Kwa mujibu wa mtandao wa SkySports kutoka nchini Uingereza umeripoti kuwa kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ataukosa mchezo wa wikiendi hii ambao watakua ugenini kukipiga dhidi ya Aston Villa.

Kocha huyo wa washika mitutu wa London alipata kadi ya njano wakati akishangilia goli la dakika za mwisho kabisa la Declan Rice ambapo lilibadilisha matokeo kutoka 3:3 na kushinda 4:3 mbele ya Luton usiku wa Jumanne.

Kadi hiyo ni ya 4 kwa Arteta ndani ya msimu huu inayompelekea kupata adhabu ya kutokuiongoza Arsenal mbele ya Aston Villa wikiendi hii.

Arsenal wanawafuata Aston Villa wakiwa na rekodi ya kushinda mechi 12 bila kupoteza nyumbani.

Leave A Reply


Exit mobile version