Ilipoishia “Doa likaingia kwenye ndoa ya Robson na Sylvia huku kila mmoja akifikiria kimpango wake, hakuna aliyetaka kujishusha sababu Sylvia alikuwa akiamini anapendwa sana na Robson hivyo hawezi kufanywa chochote wakati huo Robson akimuona Sulvia ni Msaliti, japo kulikuwa na ahadi kati yao.”

Endelea
SEHEMU YA TANO-05

Haikua utani kwa Brahama, alipomuona Sylvia alianza kumpenda upya kama zamani, tena alijilaumu kwanini aliondoka Tanzania, alijiona mjinga sana. Siku mbili aliishi kwa kumuwaza sana Sylvia, Mage alikataa kutoa namba ya Sylvia kwa kuhofia ataharibu ndoa ya Sylvia na Robson.

Mawazo yalimzonga Brahama, harufu ya huba zito ilimjaa, akamkumbuka sana Sylvia wa Chuo Udom jinsi alivyokuwa na mapenzi moto moto

“Katika vitu ambavyo Mage unaukirihisha moyo wangu ni kukataa kunipa namba ya Sylvia” Alisema Brahama jioni moja wakiwa wanapata chakula

“Sijakataa bali nina hofu na huo ukichaa wako utasababisha matatizo kwenye ndoa ya Watu”

“Matatizo yapi, Mimi nilikuwa wa kwanza kwa Sylvia, Robson amekuja baada yangu, nitakubali vipi kumuachia?”

“Usijitoe ufahamu Brahama, wamefunga ndoa wale, alafu wewe ni Kijana Handsome sana, Wanawake wengi wanakupapalikia, kwanini umg’ang’anie Sylvia?”

“Kwasababu nampenda na ananipenda!”

“Unampenda? Ungemkatia mawasiliano kwa mwaka mzima Brahama?”

Alihoji Mage, wawili hawa walishibana sana, walikuwa wakipeana siri nyingi kama ndugu waliozaliwa pamoja.

“Yalikuwa ni makosa yangu ndiyo maana nimejirudi, kwanini

niukatili moyo wangu!”

“Najuta kwanini nilikwambia kuhusu Sylvia ni bora ningekaaga kimya ikaisha hivyo” Alisema Mage,

Brahama alifanya kila namna kupata namba ya Sylvia ili awasiliane naye wakati huo Sylvia alikuwa akimwambia pia Mage ampatie namba ya Brahama, ukuta uliozuia Wawili hawa kuwasiliana alikuwa ni Mage.

Brahama akamwambia Mage

“Naenda Dar-es-salaam kuhakikisha namchukua Sylvia kutoka kwa Robson”

“Brahama hiyo ni shari tena ni vita isiyo na suluhu, Sylvia ni Mke wa Mtu nakuomba liheshimu hilo” alisema Mage lakini maneno yake yalikuwa ni sawa na machozi ya Samaki

Brahama aliondoka Mwanza kwa ndege hadi Dar-esa-salaam kwa ajili ya Sylvia.

Alfajiri alikuwa akiteremka Uwanja wa Mwalimu Julius nyerere, Licha ya kutembea barani ulaya lakini

alikuwa mgeni katika Jiji hili, alikuwa na mkakati kichwani pake nao ni kumsaka Sylvia kwa udi na uvumba maana Mage alikataa kutoa namba

Akaingia kwenye Tax bila kusema chochote akiwa amevalia koti kubwa lililomkinga na Baridi ya Alfajiri

“Unaenda wapi Boss?” Aliuliza dereva wa Tax

“Hoteli yenye hadhi ya nyota tano” alijibu Brahama

“Hoteli hizo zipo nyingi hapa Mjini Kaka au nikupeleke nzuri zaidi?”

“Itapendeza pia”

Mwendo wa saa moja na nusu walikuwa wameshafika kwenye Hoteli ya Ocean view iliyopo Masaki, ilikuwa ni Hoteli ya nyota tano, kuishi hapo haikuwa shida kwa sababu wazazi wake wanaoishi Ulaya walikuwa wakimtumia pesa nyingi za matumizi akiwa Tanzania

“Samahani unamtambua huyu?” Brahama alitoa picha ya Sylvia akamuonesha dereva wa Tax

“Kaka hili jiji lina kila aina ya Watu, ni ngumu kwangu kumjuwa kila Mtu, kama unantafuta Mtu hapa kwa picha itachukua muda mrefu sana kumpata” alisema dereva, akapatiwa pesa yake kisha Brahama akaingia Hotelini.

Tukiachana na safari ya Brahama kutoka Mwanza hadi Dar, upande wa Sylvia na mume wake Robson hakukuwa na maelewano mazuri, kichwani pa Sylvia alijaa Brahama Mtupu, hata yeye alichizika baada ya kumuona Brahama kule Mwanza.

Siku moja aliwaambia Wazazi wake kuwa

“Mlinilazimisha niolewe na Mwanaume ambaye analala nje ya nyumba yake, Mwanaume ambaye hazungumzi na Mke wake vizuri, sijui ndoa gani ya namna hii?” Alisema Sylvia.

