Ilipoishia “Una nini Mke wangu?” Alihoji kwa utaratibu kama siyo yeye aliyemfokea rafiki yake muda mchache uliopita, Sylvia aliketi bila kusema chochote huku ndani yake akiwa kwenye vita kubwa, alijiuliza amweleze Robson kuwa Brahama amerejea Nchini au akae kimya, alijiwazia kwa sekunde kadhaa kabla ya kupata jibu” 

Tuendelee 
SEHEMU YA TATU – 03

“Sikwambii chochote hadi nizungumze na Brahama niusikie msimamo wake juu yangu” Alisema Sylvia ndani ya moyo wake kisha alikunjua tabasamu wakati huo simu yake ikiingia ujumbe, alichungulia akaona ni Mage, pale kwa juu aliusoma ujumbe uliosomeka

“NIMEONGEA NA BRAHAMA AMESEMA KESHO MNAWEZA ONANA” Meseji hiyo iliongeza Bashasha kwa Sylvia ambaye alimtazama Robson

“Ghafla tu umekunjua nafsi yako, umesoma nini?” Aliuliza Robson

“Aaah! Hamna nilikuwa nawasiliana na Fifi ameniambia nikirudi atanipa ofa ya kusuka bure” Alisema Uwongo Sylvia

“Oooh kumbe, sasa ni jambo gani lililokufanya ukawa mnyonge, au kuna Mtu amekukwaza huko sokoni?” Aliuliza Robson, Sylvia alitikisa kichwa kwa ishara ya kukataa kuwa hakuna aliyemkwaza

“Sema ukweli Mke wangu yaani kwa ajili yako nipo tayari kwa lolote lile” Alisema Robson na kumfanya Sylvia atabasamu.

“Ngoja nipike basi” Sylvia aliaga kisha akaelekea jikoni, alimuacha Robson akiwa mwenye furaha sana, alijitanua kochini kama tajiri fulani, aliithamini sana furaha ya Sylvia kuliko chochote kile katika Maisha yake.

Alipofika jikoni Sylvia alimtumia ujumbe Mage kisha simu akaiweka Sailenti ili Robson asisikie chochote kile

SYLVIA: Unasema kweli Mage?

MAGE: Wallah sikuongopei, tulipoachana alinipigia Brahama nikaona ni bora nimweleze

SYLVIA: Alifurahi eeeh?

MAGE: Mtaongea wenyewe Bwana!

Jumbe hizi ziliacha tabasamu zito sana kwa Sylvia.Usiku ulipoingia Brahama alimpigia simu Mage wakapanga kuonana ili wazungumze kuhusu Sylvia, walikutana kwenye Baa moja wakaagiza vinywaji ili wazungumze

“Brahama hivi unajuwa Sylvia anakupenda kufa kabisa?” Alisema Mage akiwa anafungua kinywaji, Brahama alicheka kisha alizungumza

“Kwanini unasema hivyo, angekuwa ananipenda ndiyo angeolewa na Robson. Yaani nyie Wanawake sijui mkoje, nakumbuka Tulipokuwa chuo Siyvia alisema Robson ni rafiki yake tu na hawana mahusiano, kumbe alikuwa ananizuga Mimi” Alisema

Brahama akiwa anagida unywaji

“Hayo ni mawazo yako tu, hebu fikiria umeenda ulaya umekaa bila kumtafuta Sylvia lakini Mtoto wa Watu anakupenda hadi hivi leo tena kachanganikiwa kusikia umerudi Tanzania, na kuhusu Robson kwa jinsi alivyonisimulia ni kuwa walianzisha mahusiano baada ya wewe kumtelekeza”

“Hana lolote si angenisubiria sasa kwanini kaolewa, mbona Mimi sijaowa?”

