Ukiutazama mchezo huu ni wazi kuwa klabu ya Simba wataingia huku wakiwa na lengo kubwa moja ambalo ni kuondoka na alama 3 baada ya kupata sare mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc na tambua kuwa bado Simba itaendelea kucheza chini ya presha inayotokana na timu ambazo zipo juu yake ambao ni Azam na Yanga na haswa ukiwaza kuhusu kwenye mbio za ubingwa wa Ligi ya NBC msimu huu.

Katika mchezo huu ambao Geita ni mwenyeji na unachezwa katika uwanja uleule ambao Simba ametoka kupata sare ni wazi kuwa utakua ni mchezo wenye presha kutokana na jinsi mzunguko huu ulivyokua kwa klabu ya Simba na namna ambavyo hali ya msimamo wa ligi ilivyo.

Baada ya Simba kupata sare dhidi ya Azam ni wazi kuwa kama bado wana nia ya kushinda ubingwa msimu huu basi leo ni lazima wapate matokeo ya ushindi ili kupunguza tofauti ya alama ili ibaki kama lilivyokuwa baada ya mchezo wao dhidi ya Azam.

Ushindi wa Yanga dhidi ya Tanzania Prisons umeendelea kuongeza tofauti ya alama kati ya Simba na Yanga kutoka saba hadi 10 na hapo ufahamu kuwa Yanga inaongoza Ligi ikiwa na alama 40 wakati Simba ipo nafasi ya tatu kwa alama zake 30 lakini bado ina faida ya michezo miwili nyuma ya Yanga.

Mchezo wa leo wa bado ni mchezo mgumu kwa Mnyama ukilinganisha na msimamo wa Ligi ulivyo lakini pia Benchikha ni kama bado anajitafuta kutengeneza timu ambayo itampa matokeo kwa misimu ijayo.

SOMA ZAIDI: Marefa na washika vibendera mjitathmini. 

Leave A Reply


Exit mobile version