Uongozi wa Geita Gold umeweka wazi timu hiyo itaachana na mastaa 10 ambao hawatokuwa tena sehemu yao msimu ujao, huku miongoni mwa waliofyekwa ni Mjapani, Shinobu Sakai ‘Shino’.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Simon Shija alieleza sababu kubwa ya kuachana na mastaa hao ni kutokana na kumaliza mikataba yao na kutoridhishwa na viwango vyao.

“Kwa sasa tumewapa barua wachezaji saba lakini wengine watatu bado tunaendelea kuongea nao tena na kama tutashindwana basi nao tutawafungulia mlango wa kutokea japo hatutamani hilo kutokea.”

Shija aliongeza moja ya mchezaji waliopo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya ni Elias Maguri ambaye wanatamani kuendelea naye msimu ujao baada ya kuonyesha kiwango kizuri tangu ajiunge nao.

Wachezaji waliopewa ‘Thank You’ ni; Fabrice Kayemba, Arakaza MacArthur, Shown Oduro, Mussa Gadi, Jeremiah Thomas, Daniel Lyanga aliyetua JKT Tanzania na Mjapani Shinobu Sakai ‘Shino’.

Shinobu alijiunga na Geita Gold mwaka jana na kubeba matumaini makubwa kwenye kikosi hicho ingawa ameshindwa kupigania namba huku ikielezwa yuko mbioni kujiunga na Tokyo International ya nchini kwao.

Kwa taarifa zaidi za usajili tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version