hawatasumbuana, aliangalia picha ya Gorii anaonekana bado anae akili ya kitoto kitoto, mambo yake ndio usiseme! Hajui kuvaa vizuri yeye ni minguo ya kijijini ndio anapenda yaani hajui kuumode mwili wake ukakaa vizuri! Lakini ndio anavutiwa nae!  Aliona isiwe shida wote aachane nao awaze masomo yake! Make karibuni atakuwa na mitihani.

Asubuhi yake hata kulipopambazuka Gorii Kama kawaida huwa anaamka kufanya kazi za ndani, siku hiyo nyumba ilikuwa kimya Joely, Esau walikuwa wamemsindikiza Rich kuriport chuo.

   “” Humu ndani wote wameenda kumsindikiza Rich chuo, wanaupendo kweli! Mama nae kazini! Bibi sijui nae kaenda wapi!?”

Aliandaa chai, akisaidiana na wadada wa kazi waliweka mezani huku wakiendelea na pilika mbalimbali za usafi.

Muda kidogo ndio wanarudi wote, baada ya kumfikisha Rich Airport.

Gorii aliamua akatulie Chumbani kwake make kuleta shobo na matajiri ni Kama kujipendekeza.

Bibi baada ya kufika alimuulizia Gorii” huku akielekea Chumbani kwake.

“” Wewe Mjukuu! Njoo tunywe chai! Mbona meza ipo pekee!?”

Gorii” ndio anatoka Chumbani nusura apamiane na Bibi.

   “‘ Sorry Bibi! Niliwasubili mfike ndio tunywe chai!!?”

Bibi alicheka tu.

“” Miguu yako hainayo break!?”

“” Aaah!! itakuwa ni njaa hii! “

Walifika pale mezani wakaendelea kunywa chai. Baada ya kumaliza kunywa Esau alimuita Gorii waongee nje.

   “” Gorii Unajua kesho na sisi tunaondoka! Mimi narudi kazini Joely anarudi chuo! humu ndani mnabaki watoto wawili, wewe na Jolvin! Naomba mkae vizuri pamoja na Mama na Bibi! Muwapatie upendo hata kwa niaba yetu!” 

  “” Sasa.. Kaka mkubwa! Mimi nitakuwa shule na Kaka White! Bibi si atakuwa anabaki pekee mpaka turudi jioni ndio tunakuwa wote!?”

   “” Huo muda mkirudi basi mkae nae kwa pamoja! Ila Kuna kitu nataka nikuombe!”

“” Uniombe tenaa!!?”

“” Kaa na Jolvin karibu! Make akikosa mtu wa kukaa nae karibu huwa ana vitabia vya kuzira zira ovyoo! Muda mwingine huwa anakataa kula! Wewe uwe unamsimamia endapo itajitokeza vile!?”

Gorii ilibidi acheke Kwanza huku akimtizama Esau.

“” Si mtu mzima Yule!!? ” Mbona anavitabia vya kitoto japo Yeye huwa ananiambia nina mambo ya kitoto kitoto!?”

“” Ndo hivyo Sasa! Wewe kaa nae vizuri!”

Muda huo Joely Alifika, Alisogea Hadi kwa Gorii akiwa na Simu kubwa alichukua picha Kama selfie, huku wakiungana kwa pamoja katika picha ya pamoja.

   “” Leo Gorii umependeza kweli! Yaani umepigilia vitu vya mambele track na hilo prouva limekukaa Kweli!”

   “” Wewe J wa pili! Piga picha bhana achana na hizo nguo! Unaniharibia pouze!”

Ilibidi wote wacheke, baada ya kumtizama staili aliyoweka kwaajili ya Picha.

” Halafu mbona uliikataa Simu, Sasa utakuwa unatupataje ukitaka kuongea na sisi!?”

   “” Ipo ndani mbona.. nilimrudishia Kaka White akaikataa! Ila majuzi nilivoenda nyumbani! Nilimkuta rafiki yangu kanunua Simu nikawa nimechukua namba nikaisevu kwa Kaka White! Itabidi na nyie mniachie namba zenu nizisevu kwenye simu yangu make nilikosa mtu wakumpigia! kwa kuwa nyie mpo nitakuwa nawapigia?”

   “” Kwahiyo na sasahivi! Unaenda kuzisevu kwa Jolvin tukikupatia!?” 

  “” Hapana bhanaa! Ngoja nifate simu mniandikie, zitakuwa kwenye Simu yangu!”

Muda kidogo alirudi na Simu Kisha Alimpatia Esau.

