Ilipoishia ” Bibi hata usihangaike kujua kipi wanachokihitaji, Wewe kubali Mimi nikakae mbali na hii familia ya Mishoki, uone Kama Anelisa ataendelea kuleta michezo ya kijinga! Sema yeye hawaambii tu..  ila ni kwamba, Anelisa hataki ukaribu wa Mimi na Jolvin! Kwasababu ndie Mwanaume wake wa ndoto zake kwa baadae! Halafu Jolvin wewe Ndio wataka kunifanya nichukiwe zaidi na Anelisa…

Kabla hajajua kuwa ulinitetea kwa Hammad ukidai Mimi ndie mchumba wako! Basi mwambie mapema nisije vunjwa miguu Mimi na Yule Askari wake aliyemlipa pesa!! Mamangu bado ananihitaji ujue!?”

Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

 

   “” Askari yupi tenaa!? Bibi alihoji kwa mshangao.

  “” Jana mlipoondoka tu,  Anelisa alifika akamuita Askari mmoja! Yule aliyekabiziwa kunitazama nilimuona akimuachia nafasi yule Askari alieongea na Anelisa, alishikishwa kiasi Cha pesa alitoka  akifurahi, Baada ya hapo yule Askari aliebakia alianza kunishurutisha vibaya mara simama, kaa, inua mikono juu, ruka kichura hata nilipomwambia nmechoka alinipiga na rungu huku akinitishia nikae mbali na hii familia! Kama nitaendelea kukaa karibu nayo Mama’ngu sitamuona Tena!  kuliko nimpoteze Mamangu bora nirudi kijijini kwetu!

Gori alimaliza kuongea huku akirudi hospitali kubeba kila kitu chake aondoke. Huku kwa Jolvin alikuwa haamini Kama Anelisa anaweza kufanya vile!

   “” Hivi Bibi unamwamini Gorii! Kwa Maneno aliyoyasema!? ” Naomba tulifanyie uchunguzi kwanza!”

Bibi muda wote alikuwa kimya akimfikilia Gorii Kama ataondoka itakuwaje!

   “” Bibiii ..!! 

Jolvin alimuita tenaa.

   “” Niache kabisa! Kwa kumwamini Anelisa leo unaenda kunitenga na Mjukuu wangu anae nipa furaha muda wote!”

Gorii ndio anarudi raratibu huku kashikilia baadhi ya nguo zake kwenye mfuko! Alijitahidi kupiga hatua huku akimfuata Bibi.

   “” Huu mguu nao unasumbua kweli! Huyu mla rushwa kajua kuninyosha!”

Jolvin na Bibi walibaki kumtizama Gorii jinsi anavyokuja akijivuta mdogo mdogo! Ilifikia hatua mguu ukagoma ilibidi asimame kwanza huku akiutizama mguu!

   “” Atakuwa kaumia Sana Gorii!! lakini naona anajitahidi kujikaza!”

Huku kwa Gorii Baada ya kuutizama vizuri aliona ukivuja damu, Jolvin aliamua kumfuata baada ya kuona kasimama kwa muda mrefu! Alibaki kujiuliza kimya kimya.

 “” Gorii itakuwa waumia Sana!!?”

Baada ya kumfikia Gorii” Ilibidi amtizame kwanza usoni kisha aliongea..

   “” Muda mwingine ni Kama unakuwa mwema kwangu!?”

Jolvin aliamua kumbeba huku akimpeleka kwenye gari pasina kumjibu kwanza, Bibi nae alifatia pamoja na Rich ambae muda huo alienda kuongea na Doctor.

Baada ya kufika Nyumbani! Walimkuta mama kawaandalia chakula, ilikuwa ni surprise ya khari ya juu make mama alikuwa haingii jikoni na Kama akiingia huwa anaandaa chakula muhimu kwa mtu muhimu.

Walikaa mezani wakawa wakiendelea kula, siku hiyo meza ilichangamka kweli familia ilikuwa ikimpenda Gori na ilifurahi kumuona yupo mzima. 

Gorii”  aliona upendo wa hiyo familia akawa anawaza hata jinsi ya kuondoka pale familia ataiaga vipi, lakini alipiga moyo lazima ataondoka, baada ya kumaliza kula Gorii’ ilibidi akohoe kwanza Kisha aliongea.

