IlipoishiaGorii hakuelewa baada ya kuona watu hawana furaha, aliwaona hata watoto wakiume wakipikicha macho yao! Ishara kunae huzuni inayowatoa machozi na yeye alianza kulia, yeye kamkumbuka Mamake anatamani hata angekuwepo akamwelezea jinsi familia inavyopambana kwaajili yake! Angejisikia furaha Sana.

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA NNE

Baadae alinyamaza Baada ya kuona watu wote wakimtizama yeye! Aliinua kichwa akiwatizama Kisha aliongea.

   “” Mama! Nashukuru Sana kwa kunifanya niwe binti yako! Mamangu alikuwa akinipenda Sana! Muda wote alitamani nitimize ndoto yangu, kutokana na mazingira aliniahidi siku moja nitaishi maisha ya kawaida Kama hatotimiza malengo yake ila maisha yawe ya kati! Kutokana na maisha ya kijijini! Mama alinipatia mtaji wa kuuza mboga mboga! Kwa yale maisha sizani Kama tungetoboa! Muda mwingine nawaza huenda zile pesa alizozichukua ni kwaajili yangu.

Gorii aliweka kituo Kisha aliendelea kulia, Mama ilibidi amshike mkono akimpeleka Chumbani Kwake.

   “” Basi pumnzika! Leo umefanya kazi kubwa Sana! Usiendelee kuumiza kichwa! Kila kitu kitakaa sehemu yake! Nashidwa hata nikushukuru vipi kwa kazi uliyoifanya! Mungu akubariki mwanangu.

Siku iliyofuata Esau, Joely waliondoka wote wakirudi chuoni na kazini, Nyumba ikawa imebakiwa watoto wawili Jolvin na Gorii! Siku hiyo hiyo Gorii aliingia chuo Cha maendeleo! Alipelekwa na mama kuripoti, Jolvin pia alielekea chuoni.

Huku kimbembe kwa Gorii kilianza, Baada ya kukabithiwa kwa mkuu wa chuo alielekezwa darasa lilipo. 

Kunae mwalimu wa darasa alikuwa akifundisha, Kama kawaida Mwalimu mara nyingi hukalili wanafunzi wake! Siku hiyo aliona sura ngeni ilibidi amsimamishe Gorii.

   “” Wewe binti! Naona ni mgeni hapo! Majina yako unaitwa Nani? Na unatokea wapi?”

   “” Gorii Goryanah! Natokea ndani ya huu mji.”

Wanafunzi wote waligeuka kumshangaa ni jina geni hawakuwahi kulisikia, ilibidi wacheke. Gorii hakupenda ilibidi awageukie kuongea nao.

   “” Ndio Wazazi wenu wamewafundisheni hivyoo! Kwani jina Gorii ni jina lakushangaza sana mpaka mcheke! Hamna adabu kabisa!”

Wote walikaa kimya wasiamini Kama Gorii ni binti jasiri anaweza kuwajibu vile! Mwalimu mwenye alibaki kufurahi baadae alimuuliza tena Gorii.

   “” Umesema waitwa Gorii Goryanah! Mbona usajili wako umesajiliwa Goryanah Mishoki.”

Gorii ndio anakumbuka kuwa kwasasa yeye ni familia ya Mishoki, ilibidi acheke kwanza Kisha aliomba msamaha kwa Mwalimu.

   “”I’m sorry! Niliwatania tu ili wafurahi si wamecheka! Wengine wakaanza kunisema chini chinichini! Anyway wanizoee tu!?”

  “” Unapenda kingeleza Sana!?

Mwalimu alimuuliza Gorii, lakini alibaki kutabasamu ukimuuliza zaidi hajui zaidi ya kuibia ibia tu.

Huku kwa nyuma Kuna wanafunzi walianza kusema chini chini.

  “” Huyu si ndio Mjukuu wa Mishoki! Halafu majuzi kati wamefungua duka la fashion new clothes! Kame trend kweli mtandaoni.

Kuna baadhi ya wadada walisogea karibu huku wakiangalia ile video aliyokuwa akicheza! Wakaiachia kwa sauti! Kuna mkaka mmoja alisimama huku akimnyoshea mkono Gorii”

   “” Wewe si ndie Gorii wa fashion clothes! Huku umeijia Nini Sasa wakati unakipato chako!?”