“Ha!ha!ha! Najuwa unamfikiria Sylvia ndiyo maana hujaowa”

Alisema kwa utani Mage wakiwa wanakula sato aliyekaangwa

“Labda lakini sijui, mimi nilipoondoka sikujuwa kama ningerudi hivyo niliona mapenzi ya mbali siyo mapenzi ya kuyategemea” Alisema Brahama aliyekuwa na nywele nyingi kama Muarabu wa Msiri

“Tuachane na hilo, nimemwambia Sylvia kuwa unahitaji kuonana naye kesho hivyo ujiandae”

“Eeeh yaani wewe mbona unafanya mambo kwa kukurupuka hivyo Mage, yule ni Mke wa Mtu alafu wapo kwenye fungate ujuwe”

“Tatizo lako nini Brahama wakati Mtoto anakuzimia?”

“Mh! Haya Dada wa mipango”

Walizungumza mengi, walikula na kunywa. Usiku ulipokuwa mwingi waliondoka wakiwa wamelewa sana. Brahama alienda kumwacha Mage nyumbani kwake kisha yeye akalekea kwake usiku huo.

Upande wa pili, Fungate iliingia mdudu, Usiku kucha Sylvia alikuwa akifikiria namna itakavyokuwa atakavyoonana na Brahama kwa mara ya kwanza baada ya mwaka kupita, alikesha akiwa anamsikia Robson akikoroma hadi kulipo pambazuka.

“Kesho tunarudi Dar Mke wangu, mchana nitafwatilia tiketi ya ndege” alisena Robson akiwa amejilaza

“Eeh mbona ghafla?” Aliuliza Sylvia

“Kuna mambo ya kufwatilia kazini, hata hivyo Tulienjoi sana Kilimanjaro, huku Mwanza hata sijaona kipya” Alisema Robson, moyoni Sylvia alichukia hakupenda kabisa kuondoka Mwanza tena alitamani hata wangehamia Mwanza kabisa ili awe karibu na Brahama

“Sawa Mume wangu, kama ni hivyo itabidi nifanye maandalizi” alisema Sylvia, Robson alimvuta Sylvia akamlaza kifuani kisha akamwambia

“Wewe ndiyo furaha yangu Sylvia usije ukaenda mbali na Mimi sababu nitakuwa tayari kufanya chochote kile” Alisema Maneno ambayo yalimfanya Sylvia atabasamu tu bila kusema chochote kile.

Mchana ulipofika Robson alimuaga Sylvia kuwa anaenda kushughulia tiketi ya ndege pia kuna baadhi ya vitu akanunue kama zawadi watakaporejea Dar, hakujuwa nyuma yake Sylvia alijiandaa haraka sana akampigia simu Mage kuwa yupo tayari kuonana na Brahama

“Haya uje Kongwa House, ukifika hapo utaona nyumba inauzio wa ukuta mrefu wa bluu” Alisema Mage

“Enhee baada ya hapo?”

“Ndiyo hapo utanikuta”

“Haya powa Mage natoka sasa hivi sababu Robson ameenda kukata tiketi ya ndege ili kesho turudi Dar hivyo ni muhimu nionane na Brahama leo hii” alisistiza Sylvia

“Haya poa” Alijibu Mage kisha Sylvia alikata simu hiyo, haraka alitoka akachukua tax kuelekea alipoelekezwa huku akiwa anawasiliana na Robson kujuwa amefikia wapi

“Ndiyo naelekea ofisi zao” alisema Robson kwa njia simu. Ilimpa amani Sylvia kuwa atawahi kurudi kabla ya Robson kurudi

“Dereva unaweza kutafuta njia ya mkato maana umesema ni mbali na leo ni Jumatatu si kutakuwa na foleni?” Aliuliza Sylvia

“Foleni? Unazungumzia Mwanza hii au Mwanza gani? Hapa siyo Dar Dada yangu….” Alisema dereva huyo ambaye alionekana kujiamini sanaa

“Ha!ha!ha! Sawa ila ni muhimu nifike mapema” Alisistiza Sylvia, dereva wa Tax alimuondoa Sylvia wasiwasi kabisa, kweli Dereva alikanyaga mafuta kwa kasi kuelekea huko alipoambiwa na Sylvia

Walipofika karibu na njia panda iliyogawa barabara tatu, moja ya kuelekea Kongwa House ambapo walikuwa wakienda, walisimamishwa na askari wa Barabarani