 

Alikuwa ameanza kutengeneza mazingira yake mapema sana sababu alishajuwa ujio wa Brahama una lengo gani hapa Tanzania japo hakujuwa kama Brahama alikuwa Dar.

“Sylvia hupaswi kujilaumu kabisa ndoa ni jambo la baraka,

ulitaka kuolewa na nani?” Alisema Baba yake Sylvia

“Niliwaambia kuhusu Mwanaume niliyempenda lakini hamkutaka kunisikiliza matokeo yake ndiyo haya” Alisema Sylvia

“Tutakaa na Robson tutalizungumza hilo Sylvia” Alihitimisha Baba yake Brahama.

Robson alirudi kwa Mark baada ya kuonana kwa mara ya mwisho ile siku wakiwa wamelewa, bado alikuwa na msongo ambao ulisababisha ashindwe kufanya kazi ipasavyo.

“Mark hali inazidi kuwa mbaya, sylvia analitumia lile tukio la Mimi kulala nje, ananiadhibu kila kona sijui nifanyaje?”

Alisema Robson. Walikuwa wametoka kidogo ili wazungumze, walikuwa ufukwe wa Bahari Beach huku wakitazama namna Watu walivyokuwa wakipiga mbizi na kufurahia Maisha ambayo kwa Robson yalikuwa machungu sana.

“Eeh imefikia hatua hiyo Rob?”

“Hatua mbaya sana, bado nina hisia ile ile kuwa Brahama anawasiliana na Mke wangu, tufanye nini Mark hebu nishauri, nipo tayari kwa lolote” alisema Robson akiwa katika hali ya kuchanganikiwa sana

“Unaonaje tukaenda Mwanza ili tupate uhakika wa tunachofikiria?” Aliuliza Mark, alimpa nafasi Robson

kufikiria mara mbili juu ya kwenda Mwanza

“Sasa Mwanza tunaanzia wapi Mark unajuwa kuwa mbali na Sylvia nahisi kama nitakuwa naharibu kabisa ndugu yangu” alisema Robson katika hali ya kuzidi kuchanganikiwa, alikuwa katika ile hali ambayo hata kama ungempa jiwe angelipokea tu, mapenzi yalimtesa sana Robson

“Si umesema tatizo lilianzia Mwanza si ndiyo?”

“Ndiyo”

“Basi huko Mwanza ndiyo kuna suluhu la hili jambo, tutajua kinagaubaga wa hili tatizo kama ni Brahama au kuna jingine” alisema Mark akionekana wazi yupo pamoja na Robson katika  nyakati hiyo

“Enhee nimekumbuka itabidi nimpigie Richard ili anipe ramani nzima ya kumpata Mage, nafikiri tukimpata Mage tutajuwa kama Brahama yupo Tanzania au bado yupo Ulaya na kama anawasiliana na Mke wangu. Maana najuwa hakuna Mwanaume anayeweza kuchanganya akili ya Sylvia zaidi ya yule Mshenzi” alisema Robson

“Ookaay!! Si unaona Robson, nilikwambia yaani tunalizima hili kitaalam, na kama umafia safari hii tutaufanya” Maneno ya Mark yalimpa tabasamu Robson ambaye alikuwa ameshikilia dafu mkononi, aliangalia saa yake kisha akamwambia Mark.

“Ngoja nirudi nikaandae mazingira ili ikiwezekana kesho kutwa twende Mwanza kwa ndege” Baada ya kauli hiyo waliagana, Mark alibaki hapo Ufukweni akisema anaangalia totozi ya kuiimbisha.

Aliingia kwenye gari yake kisha alikanyaga mafuta kurudi nyumbani, wakati huo Sylvia alikuwa akizungumza na Mage, yaani Sylvia alikuwa akilazimisha apewe namba ya Brahama lakini Mage alikuwa akikazia ila mwisho alimwambia Sylvia

“Siuoni mwisho wa hili jambo ukiwa mzuri Sylvia” Unamaanisha nini? Aliuliza Sylvia akiwa amesimama dirishani ili aweze kuona kama Robson atakuwa anarudi

“Brahama amekuja huko Dar kukutafuta wewe, kwanini msiache mambo ya zamani yakapita Sylvia, umeshaamuwa kuwa na Maisha mengine, namuonea huruma sana Robson” alisema Mage kwa sauti

iliyojaa maistizo ambayo ilimpa umakini wa kuisikiliza Sylvia

“Tatizo siyo kuendelea mbele na Maisha yangu Mage, tatizo ni kwamba moyo wangu hauwezi kufanya maamuzi, najikuta nakuwa upande wa Brahama, na kama amekuja Dar kunitafuta basi ni ishara kuwa hata yeye moyo wake hautulii kwasababu yangu.

Kingine ni kwamba hata Rob anajuwa kuwa nampenda Brahama na tulishaweka ahadi kuwa endapo Brahama atarudi basi nitarudi kwenye maisha ya Brahama” Alisema Sylvia kwa maelezo marefu yaliyomfanya Mage ashushe pumzi

“Mnanivuruga Sylvia, mmekuwa vichaa kisa penzi, unafikiria Robson atatekeleza ahadi kirahisi hivyo, eti akuache Mwanamke amabaye amekuowa mbele za Mungu tena kwa ushahidi wa ndugu wa pande zote mbili?”