   “” Heeeee! Nyie kimya! Mwalimu hebu endelea kufundisha!”

Gorii alirudi kwenye seat yake akakaa vizuri kusikiliza! Baada ya kipindi kuisha Gorii alibaki anamanga manga! Aliona kila mtu yupo busy na mambo yake! Wengine walikuwa wakifanya discussion! Jinsi ya kujiunga nao ikawa ni mitihani.

Alishika simu yake ndogo ili ajifurahishe ndio anatazama wenzake wanazo simu kubwa! Alibaki kujishangaa mwenyewe!

   “” Daah! Mjini shule na shule inaanzia hapa! Yaani mabinti wadogo wadogo wapo busy na simu! Wengine wapo na mabwana hata hawahurumii Wazazi wao!”

Wakati amekaa pale Kuna vijana wawili walifika wakavuta kiti Kisha wakakaa mbele yake wakimtumbulia mimacho. Gorii nae Kama ni utundu utundu aliuzoea, ndio alikaa vizuri akawatolea jicho pasina kupepesa.

Kuna Kijana wa kwanza aligonga meza kwa nguvu, Gorii nae akafanya vile kisha alisimama akacheka huku akiwapatia mkono.

   “” Tukubaliane!! Mimi napenda nyie muwe marafiki zangu make napendaga watu wenye akili Kama zangu!”

Walitazamana kwanza Kisha walimcheka.

“” Unatujua kwanza? Unaonekana ni binti jasiri halafu unajiamini Sana! Ila tuulizie kwanza “Shidy gang” ni kina Nani!?”

“” Oooh! Mbona inafurahisha Sana! Mimi nimetaja jina langu leo watu wote wakacheka! Mimi naitwa “” Gorii Goryanah” jeshi la mtu mmoja hili nyie mpo wangapi mniunge huko!?”

Ilibidi waondoke kwanza walijua wameingia Cha kike, binti mwenyewe hamnemo ila bomba niaje!”

Muda wa Lunch ulifika Kama unavyomjua kwa Gorii hawezagi kuvumilia  njaa labda vingine ndio atavulimia.

   “” Kaka White alisema analeta chakula! Muda umeenda hata haji kuniulizia kwa mkuu wa chuo! Sa nitakula wapi leo?”

Ghafra simu yake iliita ilibidi apokee.

   “” Uko wapi!?”

  “” Nani wewe! Sijakupata!?”

  “” Kaka White!!”

  “” Ooh! Sauti ni yenyewe kabisa! Halafu una namba yangu kumbe!?”

  “” Acha maneno! Nipo nje ya geti hapa! njoo uchukue chakula!”

Gorii alitoka mbio, mpaka wanafunzi wenzake walibaki kumshangaa anavyowapita fulu.

Baada ya kumuona Kaka White! Ilibidi ashushe pumnzi kwanza huku akicheka.

   “” Nusura nivunje mguu! Yaani nimepamiana na hao watu nahisi nikishiba nitaenda kujieleza kwao! Watu wa hapa hawanaga dogo!”

Jolvin alibaki akimtizama kupitia kioo, alimfikilia kwanza Kama hajafanya tukio leo sijui tu!

Muda huo huo alitokea mdada akamshika mkono.

   “” Kanishonee begi langu! Hunaga break kwenye miguu yako? Sasa.. kashone begi langu!”

   “” Wewe tulia kwanza nile nishibe ndio tuongee! Muda ule nakupita si ulikuwa una nguvu halafu umeshiba, ungenipisha tu!?”

   “” Kajeuri kweli haka kamdada! Leo tu kametunyamazisha tukae kimya utazani ni kakubwa! Halafu ana majibu mabaya huyu.

Dada mmoja alikuwa akipita baada ya kumuona Gorii, ilibidi asogee make ni classmates mwenzake.

Jolvin ilibidi ashuke kwenye gari, Kisha alimshika mkono Gorii akiwageukia wale wadada.

