Ilipoishia ” Jolvin aliona aibu hata kumtizama, aliona yeye ndie chanzo Cha yote hayo! Alisimama ili atoke nje lakini Gorii alimuita akaomba chakula.

Ilibidi arudi Kuna hotpot ilikuwa imeshaandaliwa tayari kwa chakula alipakua kwenye sahani Kisha alimpatia.

 Gorii” alibaki akimtizama tu make hawezi kula kwa kutumia mkono kutokana na maumivu ya kidonda.

   “” Nahitaji msaada wako nipate kula!!”

Jolvin hakuwa na budi kufanya vile, alianza kumlisha taratibu Kisha alimuuliza.

“” Mimi ni mwema kwako!? ” 

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA MOJA 

“” Hata mimi Sina majibu! Make sikuelewi tu!?”

   “” Vipi walikufanyia michezo michafu!!?”

“” Sa’ Mbona unaongea huku waona aibu, ila yule Askari nilivoongea kuwa nitamuua, Basi nitalipiza kwa hawa Askari Wenzake, hasa huyu alobaki kunisimamia jana! Yaani kanifanyia vitu vya ajabu! Sipendi hata nisiseme.”

Jolvin alishituka Kwanza huku akishusha sahani ya chakula chini.

     “” Kwahiyoo wamekubaka!?”

     “” Sio hivyo bhana na wewe!!’  , Mimi sipo hivyo! Unaona huu mguu kwenye kisigino na goti alivyokuwa akinipiga Rungu! Lakini nitapona tu! Vipi mama kaja hata kuniulizia?”

Jolvin alifanya kumsitikia tu, sio rahisi Mamake kujireta kituoni wakati ni mualifu.

     “” Kaka White! Itakuwa hajaja ee!? Vipi Bibi nae yupo wapi!?”

Kabla hajajibu, simu yake iliita alikuwa ni Anelisa! Alimuelekeza Hadi sehemu alipo akawa amefika pale. 

Alifika akamtizama Gorii ambae alikuwa akimtizama tu huku alikumbuka maneno aliyoambiwa mara ya mwisho na Anelisa anatakiwa kwenye chumba Cha mahojiano, aseme vizuri kuhusu familia yake ilipo, ilibidi Gorii ajiwahi make hakutaka kuhojiwa.

“” Da Anelisa!! Vipi Kama mtanihoji siku nyingine sahii bado naumwa!”

“” Uhojiwe Nini tenaa!?”

Jolvin aliuliza.

“” Ni kuhusu Familia yangu! Naona Kama nitaongopa kwa hili, Mimi namjua Mama tu, labda Kama ningempata ningemuulizia vizuri.”

“” Aaa basii… Kama hujui hatuwezi kukuhoji ukadanganya mahakama matokeo yako kesi ikazidi kukua!!”

Jolvin alibaki kumtizama Anelisa huku akimfikilia vitu vingi, mbona Kama analeta hoja nyingi nyingi!. 

Anelisa nae alijishitukia lakini alifanya Kama kuvunga alimtizama Jolvin Kisha alimsogelea huku akimtengenezea nywele.

“” Itabidi leo ukapumnzike Nyumbani! Halafu hewa ya hapa naona ni nzito! Mwili wako utafadhaika sana!”

Gorii” alibaki akimtizama Anelisa kwa namna moja au nyingine alihisi sio mtu mzuri kwa Jolvin.

   “”‘ aaa!! lakini Mama kaniachia kumtizama Gorii, siwezi nikaondoka nikamuacha pekee.”

   “” Kaka White.. wewe unaweza ukaenda tu! Mi sahii ninazo nguvu, kuhusu Mama atanikuta! Hata hivyo Rich yupo njiani, tuliahidiana jioni atakuja kukaa na Mimi.”

Jolvin ilibidi aitizame Kama kweli yupo sawa.

“” Nipo hapa nje! Usifikili nimekuacha mwenyewe make huchelewagi kuniwazia vibaya!”

“” Haina Shida ila unakumbuka maneno ya Bibi lakini!? Mimi nakustua karibu anafika hapa, kwahiyo tembea vizuri.”

“” Ilibidi asimame Kwanza Kisha alimgeukia Gorii” “” Ulisikia alichozungumza!?”

 Gorii” aliishia kutabasamu Kisha alijifunika Shuka.

“”” Samahani Anelisa!! Naomba uniache kwanza, kichwa hakipo vizuri! Bibi katuma Ujumbe nimsubili Chumbani kwa Gorii”

“” Okay! Hata hivyo naona upo mzito Sana leo kuongozana na Mimi! Nilitaka kukuaga tu, Byeee!”

Jolvin ilibidi arudi Chumbani kwa Gorii, alitaka kumhoji kuhusu maneno aliyoongea.

   “” Gorii, wewe ulimsikia Bibi kasema Nini kuhusu Mimi!?”

   “” Kwamba, Bibi hamtaki Anelisa! Kumbe mnataka kuoana siku zijazo!?” “Ila wewe Ndio utaamua lakini Kaka White….!! “” Ombi niliokuomba siku yenyewe unipeleke kijijini kwetu nikamuone Mama Muddy, na Muddy pia” itakuwa wamenimisi Sana! Kama ulivyosema Mimi kukaa Nyumbani kwenu nawanyima amani basii niruhusu niende.”

   “” Ndio umezamilia kuolewa na Hammad!? ” Hivi Unajua nilienda kuongea nae vipi ili akuache!? Au ni kwakua hujui tu, ” Nilimwambia wewe ni mchumba wangu na siku za usoni nitakuoa! Ndio akakubaliana na Mimi! Kama utaenda……..,, Kijiji chenu chote kinajua umechumbiwa na familia ya Mishoki! Siona haja ya kwenda kujiaibisha huko!”