   “” Mama, Bibi, Kaka zangu! Kwanza nashukuru kwa kunihifadhi nikae hapa! Nimekaa muda mwingi lakini naona hata Mamangu nae kakaa mbali na mimi hataki hata kuniona! Mimi nilifanya makusudi kumpiga yule Askari ili nikamatwe nibakie pale nikiamini siku Mamangu akikamatwa ataletwa kituoni nami nitamuona! Kama alirudi kijijini kutaka msaada naimani atarudi tenaa kwa mara nyingine. Kitu ninachokiomba kwenu naomba Jolvin anipeleke Nyumbani tu.

   “” Aa aa! Sa Gorii akiondoka humu ndani tutaishije! Kina Kaka nao likizo inaelekea kuisha! Mimi sitakaa mwenyewe labda niambatane na Gorii”

Rich aliongea huku akiwafanya Wenzake wamtizame.

  “” Hata Mimi nimeomba uhamisho! Mafunzo yangu ya chuo nitamalizia huku kwa muda uliosalia, nahitaji kukaa na familia yangu karibu.”

Jolvin aliongea, ni kitu kilichowasitua sana, hata familia ilikuwa haina habari juu ya Hilo, Upande wa Bibi yeye alijawa na furaha aliamua kuongea.

   “” Kama Jolvin atabakia Basi na Gorii abaki, hii nyumba itakuwa na furaha wawili hao Kama watakaa pomoja katika hii nyumba.”

   “” Lakini Bibi… Jolvin atakuchukulia uangalifu! Kama atahamia hapa kimasomo Mimi naweza nikaondoka tu!”

   “” Kama hutakubaliana na bibi, Basi hata Mimi sitakaa hapa nyumbani nitakufuata huko kwenu, si wewe umekaa hapa, Basi tupishane!?.”

Gorii” ilibidi acheke kwanza make akiangalia mazingira ya Nyumbani kwao kulivyo kijijini, bado chakula Cha kule ni mboga moja mezani siku imepita, alihisi kumhurumia kwanza.

“” Lakini Rich.. unayajua maisha ya Kijijini Kweli! Huko hawaishi Kama huku mara ule nyama, kuku huko ni mboga mboga pamoja na dagaa!”

Mama Ilibidi aingilie make mijadala ya Hawa watoto anaijua mwenyewe.

   “” Gorii” mwanangu Mimi sikukatazi kwenda Nyumbani kwenu! Ila iangalie pia hii familia siku ukiondoka utaiachaje!? Familia kwa ujumla tunakupenda sana! Nilitaka ubakie hapa usome Kwanza, tayari nimekutafutia chuo na mwezi wa kwanza ulitakiwa uanze, Kuna baadhi ya mahitaji nimeyakamilisha! Naomba uamue mwenyewe ila nilitaka ukasalimie kwenu halafu urudi uendelee na masomo! Katafakari usiku wa leo utanipatia majibu kesho Asubuhi!.

Gorii alibaki amepigwa butwaa, Ndoto aliyokuwa akiipenda ni kusoma ili apate kazi, na Kama atashidwa lazima apambane kutafuta kazi, je ni kazi gani atapata endapo hajasoma!?” Hili lilikuwa swali Kwake lakini leo hii linatatuliwa.

Hata usiku alipoenda kulala alikuwa akiwaza Jambo Lile lile, kabla hata hakujapambazuka vizuri aliwahi kumgongea Mlango Mamake akimwambia ataenda kijijini Kisha atarudi kusoma.

Yapata wiki moja kuisha Gorii” alikuwa tayari kapona, afya yake ilirudi Kama awali, siku hiyo walikuwa mjini wakihemea baadhi ya zawadi ya kuondoka nazo, hata ilipofika siku ya kesho yake Gorii pamoja na Jolvin walikuwa njiani wakielekea kijijini.

Baada ya kufika walielekea Hadi kwa Mama Muddy, walipokelewa vizuri! Make walikuwa wameandaa chakula kingi Kama unavyojua mambo ya Kijijini ni wali nyama, soda! imeisha hiyoo.

Siku hiyo Jolvin alikalibishwa Kama mkwilima kwenye nyumba ile, Baadae Mama Muddy aliomba aongee na Gorii”

   “” Tulisikia habari ya kuolewa na Kijana toka familia ya Mishoki, hongera Sana make mnaendana kwa kila kitu!”

   “”Sawa’ Mama, lakini Muddy yukowapi mbona simuoni!? Vipi kuhusu Mamangu umenigusia kuwa ulipata taarifa kwamba kaiba pesa kwa watu! Sijui alienda kuzifanyia kazi gani!?”

