Huku Kundi B AFCON 2024 ikiendelea huko Abidjan, wapenzi wa soka wanajiandaa kwa mechi ya kusisimua ya Egypt vs Ghana.

Hii itakuwa mara ya tano kwa Misri na Ghana kukutana katika African Cup of Nations.Wamekutana mara tatu awali katika hatua ya makundi (ushindi mmoja kwa kila upande, sare moja, na jumla ya mabao mawili kwa kila timu) Historia inaonyesha ushindani mkubwa, na Misri ikiwa na rekodi nzuri ya kushinda mechi dhidi ya Ghana.

Misri wana historia nzuri ya mafanikio, imeshapoteza mechi moja tu kati ya 20 zilizopita katika hatua ya makundi ya African Cup of Nations (W14 D5), ikiwa ni kichapo cha 1-0 dhidi ya Nigeria mwaka 2022. Baada ya kutoka sare ya 2-2 na Msumbiji siku ya kwanza,waliwaruhusu  Msumbiji kufunga mabao mawili, nao pia wanahitajika kua makini katika eneo lao la ulinzi.

Wana wa Pharao wanatazamia kuepuka kufungwa katika michezo yao miwili ya kwanza ya kundi kama ilivyotokea mwaka 1992.

Ghana inakabiliwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika mashindano haya, na wanahitaji kuboresha eneo lao la ulinzi ili kuepuka kutolewa mapema. Ghana walipata kichapo cha 2-1 kutoka kwa Cape Verde siku ya kwanza ya AFCON.

Na katika Historia yao hawajawahi kupoteza mechi zao mbili za kwanza katika mashindano tangu mwaka 1984, walipopoteza dhidi ya Nigeria na Algeria.

Mohamed Salah wa Misri amefunga jumla ya mabao saba katika CAF African Cup of Nations, ni mchezaji wa kwanza wa Misri kufunga katika mashindano manne tofauti ya AFCON (2017, 2019, 2022, 2023).

Ni mchezaji muhimu wa kutazamwa na mabeki wa Ghana kwa umakinimkubwa sana, uwezo wake wa kufunga unaweza kuwa changamoto kwa timu ya Ghana.

Kuelekea mchezo huu utakao kua wakusisimua na kutolewa macho na mashabiki, timu zote zinapaswa kuzingatia mambo muhimu:

  • Ghana imekuwa ikifunga mabao mengi kutokana na set pieces. Hii inaweza kuwa fursa kwao kuchukua faida ya mipira ya kona na free-kicks.
  • Ghana Wanapaswa kuboresha ulinzi wao na kuepuka kuruhusu mabao mengi. Pia, wanaweza kutumia uzoefu wa wachezaji kama Mubarak Wakaso kuleta matokeo chanya.
  • Misri Kwa kuwa wamepoteza mechi moja, wanahitaji kuimarisha ulinzi wao. Kupata matokeo mazuri ya awali dhidi ya Ghana inaweza kuwapa msukumo.
  • Kupunguza makosa ya kujihami kunaweza kuwa muhimu kwa pande zote kufanikiwa.
  • Kutumia vizuri Vipaji walivyo navyo, Timu zote zina wachezaji wenye uwezo mkubwa, kama Mohamed Salah kwa upande wa Egypt na Mubarak Wakaso kwa upande wa Ghana.

Kutumia vipaji vyao vyote kunaweza kuwa ufunguo wa ushindi.Kwa mtazamo wakisoka, mchezo unaweza kuwa mkali na wenye ushindani, na timu zote zinahitaji kutumia mbinu mbadala ili kufikia matokeo mazuri.

Soma zaidi: Takwimu na uchambuzi mbalimbali Hapa

Leave A Reply


Exit mobile version