  “” Ni Simu nzuri! Ila ukishajua kuitumia hii itabidi ubadilishe simu! Ununue kubwa!?”

   “” Wewe Kaka mkubwa… Na hiyo pesa nitatoa wapi Mimi!?”

   “” Zinatafutwa!

  “” Aah! Sahii Joely nae ataninunulia si unaherufi ya mwanzo  Kama Kaka White! Si J na yeye!?”

   “” Halafu Gorii! Leo tunaenda kufungua duka la nguo! Atakuwa akilisimamia Bibi na wewe! Ile mchana ukitoka chuo utakuwa waenda kumsaidia Bibi! Mama kakufungulia wewe ili uwe unapata baadhi ya mahitaji mengine na Bibi atakuwa Kama mfanyakazi wako!!”

   “” Khaaaa! Hapana Bibi tena! Nyie mnataniana!”

   “” Ndio hivyo!!”

Bibi alimjibu muda huo alikuwa kaambatana na Jolvin, wakiwa wamejiandaa tayari kwenda kuzindua duka make kila kitu kilikuwa kimekamilika.

   “” Twaweza kuondoka sahiii!” Jolvin aliongea.

Ikawa wote wamepanda kwenye Gari! Seat ya nyuma alikaa Bibi, Joely na Esau! Kukaa mbele Bibi huwa anaogopa.

   “” Afadhari nimekaa karibu na Bibi! Make leo ndio! tunakuaga lazima tukufaidi!”

Joely aliongea huku akimuegamia Bibi.

Huku mbele ilikuwa ni kimya kimya, Gorii alikuwa akimchungulia Jolvin kwenye kioo, mwisho alianza kucheka kila akikumbuka kuwa huwa anatabia ya kuzira zira ovyo.

   “” Muda wote huwa ni kucheka bila sababu! Utakuwa una matatizo wewe!?”

Jolvin alivunja ukimya, Gorii ni Kama anakela hivi!

   “” Bora Mimi nacheka! Wewe umeushona mdomo na zipu, Hatimae umeufungua! Au ndio umezira tenaa!?”

   “” Kwa kipi!?”

   “” Huenda Anelisa hajakuaga ndio maana umenuna? Vipi ulipoenda kumsindikiza Rich, ulipita pia kwa Anelisa, na yeye anaondoka leo.”

   “” Please Gorii! Naomba ukae kimya Kama huwezi…! Kakae Nyuma!”

Gorii” ilibidi akae kimya huku jicho likiwa nje.

Muda kidogo walifika Dukani! Walipaki gari pembeni. Duka lilifunguliwa Jolvin ndio alianza kutoa bei ya nguo! Huku Gorii akiwa anaandika, baada ya kumaliza kuelezea kila nguo na bei yake ilibidi akague kitu alichooandika Gorii” 

Alichukua lile daftari mwishoe aliamua kucheka tu.

   “” Kwamba umechora mtu pamoja na hio nguo kaivaa, ukaona haitoshi Hadi rangi ukaandika Kama ni suruali, shati, gauni, tisheti, vibode pamoja na aina za rangi yake?”

Esau, Joely na Bibi pia walisogea kutizama kila mtu alibaki kucheka tu!

Gorii yeye alibaki kuwashangaa! 

 “” Mbona kitu Cha kawaida tu nimefanya!”

Mwisho kabisa aliona Kama ni fedheha aliwanyanganya Daftari lake Kisha alienda kukaa nje aliwaachia wafanye wao Kama wao.

Wakati amekaa pale alianza kutizama maduka yaliyo karibu! Jinsi wanavyouza nguo! Juu ya Maduka yao kulikuwa na mabango yamewekwa na baadhi ya huduma zinazotolewa pale, aliangalia juu ya duka lao! Ndio anaona bango kubwa akiwa yeye, Jolvi pamoja na Bibi wakiwa wamevalishwa nguo nzuri kulingana na umri. Hakuamini macho yake make alikuwa kapendeza kuliko anavyovaaga, alimtizama Bibi nae kapendeza kweli Kisha alimalizia kwa Jolvin.

   “” Kaka White huwa hapendi kucheka! Ila hapa kacheka vizuri, akifika Nyumbani kimya, halafu anazira, daah!”

Alipiga makofi Kama tabia yake ya kujipongeza, akifanya kitu kikafanikiwa! Alimuita Bibi huku akikimbia ndani kulikuwa Kuna mziki umeachiwa taratibu! Aliongeza sauti akaanza kucheza kwa furaha, Kuna furaha ilimuijia hata hakuelewa imetoka wapi!?