   “” Nimeshalipoti kwa mjumbe kwa pamoja wanamfafuta! Halafu Hammad kaoa! Kama siku tatu zimepita, kwasasa yupo kwenye mapumnziko mjini.”

Wakati wakizidi kuongea Muddy ndio anakuja, alikuwa na baskeli ndogo akiendesha kwa kasi kumuwahi Gorii, Alifika Nyumbani akapaki baskeli akimuita Gorii”

Gorii baada ya kusikia sauti alitoka mbio akikimbia alifika akamkumbatia Muddy huku wakiendelea kuruka ruka kwa furaha! 

Muda huo Jolvin yeye alikuwa akitembea tembea na vijana wa pale Kama wenyeji wake, wakati anarudi ndio anakuta position ya Gorii akiruka ruka na Muddy. Jolvin alimtizama Muddy aliona Kama anamuumiza Gorii ilibidi amzuie.

   “” Wewe kijana!! Anaumia huyoo!!?”

Gorii” ndio anageuka kumtizama Jolvin, alibaki akicheka tu.

   “” Kaka White! Haniumizi bhana ni utani tu huu, hata hivyoo hii ni michezo tuliyokuwa tukiicheza na Muddy!”

Muddy mwenyewe hata hakuwa akijali, alisogea Tena akamshika kichwani.

   “” Nywele yako sahii ina matunzo, hivi unakumbuka niliwahi kukwambia wewe ni mzuri!”

Gorii” alitabasamu Kisha alimvuta masikio huku akimwambia.

   “” Nikiwa narudi! Nitaenda kukuombea ruhusa kwa Mamake na Jolvin na wewe uende shule!? Au ushabadili maamuzi ya shule!?”

   “” Kwahiyo wewe sahii unasoma!?”

Kabla hajajibu Mamake Muddy alifika akamuita Muddy! Ilibidi amweleze kwa kina baada ya kumuona Muddy anamzoea Sana Gorii, kuwa kwasasa Gorii ni mchumba wa mtu anae muona pale!

Huku kwa Gorii” aliamua atembee tembee na Jolvin kuelekea kwenye mashamba yao! Walifika kwenye shamba la mihogo ilibidi wakae pale huku wakiendelea kutafuna mihogo. 

Muda huo Jolvin alikuwa hoi kwa kutembea, make Gorii alikuwa akimtembeza umbali mlefu, alivyochoka aliomba apumnzike kwenye kimvuli Cha mti wakawa wamepunzika wote! 

Huku kwa Jolvin ilikuwa mbinde kila akilala alihisi Kama anachafuka, Gorii aliliona vile ilibidi asogee karibu huku akimruhusu aegame miguuni Kwake.

   “” Kaka White! Naona unahangaika Sana nilikwambia kwetu kijijini! Ani umepauka hiyo midomo kwa kutafuna mihogo.””

   “” Nifute basii… Si Mimi mmeo!?”

   “” Alitabasamu tu huku akimfuta..”

Jolvin aliamua kukaa ili amtizame vizuri Gorii akizungumza.

“” Huwa una macho mazuri na nywele zako laini Kama wale waarabu weusi!” 

   “” Utani huo!! Itakuwa nimefata kwa mama! Make hata yeye ana nywele Kama zangu!”

“” Mamako anaonekana kuwa mrembo Sana! Halafu Gorii Unajua leo uliniuzi sana! Tabia gani ya kuchekeana na Muddy mpaka muanze kushikana, mkumbatiane! Bado unaniita Kaka white! Hujui Mimi na wewe tu wachumba!?”

Mara Simu yake iliita alikuwa ni Anelisa, alimtizama kwanza Gorii, nae kamtolea jicho alijua kabisa atakuwa ni Anelisa. Ilibidi asimame pale awapishe waongee kwa uhuru lakini Jolvin alimshika mkono huku akimruhusu abakie, Gorii ilibidi akae Kama afande make hakuna kitu ataongea mbele ya wapenzi wawili wakiongea na yeye ni mtu baki.

Jolvin alipokea Simu ili amsikilize Anelisa, alichoamua ni kumvuta Gorii” akamlaza miguuni Kwake huku akizidi kuchezea nywele zake! 

   “” Nipo kijijini! Kwao Gorii nimemleta kuona familia yake baada ya siku tatu tutarudi! Halafu nikirudi nina mazungumzo nawee!”

  “” Jolvin umebadilika sana, unatoka hata kaniambia hamna, au yote ni sababu ya Gorii!?”

