Kama ulikua hujui basi nikutaarifu kuwa Getafe dhidi ya Rayo Vallecano ni mechi inayowahusisha watani wa jadi kutoka Kusini mwa jiji la Madrid na mechi hii itachezwa katika uwanja wa Wanda Metropolitano.

Getafe wanaingia katika mchezo huu wa ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga wakiwa na rekodi ya kushinda mechi 3 wakisare mchezo mmoja na kupoteza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Las Palmas kwa jumla ya magoli 2 kwa 1.

Rayo wao wanaingia katika mchezo huu wakiwa wameshinda mchezo mmoja pekee katika mechi 5 zake za La Liga huku aksare mchezo mmoja na kupoteza michezo 3 na yeye akipoteza mchezo wa mwisho kwa kufungwa mabao 4 kwa sifuri kutoka kwa Athletic Bilbao.

Ukiutazama msimamo wa La Liga klabu ya Getafe yuko nafasi ya 8 na alama zake 26 katika mechi 18 huku Rayo akiwa nafasi ya 11 na alama 20 katika mechi 18 alizocheza mpaka sasa.

Katika mechi ambazo mara nyingi wamekutana wao kwa wao hakuna mchezo uliowahi kuzidi mabao 5 na mchezo ambao ulikua na mabao mengi ni ambao uliisha kwa Rayo kuondoka na ushindi wa mabao 3 kwa sifuri huku mchezo wao wa mwisho kwa msimu wa 2023 ukiisha kwa sare ya bao 1:1.

VIDOKEZO VYA MKEKA

Kwa namna rekodi zilivyo wakikutana katika dabi hii licha ya kiwango kibovu cha timu moja kwa mechi zake 5 za mwisho SIKUSHAURI kutoa ushindi wa moja kwa moja kwani hawatabiriki hawa.

Unaweza kuweka mkeka wako kwa upande wa magoli wa klabu mojawapo kwamba ashinde kuanzia bao moja mfano ( Getafe Goals Over 0.5)

Kama unaona kuna nafasi ya Rayo Vallecano kutopata magoli mengi basi unaweza kumpa asipate magoli kuanzia 4 yaani ( Rayo Vallecano Under 4.5)

Endelea kufuatilia zaidi kuhusu vidokezo na takwimu za kabla ya michezo mbalimbali kwa kusoma hapa.

 

1 Comment

  1. Pingback: Real Madrid vs Mallorca : Utabiri Na Vidokezo Vya Mkeka - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version