   “” Wewe mwenye begi Kushonesha huo mkanda, ni shingapi!? Halafu na wewe endelea na Safari yako! Namjua vizuri Gorii huwa anaongea point huenda kweli mlikuwa mkipiga kelele darasani, lazima awanyamazishe huwa hapendi makelele isipokuwa utulivu tu!”

Alitoa elfu tano akampatia mwenye begi lake akashone Kisha waliingia kwenye gari na Gorii akaanza kula.

  “” Umefanya Nini huko darasani!?”

  “” Kaka White…!!  Nitakuelezea nishibe kwanza..!”

  “” Mhuu…!!”

  “” Nimeshiba sasa!! Ipo hivi nilijitambulisha darasani nikasema naitwa Gorii Goryanah Wakacheka na Mimi nikawanyamazisha wakae kimya kwani maajabu pale  ni kusema naitwa Gorii Goryanah!? Mimi nimekosea wapi?”

   “” Hujapigana? Make huwa unajiona unae nguvu nyingi zakuingia ulingoni.”

   “” Nimekua sahii! Wewe si bado unawapiga watu makofi!?”

   “” Hebu nitazame vizuri..!!?”

   “” Nini tenaa…!?”

   “” Hapo sawa! Nikahisi unae kidonda usoni! Halafu leo jioni tutaenda kupromote tangazo la biashara Mimi na wewe! Kuna mshiko mzuri ila Mimi nitafanya kukusaidia tu! Wao wanataka ma partiner wawili nafasi hiyo nitaichukua Mimi ili upate pesa!” 

   “” Na Bibi je!?”

  “” Unataka uende nae?”

  “”Je,  Dukani!!?”

  “” Ni baada ya kufunga! Make utaenda kufanyiwa Makeup ya live! Ile siku si walikuedit kwenye lile bango ukaona umetoka, leo ni live!”

  “” Unafikili nitaweza kweli! Ungekataa tu, make nitaogopa! Na namba walitoa wapi!?”

  “” Kwenye page yangu Instagram! Niliwaambia Kama watakuhitaji kikazi wanitafute Mimi!”

  “” Hapo sawa! Halafu Simu yako inaita! Mbona hupokei!?”

Jolvin ilibidi aifunike na kitabu! Kisha aliendelea kuongea na Gorii.

   “” Itakuwa ni Anelisa huyo! Pokea bhana huenda Kuna shida!?”

   “” Nambie Anelisa!!! Nilikuwa busy kidogo darasani! Kuna shida lakini mbona unaongea kwa shida hivyoo!?”

Gorii ilibidi avunge hasikilizi mazungumzo yao, alianza kupekua kitabu Cha Jolvin akikagua kila page.

   “” Umesema unaumwa kifua tena!? ” Vipi khari? Umetumia dawa lakini!?”

   “” Nimetumia lakini bado! Nampigia mama nae kasafiri yupo kikazi! Baba nae yupo busy na kazi! Nakuomba basi kesho nenda nyumbani mpatie simu mdada wa kazi nimpatie maelekezo akupatie dawa Kisha uniletee chuoni!”

   “” Sawa’ nitafanya hivyo hakikisha unaendelea kutumia dawa za maumivu! Kesho kwenye mida ya mchana nitakuwa hapo!?”

Baada ya kukata Simu, Gorii alibaki akicheka huku akijifanya busy anafunua kitabu! Jolvin aliamua kukifunika Kisha alimgeuza Gorii amtizame vizuri.

“” Si unanicheka Mimi! Anelisa huwa anaumwa kifua! Huwezi ukawa na huruma nae? 

 “” Muongo huyo! Eti anaumwa kifua! huyo analake jambo!!” “Kaka White… Naona umemisiwa na rafiki mpenzi!”

“” Nenda kwanza chuoni! Hunaga upeo wa kufikili katika matamshi yako “

Gorii aliondoka huku akiongea pekee.

   “” Huyu Anelisa anafanya kila namna ampate Kaka White..! Namimi sitokubali nitafanya kitu ili asiende! Ingekuwa ana moyo safi ningemuachia aende!”

Majira ya jioni walikuwa wameshafunga Duka, Jolvin alienda kuongea na Bibi akawa amewaruhusu waondoke wote!