  “” Ni mdogo wangu, Dadangu pia kwasasa ni familia yangu kwahiyo nafanya kama majukumu ya familia!”

Anelisa alichukia akakata Simu, Jolvin alibaki akimtizama Gorii, Kuna vitu alianza kuviona kwa Gorii vilianza kumvutia taratibu hata yeye akawa anashangaa!

   “” Goryanah!! Usingizi tayari!!?”

   “” Ooh! Umeniita Kama mama kabisa!! ” Bora hata nimepitiwa usingizi sijamsikia Anelisa, Lakini Kaka White… Huwa unampenda Anelisa tofauti na urafiki! Yeye anakupenda wewe!”

Jolvin ilibidi ang’ate midomo kwanza Kisha alimuinua Gorii, akimuweka sawa.

  “” Aaa.. Goryanah! Anelisa ni rafiki yangu tu! Hata wewe unahisi kuwa mi nampenda!?”

   “” Sijajua nyie! Mi nitajuaje Sasa! Make upendo huzaliwa ndani ya mtu! Ndio huanza kuhisi anampenda! Labda mshapendana tayari.”

   “” Wewe unampenda Muddy!?”

   “” Rafiki yangu bhana! Wewe hujui kutofautisha Mahusiano ya kirafiki!?”

Jolvin ilibidi atulie kwanza, akimtizama Gorii, kumbe huwa ana maneno ya utu uzima, ilibidi amuulize..

   “” Goryanah! Sahii una miaka mingapi!?”

   “” Ishirini kwa Sasa! Make nimeondoka huku siku ya birthday yangu ya kutimiza miaka kumi na nane! Hammad alipania kunioa eti mi mkubwa si Bora sahii nimekuepo.”

Jolvin alitabasamu tu, huku wakisimama waondoke! Wakiwa njiani ilibidi amuulize;-

“” Vipi Rich unamfikiliaje!? Naona mpo karibu Sana!?’

“” Aa kale.. ni kajinga kajinga tu.. Anyway, ni karafiki kangu huwa nafurahia kampani yake!”

“” Unavopenda kingeleza sasa…. Hivi  Gorii Ushawahi kuwa kwenye kwenye Mahusiano! Kabla hujaja kwetu!?”

“” Kaka White! Mimi sipendagi mambo ya hivo! Nawazaga kutafuta pesa kwanza! Mamangu aishi vizuri ikiwezekana aishi Kama mamako anavyoishi.”

Jolvin alicheka huku akimbinya mkono.

   “” Natamani Ndoto zako zitimie hata mimi! Nitakuwa karibu yako kuzitimiza!”

  “” Wewe hapana! Halafu si bado wasoma lakini? Mimi nikianza kusoma wote tunakuwa wanafunzi! Hapo ni kila mtu atakuwa akitafuta maisha yake ya Baadae.”

   “” Kaa kimya.. tumefika Nyumbani, make unaongea sana!”

Baada ya kufika Nyumbani, walikuta kumetulia japo umeme ulikuwepo muda huo Muddy alikuwa kwenye Mawazo Sana kila akikumbuka maneno ya Mama kuwa Gorii kaambatana na mchumba wake ilimuuma Sana, alitegemea siku moja angemuoa!

Gorii alimuacha Jolvin sebuleni wakiwa wamekaa na Muddy kila mtu kaupiga wa kimya! Ilibidi Jolvin amsemeshe.

“” Muddy!! Wewe ndie rafiki wa karibu na Gorii! Muda wote huwa haishi kukuzungumzia!”

Baadae Gori alirudi huku kashikilia sahani yenye papai zilizokatwa katwa alifika Hadi kwa Muddy akachukua kipande akamlisha. Kisha alielekea kwa Jolvin ambae alivunga kuangalia taarifa ya habari.

Gori alimsogelea karibu Kisha alikaa karibu yake, aliushika ule mkono uliokuwa umeshikilia remote akamshikisha kwenye sahani.

   “” Ulivonuna,, ulizani hautakula? Kwa watu ninaowapenda huwa napenda wote wawe na furaha! Hata wewe nitakulisha!”

Jolvin alibaki kuenjoy, baada ya kusikia vile, alifanya kumlisha pia. Japo Gorii yeye alifanya Kama kamlisha Kakake ila yeye alichukulia tofauti kabisa, kale ka upendo kalizidi kuzalishwa.

Hatimae siku za kukaa kule ziliisha Gorii pamoja na Jolvin ilibidi warudi Nyumbani!