Wote walibaki kumshangaa jinsi anavyofurahia! Baadae alimshika Bibi acheze nae make ilikuwa ni nyimbo ya asili zilikuwa zikichezwa zamani, Bibi nae akaona wee! Kuliko kuvunga acha ajiachie.

Watu waliokuwa wakipita pale walibaki kushangaa na kusababisha watu wazidi kusogea pale! Walianza kujaa huku kila mtu akisoma bango lilokuwa pale walijua ni duka jipya limefunguliwa bado ni la familia ya mtu maarufu Mishoki, walianza kujazana dukani kila mtu akiulizia nguo na kununua atakavyovutiwa nayo, Wakawa wamepata wateja wengi kupitia furaha ya Gorii.

Kunae mapapalazi wao huwa hawapitwi kitu walichukua baadhi ya matukio yaliyoendelea pale huku wakipost crip ya video Bibi na Gorii wakicheza, hii iliwavutia sana! Kwa mtu alioiona Crip ile alitoa comments anatamani afike kwenye duka hilo siku moja anunue nguo pale.

Huku kwa mama akiwa yupo kazini hana hili wala Lile, alipokea Crip ya Gorii pamoja na Bibi wakicheza alibaki kucheka Kwanza, ndipo akaamua kufatilia kipi kimejili! Alifunga Safari ya kuja dukani ajue kipi kimeendelea ndio anashangaa kukuta watu wamejaa huku waandishi mbalimbali wakimhoji Gorii! Ilibidi abakie ndani ya Gari kuogopa jamu ya waandishi wangempotezea muda Kama atawasikiliza.

Alimua kuondoka akiwa na furaha huku akiongea pekee.

   “” Furaha ya Gorii! Leo naitimiza kwa niaba ya Binti yangu! Nilimpenda Sana lakini Mungu alimpenda zaidi! Naimani Gorii kaja kwa niaba ya Mwanangu Naina! Daima alikuwa ni mcheshi! Aliipenda familia yake! Kutimiza wajibu ilikuwa ni jukumu lake, naiona nafisi yake ipo ndani ya Gorii”

Huku Gorii Baada ya kumaliza kuhojiwa, waandishi walihitaji picha ya pamoja wakiwa na Bibi, Jolvin pamoja nayeye! Taarifa zake zikawa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ule ucheshi wake hasa katika kazi yake!

Siku hiyo waliuza kalibia mzigo! Wote majira ya jioni walitoka pale wakiwa wapo hoi, lakini walikuwa na furaha kila wakikumbuka kilichotokea pale walibaki kucheka.

   “” Bibi kumbe na Wewe huwa ni mtaalamu wa kucheza, Mimi nilifikili ni wale wa Bibi wa kihindi wanavyochezaga nachi! Kumbe ni Bibi wa kitanzania!?”

Joely alimtania, lakini muda huo Jolvin na Essau walikuwa busy wakisoma comments kwenye peji zao za Instagram, baada ya kupost Crip ya Gorii akicheza. Jolvin aliipost huku kaipa kipaumbele kaandika

 “” Dadake na Kaka White! Akiwa kwenye harakati za kutimiza wajibu”

Comments zilizomiminika ni watu wengi walitaka namba ya Gorii! Wengine waliomba wafanye nae kazi kwa kuwatangazia biashara zao! Wengine walionesha kumtaka Gorii kimahusiano,Jolvin aliwaachia namba zake Kama watamhitaji Gorii kikazi.

Baada ya kufika Nyumbani Gorii alikuwa hoi! Mamake Alifika huku akiwa na furaha kuna zawadi alimletea huku akimshukuru sana, furaha aliyokuwa nayo ilimfanya mpaka atokwe na machozi, alimkumbatia Gorii Kisha alimshika usoni huku akiongea nae.

“” Wewe ni mrithi wa Binti yangu Naina!? Kila unachokifanya unanitia nguvu Mimi mamako niendelee kupambana kwaajili yako!”

Kila mtu alisikia vizuri maneno ya Mama, hutaamini baada ya kusikia jina Naina, kila mtu aliinamisha kichwa chini huku akijawa na simanzi Ghafra.

Gorii hakuelewa baada ya kuona watu hawana furaha, aliwaona hata watoto wakiume wakipikicha macho yao! Ishara kunae huzuni inayowatoa machozi na yeye alianza kulia, yeye kamkumbuka Mamake anatamani hata angekuwepo akamwelezea jinsi familia inavyopambana kwaajili yake! Angejisikia furaha Sana.

Itaendelea Sehemu Ya Kumi Na Nne …….

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

14 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version