Walifika Hadi sehemu wanapofanyia tangazo, Gorii alianza kubadilisha mwendo huku akijificha ficha! Wadau baada ya kumuona walimuwahi make alikuwa tayari ameshajulikana kutokana na like tukio.

Aliingizwa chumbani kubadilisha nguo huku akifanyiwa makeup ya kutosha mwisho kabisa aliletwa sehemu ya kuchukuliwa picha, alitazama upande wa pili ndio anatokea Jolvin akiwa ameupara balaa, kila mtu alibaki kumtizama mwenzake asiamini alivyopendeza.

Modo wao alisimama huku akiwaongoza jinsi ya kupiga pozi kwa kujiachia.

”” Jolvin sogea ukae nyuma ya Gorii! Mshike kiunoni fanya Kama unataka kumkisi! Ewaa happy imekaa vizuri! Pozi la pili fanya Kama unataka kumdaka”

Tukio la pili lilichukuliwa! Baadae yakafatia mapozi mbalimbali wakiwa kwenye nguo tofauti!

Baada ya hapo walisaini wakapatiwa pesa yao! Safari ikaanza kurudi nyumbani! Huku Njiani kila mtu alianza kufikilia yale mapozi yalimfanya amuonee aibu mwenzake! Mpaka walipokalibia nyumbani Jolvin alitoa ile bahasha akamkabizi Gorii.

   “” Pesa yako hiyo! Utaifanyia kitu unachokitaka!”

Gorii alichukua Bahasha akatizama pesa iliyopo, alichoamua alichukua nusu ya pesa akampatia Jolvin.

   “” Wote tulishiriki! Kila mtu achukue nusu!””

Jolvin aliichukua ile pesa akatoa kiasi Kisha akairudisha tena kwa Gorii.

“” Sitaki unirudishie tenaa! Mchezo huu uishie hapa!” 

Muda huo walifika nyumbani kila mtu aliingia chumbani Kwake! 

Huku kwa Gorii” alibaki akiihesabu ile pesa huku akifikilia namna ya kuifanyia.

 “” Pesa zote hizi! Hapa nitafanya kuzituma kijijini kwa Mama Muddy angalau wakarabati nyumba nipate pa kufikia! 

Alilala kitandani huku akivuta picha ya muda mfupi akiwa na Jolvin, Yale mapozi ya hapa na pale yalimchanganya.

“” Haya mapozi si huwa ya faragha mtu na mpenzi wake ndio hufanya vile!? Mbona Jolvin kafanya Kama mimi ndie Anelisa wake!”

Vilevile huku kwa Jolvin moyo ulikuwa kwatuu, kila akifikilia jinsi picha zilivyopigwa alitamani iwe Kweli. Kila akijaribu kulala aliona hakulaliki alichukua Simu yake akampigia Esau huwa anamwelewa Sana japo ni Mtoto wa ba mkubwa walizoeana kuliko hata Ndugu yake Joely ambae ni wa damu.

“” Mmetutenga bhana huku! Hata hamumuulizii Bibi, Mama Gorii! Mpaka tunawamisi.”

“” Mama nishaongea nae! Bibi kila siku! Kwa Gorii simpati kwenye simu labda nikuulize wewe mtu wa karibu nae, anaendeleaje?”

“” Mzima tu! Kashaanza vituko vyake huko shuleni Kesi haziishi, mara kakata mkanda wa begi, mara kawajibu watu vibaya! Yaani ni shida tu!”

“” Leo nakuona umeongea kuhusu Gorii vizuri,  na siyo kwa kumkalipia Kama siku zingine, inaonesha umeanza kumzoea tabia zake! Vipi Anelisa anasemaje!?”

“” Hapa nawaza keshoo…!! Alikatisha kwanza kuongea make alikuwa anaenda kuropoka kuhusu Anelisa! Kama akimwambia anaenda kwa Anelisa! Esau atalisanua kwa Bibi.

“” Nilitaka kukwambia.. kesho nataka nikahemee mzigo! Si Unajua dukani kumepungua! Kuhusu Anelisa yeye mzima tu..!”

“” Sawa!! Ila umeshamwambia Gorii! Unavyojisikia Kwake?”

