Klabu ya Azam imeendelea kuonesha balaa lao katika ligi kuu Tanzania bara kwa kuwafunga klabu ya KMC Mabao 5 kwa 0. KMC walipoteza idadi kama hiyo dhidi ya Yanga SC na mabao ya Prince Dube aliyefunga mawili, Feisal  Salum akifunga moja, Djibril Sillah akifunga moja naye pamoja na bao la kujifunga la Ismail Gambo ambayo yametosha  kuwakanya watoza Ushuru hao wa Kinondoni na kugomewa kukusanya Ushuru kwenye Wilaya ya Temeke.

George Ambangile ni mchambuzi wa soka kutoka Wasafi ambae baada ya mchezo ameweza kutoa uchambuzi wake na kusema yafuatayo:

Kati ya wachezaji ambao wananivutia sana kuwaangalia kwenye ligi yetu basi ni hawa wawili pia : Kipre Jr na Sillah na jinsi pia wanavyotumiwa na makocha wao

Kwa hali ya kawaida huwa tunaona mawinga wakiwa pembeni basi mafullbacks wao wana overlap ( wanapita nje yao ili kupiga krosi ) lakini ni tofauti kwa Azam FC na nafikiri matumizi ya fullbacks wao ndio inawapa makali zaidi mawinga wao na pia inaboresha ushambuliaji wao …. wanatumikaje ?

Wachezaji wa Azam Fc wakifurahia moja kati ya bao ambalo wamewafunga wachezaji wa KMC. Mchezo uliomalizika kwa Azam kuondoka na ushindi wa bao 5:0

1: Mara nyingi Kipre na Sillah wakiwa pembeni zaidi ya uwanja kulia na kushoto basi fullbacks wao ( Lusajo na Sidibe/ Msindo ) huwa wanafanya ‘ UNDERLAPS ‘ yani badala ya kupita nje yao wenyewe wanapita ndani yao hii inasaidia nini ?

2: Hii inawapa fursa Kipre Jr na Sillah wanapata 1v1 na mabeki wa pembeni wa timu pinzani ambao huwa wanakosa msaada kutoka kwa mawinga wao … na kwanini wanakosa msaada ?

3: Kwasababu zile Underlaps za fullbacks wao maana yake mawinga wa timu pinzani wanalazimika kuwafuata hao mafullbacks wa Azam FC ndani ya uwanja .

4: Ushambuliaji unaboreshwa vipi ? Kwasababu fullbacks wa timu pinzani wanalazimika kuwafuata wingers wa Azam FC basi distance inakuwa kubwa ( Gap ) baina ya hao fullbacks na mabeki wao wa kati kwahiyo hiyo space iliyo wazi ndio mara nyingi FEISAL huwa anaitumia kuishambulia au kufanya safari zake kwenye penati box akiwa kama mshambuliaji wa pili .

5: Na Azam FC wanafanya hivyo bila kuharibu muundo wao wa ulinzi wanahakikisha nyuma watu wanne wanabaki ( mabeki wawili wa kati na mbele yao viungo wawili wa kati ambao wanakuwa tayari kwa ajili ya second balls na pia kukabiliana na counter attacks za timu pinzani )

Aidha Ambangile anasema kuwa Ili vyote hivyo vifanye kazi vizuri vinategemeana na ufanisi wa Wingers wao Sillah na Kipre Jr kwenye ” Duels ” za 1v1 na fullbacks wa timu pinzani na siku hizi Sillah na Kipre Jr wanawatafuna sana mafullbacks wa timu pinzani .

Ile combo ya Sillah Kipre Feisal na Dube inahitaji kuwa fit ( majeraha yapite pembeni ) wametengeneza combination nzuri .

Singida Fountain Gate kukipiga Karatu mechi zake 2 kwa undani zaidi soma hapa .

Leave A Reply


Exit mobile version