“Ooooh yaani hawa askari wa Mwanza” Alisema Dereva akiwa anashuka ili azungumze na askari huyo, muda ulizidi kwenda,

Mage alikuwa akimpigia sana simu Sylvia kuwa mbona hafiki

“Tumekamatwa na askari wa Barabarani hapa njia panda Mage, ila nakuja” Alisema Sylvia kisha alikata simu ya Mage, akawa anaangalia saa na kumwangalia yule dereva aliyekuwa akiongea na polisi, aligundua huwenda wakachukua muda mrefu, alimuita yule dereva

“Samahani Kaka nina haraka sana hivyo naenda” Alisema Sylvia kisha alimpatia yule dereva pesa kidogo ya kumtoa Hotelini hadi hapo waliposimamishwa

“Si ungesubiria kidogo Dada yangu, muda siyo mrefu namalizana na yule askari”

“Hapana nitachelewa”

“Haya sawa!!” Alisema Stlvia kisha alianza kutembea kutafuta Bodaboda, mara simu yake iliita, alijuwa ni Mage ndiye aliyekuwa akimpigia, aliipokea bila hata kuangalia ni Nani aliyekuwa akipiga sababu kilikuwa kisimu kidogo alafu alikuwa barabarani

“Mage nakuja nipo hapa Njia panda, mnisubirie” Alisema Siyvia kisha alikata simu, kumbe aliyekuwa amempigia Sylvia hakuwa Mage bali alikuwa ni Robson, ilimchanganya sana Robson akajiuliza Mke wake anaenda wapi wakati Mwanza wao ni wageni,

Robson alichukua pikipiki bahati nzuri alikuwa ameshamaliza kukata tiketi, alirudi Hotelini huku akipiganisha akili Mke wake ameenda wapi, alimpigia simu lakini Sylvia hakupokea simu ya Robson.

“Mage! Mage! Ni Mage yupi huku Mwanza?” Alijiuliza Robson huku akizunguka sebleni, alipotuliza akili akamkumbuka Mage rafiki yake Brahama ambaye walisoma naye, yeye pekee ndiye aliyekuwa akiishi Mwanza, Sasa akajiuliza

“Ina maana Brahama yupo Tanzania, kwanini amesema mnisubirie kama anaenda kuonana na Mtu mmoja angesema nisubirie na sio mnisubirie, basi itakuwa anaenda kuonana na Brahama” Alijisema Robson, mawazo yake yalienda sawa kabisa na jinsi alivyofikiria

Muda huo Sylvia alikuwa ameshafika Kongwe House, alifuata maelekezo hadi alifika nyumbani anakoishi Brahama, Mage alifungua geti

“Waoooo karibu sana Sylvia” Alisema Mage akiwa anamkubatia

Sylvia, tabasamu zilitanda kwenye nyuso zao

“Asante Mage kumbe unaishi hapa?”

“Hapana hapa ni kwa Brahama”

“Oooh Mungu wangu moyo unanienda mbio Mage” Alisema Sylvia

akionekana mwenye hofu ya kumwona Brahama

“Usijali Sylvia, Brahama yupo ndani anakusubiria wewe tu”

Alisema Mage, basi waliongozana taratibu hadi ndani.

Sylvia alifanikiwa kunwona Brahama kwa mara ya kwanza baada ya Mwaka mmoja wa kutokuwa na mawasiliano naye, mwili wa Sylvia ulitokwa na jasho, jinsi alivyokuwa akimpenda Brahama alijikuta akidondosha chozi, Mage aliondoka ili awaache wawili hao wapate kuzungumza, Brahama alimkumbatia Sylvia ili amtulize maana aligundua Mwanamke huyo alikuwa na furaha sana kuliko hata maelezo.

Nini Kiliendelea? Sylivia atarudi kwa Robson? Itakuaje? Usikose sehemu ya nne

 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

Fungate Sehemu Ya Kwanza 

Fungate Sehemu Ya Pili

 

25 Comments

  1. Pingback: FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04 - Kijiweni

  2. Pingback: FUNGATE (Sehemu Ya Sita) Fungate-06 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version