   “” A aaa! Kwanini useme mi mchumba wako tena!? ” Si ungejitetea vinginevyo na sio useme vile! Basi Mimi naenda kwao Hammad kuvunja huo uchumba! Na nitasema ni uongo!! Nipo tayari kuolewa na Hammad na sio wewe!!?”

Mabishano yaliendelea baina ya wawili, muda huo alifika Bibi pamoja na Rich wakiwa wamebebelea vyakula mbalimbali kwaajili ya Gorii, khari walioikuta ndani ni kila mtu kakaa pembeni kajitenga huku akiwa kwenye wimbi la Mawazo.

“” Jolvin..!! Khari ya Gorii imebadilika! Mbona hauna raha!?” Bibi Alihoji.

Jolvin hata hakumjibu  aliamua kutoka nje, yeye kilichokuwa kinampa Mawazo endapo Gorii” ataenda Nyumbani kwao halafu akatae yeye si mchumba wa Jolvin na alifanya vile ili kumuwekea ulinzi familia yake itafedheheshwa kwa uongo wa Jolvin.

Huku ndani Bibi ilibidi akae kitandani huku akimshika mkono Gorii” amtizame.

“” Mjukuu wangu kipi tena kinakusumbua! Unaumwa Sana ee!?”

Gorii alimtizama Bibi jinsi anavyomjali, alihisi upendo uliokisiri ndani ya Bibi, aliamua kumkumbatia huku akicheka mpaka Bibi akasituka huku akimtizama Rich.

“” Anapenda utani huyu! Ulitaka Mimi Bibi yako nikose furaha! Ndio umefurahi!?”

“” Hapana Bibi! Mimi nilichukia kwasababu umechelewa kufika! Rich nae sijui ndio mlikuwa mwakokotana njiani,, Ani mmechelewa!!?”

“” Basi Basi… Rich mpatie chakula Dada’ko! Naona kamepungua Kweli…

“” Bibi Nenda nje Jolvin kakusubili kwanza, Ila Kaka anadekaga huyo kwako daaah!”

Bibi ilibidi awapishe, Rich alipakua chakula kiasi Kisha alianza kumlisha Gorii” huku stori zikiendelea.

“” Vipi Kaka white kakujali kama Mimi navyokujali!? Make yeye muda wote hufurahikaga na Anelisa tu!”

 

“” Kafanya Kama wewe! Ila wewe ni zaidi, yeye ni kuulizaga maswali tu eti ” Mimi ni mwema kwako!?” Hivi ningemjibu vipi Rich!?”

“” Kaka nae mtata kwahiyo akawa anagongelea nyundo tenaa!!?”

“” Ushaanza viudadisi vyako vya kijinga! Nipe majibu kwanza.”

“” Ungemwambia huenda ni Mwema ila sijui Kama ni Mwema! Fanya kitu nipate majibu ya swali lako!?”

Ilibidi wote wacheke, lakini huku kwa Bibi Baada ya kukutana na Jolvin, ilibidi wakae sehemu kwanza wazungumze! Jolvin aliamua amweleze kilichotokea siku yenyewe mpaka Hammad akakubali kuwa mbali na Gorii, na mpaka maamuzi ya Gorii aliyoyachukua kwasasa.

   “” Kumbe ni hicho tu Mjukuu wangu! Wewe mpeleke kwao akasalimie Ndugu zake! Najua kama utafika pale watakuchukulia Kama mme wa Gorii” make taarifa Kijiji kizima wanajua umemuoa Gorii! Kwahiyo Gorii hatokubali aaibike kuwa kakukataa mbele ya watu! Watamchukulia mtu wa ajabu lazima akubali tu!”

   “” Lakini Bibi hii michezo michezo itakuja kunifunga baadae! Mimi nataka Gorii akaseme tu kuwa nilifanya vile ili kumlinda yeye! Na akishasema Mimi nitatafuta njia nyingine ya kukabiliana na Hammad!”

“” Najua unataka ujitoe kwenye dili lako ni sababu ya Anelisa!? Kwanza Binti huyu muongo, Mamako kafatilia kila kitu kuhusu hizo pesa!! na inasadikika ni milioni moja iliyochukuliwa na sio million tano! Nahisi Kuna kitu wanakitaka kwako au kwa huyu Binti wa watu.

Ghafra walisikia mtu akiwapigia makofi, alikuwa ni Gorii” kapatiwa muda wa kufanya mazoezi ili viungo vyake vikae vizuri, katika pita pita ndio  akabahatika kusikilia maneno ya mwisho mwisho, aliamua kumjibu Bibi.

   “” Bibi hata usihangaike kujua kipi wanachokihitaji, Wewe kubali Mimi nikakae mbali na hii familia ya Mishoki, uone Kama Anelisa ataendelea kuleta michezo ya kijinga! Sema yeye hawaambii tu..  ila ni kwamba, Anelisa hataki ukaribu wa Mimi na Jolvin! Kwasababu ndie Mwanaume wake wa ndoto zake kwa baadae! Halafu Jolvin wewe Ndio wataka kunifanya nichukiwe zaidi na Anelisa…

Kabla hajajua kuwa ulinitetea kwa Hammad ukidai Mimi ndie mchumba wako! Basi mwambie mapema nisije vunjwa miguu Mimi na Yule Askari wake aliyemlipa pesa!! Mamangu bado ananihitaji ujue!?” Itaendelea Sehemu Ya Kumi Na Mbili …….

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

11 Comments

Leave A Reply


Exit mobile version