Huku maandalizi yalikuwa mazuri kila mtu alikuwa akiwasubilia kwa hamu Sana ili wawaone.

Upande wa Rich siku hiyo walikuwa wametoka na Sophia kutembea make zilikuwa ni siku za mwisho mwisho Rich aende chuo, siku hiyo waliamua kufurahi kwa pamoja huku wakitembea tembea baadhi ya sehemu zenye starehe!

Majira ya jioni Rich ndio anarudi, alimkuta Kakake Jolvin akimsubili getini, ile anagonga geti ndio anafunguliwa na Jolvin.

   “” Wewe Rich, yaani nikishaondoka tu, unaanza kutembea tembea usiku ovyoo! Ndio ulienda kuonana na huyo Sophia?”

Rich alishidwa kujitetea ilibidi akubali huku akimuomba msamaha.

   “” Na mkononi umebeba Nini!?”

   “” Zawadi kwaajili ya Gorii!”

   “” Zawadi…!!?”

   “” Ee!!”

   “” Si maua hayoo….!”

Rich ilibidi ampatie Jolvin, huenda kamchukulia tofauti alianza kujieleza.

   “” Samahani Kaka.. hii ni zawadi huwa unampatia mtu aliyekuwa mbali na wewe! Ni kuonesha ulimkumbuka tu! Pia unamtakia kheri, ya kumshukuru katika Safari yake kafika salama.”

   “” Oooh!! Sawa! Ila uwe unawahi! Humo ndani wote wanakuwaza wewe! Umewakosesha amani, hasa Bibi na Gorii!”

   “” Nimekuelewa kaka! Sitarudia tenaa!”

Alifika Hadi sebuleni, familia kwa ujumla walisimama kumpokea.

   “” Ulienda wapi Rich? Siku ile ulipotea ghafra aliyekuokoa ni Gorii, na leo tenaa unarudi muda huu! Huoni familia nzima haina amani! Muone Gorii kafika anakuulizia muda wote na wewe haupo! Kajisikia vibaya ujue.”

Rich alimtizama Gorii, ambae alikuwa akimtizama alijua kabisa ashajua kama alienda kuonana na Sophia, lakini Rich aliamua kumkonyeza asizunguze kitu!

   “” Njoo bwana! Mi nilikumisi! Wewe hauwezagi hata kupiga simu unijulie khari! Sijapenda”

Rich ilibidi amsogelee Kisha alimkumbatia huku akikaa karibu nae! Walianza kula kwa pamoja huku michezo yao ikiendelea kimya kimya.

Jolvin alikuwa akiwatizama, mwisho kabisa alichukizwa na kitendo kile alitoka nje kupunga upepo make ndani kulikuwa na joto.

Esau aliona Kama Jolvin hayuko sawa aliamua kumfuata Hadi nje huku akiwa na kinywaji.

“” Vipi Jolvin! Safari yenu ilikuwaje!? Halafu mbona hauna furaha!?”

“” Hapana nipo sawa Esau! Rich amebadilika siku hizi! Yaani kawa na mazoea ya ajabu ajabu! Sijui kamuiga Gorii!”

“” Ni kawaida yake mbona.. au umemsahau!?”

“” Ndio wanakuwa wakikumbatiana na Gorii! Mbele ya Wazazi hata hawaogopi! Yaani tabia zingine humu ndani zinaboa!”

Alisimama huku akielekea chumbani Kwake! Muda huo alikuwa amefura hasira! Lakini Esau ni mtu mkubwa alielewa kipi kinamsumbua mdogo Wake, aliwaza namna ya kumsaidia japo itakuwa ngumu Gorii, akamuelewa kwa akili yake ya kitoto kitoto kazi ipo. Itaendelea Sehemu Ya Kumi Na Tatu …….

Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako 

Ulipitwa na SIMULIZI NYINGINE? 

SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya Goryanah Kumtumia Chochote

Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

 

20 Comments

  1. Daaaaah I can’t wait To see Gorii na Jolvin pennziniiii….admin ubarikiwee tutolee mbil kwa Siku bbaaaaas🙏🙏🙏🙏

    • Hii stori ni ngumu kutabiri mwelekeo wake, Gori kiu yake ni maisha, vijana wanamfikilia kimapenzi, sijui ni njia ipi itamsaidia kufikia ndoto zake za kuwa na maisha mazuri, je nikupitia kuolewa na familia tajiri au atapambana mwenyewe, mama yake Yuko wapi? Hapo patamu

Leave A Reply


Exit mobile version