Jolvin ilibidi ashushe pumnzi kwanza, alifikikilia kumbe Esau analitambua hilo, hapana lakini nitakuwa nimewaza tofauti, Ile anataka kumjibu Esau alikata Simu  aliitiwa kazi.

Kesho yake Jolvin alikuwa kajiandaa Asubuhi aondoke, muda huo Alifika Bibi akimuita Jolvin kuwa Gorii anaumwa tumbo linamsumbua! Ilibidi aweke begi kukimbia chumbani Kwake! 

Alimkuta akigalagala kitandani huku kashikilia tumbo akiliminya.

   “” Gorii! Goryanah! Shida Nini Mama!? Ni tumbo linakusumbua!?”

  “” Kaka White.. tumbo linanisokota Kweli!!?”

  “” Sasa hukusema Kama huwa linakusumbua! Tukakutafutia tiba mapema! “Bibi amekula chochote huyu!?”

   “” Hapana labda tumuulize!?”

  “” Goryanah!! Usilale ngoja nikuletee dawa za maumivu.

Baada ya kutoka tu Gorii akawa mzima! Alimtizama Bibi yake Kisha aligonga tano misheni yao imeenda vizuri.

Wakati anarudi Bibi aliekiti kapigiwa simu na mteja anataka nguo yake aliilipia! baadae alikata Simu akawa amerudi kwa Gorii'”

   “” Mjukuu wangu sijui nitakuacha na khari gani!? Wateja wanataka nguo zao! Duka limefugwa pia! Isitoshe huu ni msimu wa chrismass.”

   “” Bibi wewe kafungue! Gorii akikaa sawa nitakwambia!”

Bibi alisogea karibu huku akidai anamuaga Gorii, alimtizama Jolvin ambae kachukua Simu akimpigia Doctor aje.

   “” Bibi Doctor tenaa! Kuna sindano zinafata hapa!?”

Alifanya kuongea chini chini lakini Bibi alimpatia mbinu akawa ameondoka pale.

Baada ya kukata Simu, ilibidi akae akimtizama Gorii ambae alifunga macho akidai anausingizi, Kama angebaki macho angejikuta akicheka! 

Jolvin aliamua kujiegesha kitandani huku akizidi kumtizama Gorii, akizania amelala! Aliamua muda huo kumtizama vizuri! Unaambiwa mtu akishalala ndio utaujua uzuri wake halisi kwa kumtizama.

Alibaki akimtengenezea nywele! Zilizokuwa zimesasambuka kuelekea usoni alifanya kuzirudishia vizuri huku akibaki akitizama Rip’s za midomo yake, baadae alijiegesha pembeni yake huku mkono wake akiunganisha na vitanga vya Gorii, aliongea maneno machache huku akitizama pembeni!

    “” Nahisi kukupenda Goryanah!”

Gorii sauti ilipenya masikioni mwake, mpaka akahisi joto nimezidi nyuzi kadhaa!

Jolvin alisituka huku akifikilia huenda kasikiwa na Gorii! Lakini ndio Gorii anageuka upande wa pili huku akiongea pekee.

   “” Leo ndio nitakoma! Naona nimechokoza nyuki kwenye mzinga wake!”

Jolvin alipokea Simu kutoka kwa Doctor kuwa kafika, Alishuka kitandani kumpokea Doctor!

Baada ya kutoka Gorii alishuka haraka akaurudishia mlango huku akishusha pumnzi ndefu huku akizunguka chumba akitafuta namna ya kumkwepa Doctor!

   “” Mbona tukienda hospitali huwa tunaenda wazima lakini tukipimwa tunaambiwa tunae Malaria au UTI lazima na Mimi niambiwe vile!”

Alifungua mlango Kisha akarudi kitandani, alimsikia Jolvin akimwelezea Doctor.

   “” Ni tumbo la ghafra tu! Limemkamata ameteseka kweli! Nimemkuta kitandani akiweweseka kwa maumivu! Fanya umsaidie haraka Doctor! Akipata nafuu Kuna sehemu naondoka itabidi niende nae Kama khari haitabadilika, na hii ni kwa usalama zaidi Itaendelea Sehemu Ya Kumi Na Tano

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

14 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version