“Sitojali kuhusu hilo, ninachokiangalia ni moyo wangu kupata tulizo Mage…”

“Ooooh!! Kwahiyo unataka nifanyaje?” Alihoji Mage…

 

 

“Nipe namba ya Brahama, ni rafiki yako huwezi kumwacha ateseke” Alisema Sylvia. Mage alikata simu bila kutoa jibu lolote lile kuwa anatoa namba au anaendelea kuibania.

Sakata hili lilimpa nyakati ngumu sana Mage, alishaona namna mambo yanavyoweza kuja kuwa mabaya, moyo wake ulizidi kumwambia ni bora aendelee kutokutowa namba ya Brahama kwa Sylvia, hakutaka kuwa shahidi wa kitakachoendelea maana mapenzi yana nguvu kubwa sanaa

Masaa mawili baadaye Robson alifika nyumbani kwake, alimkuta Sylvia akiwa ametulizana, baada ya kuachana na Mark alienda kwanza kazini kuomba likizo ya kuendelea na fungate kwasababu aliikatiza kwa ajili ya kurudi kazini, alikubaliwa.

Kilichobakia kilikuwa ni kumpa taarifa Sylvia ambaye alikuwa amemnunia Robson, kwanza aliketi kisha aliitupa funguo juu ya sofa akamwambia Sylvia

“Hakuna maisha upande wangu bila wewe Sylvia, hakuna thamani bila wewe Mke wangu. Mapenzi yangu yanatoka ndani ya uvungu wa moyo wangu, tafadhali kama kuna mahali nimekosea nisamehe

sipendi kuishi nawe katika hali hii” alisema Robson.

Sylvia alimtazama Robson kisha alinyanyuka na kuingia chumbani, hakumpa jibu lolote Robson kitu ambacho kilizidi kumtia uchungu na wazimu Robson

Akamtumia meseji Mark akamwmabia ajiandae asubuhi waende Mwanza, yalikuwa ni maamuzi yaliyotoka kwa hasira sana, mapenzi aliyonayo kwa Mke wake Sylvia yalimwambia kuwa alistahili kilicho bora zaidi kutoka kwa Sylvia na siyo maumivu.

Akamfuata Mke wake chumbani lakini Sylvia hakutaka hata kumtazama Robson, walilala Mzungu wa nne hadi asubuhi, tena Sylvia alilala na jinzi kabisa kuashiria kuwa hataki hata kuguswa na Robson.

Kulipopambazuka, Robson alichukua baadhi ya nguo akaandika meseji kwa Sylvia ambaye alikuwa amelala akamwambia amepata safari ya kikazi anaenda Dodoma hatochelewa atarudi.

Akamtazama Sylvia huku chozi likimtoka, akalifuta kisha akaondoka nyumbani kwake asubuhi ili kuelekea Mwanza kuutafuta ukweli wa kinachoisumbua ndoa yake changa.

Upande wa Brahama, hakutaka kuendelea kumbembeleza Mage atume namba ya Sylvia sababu aliamini angempata kwa kutumia njia zake, aliweka moyoni upendo wake kwa Sylvia

Asubuhi hiyo alijiandaa kwa ajili ya kumtafuta Sylvia lakini kabla hajatoka alisikia simu yake ikiita kutoka kwenye mfuko wa koti, alipoangalia aliona ni Mage ndiye aliyekuwa akimpigia simu, akatamani kuikata sababu alishambembeleza Sana Mage atoe namba ya Sylvia lakini alikataa, mwisho akaipokea akiwa anafunga mlango wa chumba cha Hoteli

“Mambo Brahama, naona jinsi unavyohangaika, najisikia vibaya sana. Wewe ni rafiki yangu tokea tukiwa wadogo hivyo nakutumia namba ya Sylvia lakini niahidi kuwa hautoharibu ndoa yake” Alisema Mage kwa kutiririka, Brahama alitabasamu akamjibu Mage

“Sawa nimekuelewa” Moja kwa moja simu ilikatika, dakika moja baadaye Simu ya Brahama ikaingia ujumbe mfupi kutoka kwa Mage, ilikuwa ni namba ya Sylvia ndiyo iliyotumwa, Brahama hakuamini macho yake, akajaribu kuipiga.

Mara ya kwanza haikupokelewa sababu bado Sylvia alikuwa amelala, ya pili ndiyo ilimshtua kutoka Usingizini.

“Hello?” ikasikika sauti iliyojaa usingizi ya Sylvia, Brahama hakutaka kusema chochote akakata simu baada ya kujiridhisha kuwa namba hiyo ilikuwa ya Sylvia

Alimtumia meseji Mage akamwabia

“asante sana Rafiki yangu” Brahama hakuona sababu ya kutoka tena, alisubiria hadi muda ambao atahisi Sylvia ameamka, hakutaka kumsumbua Mwanamke aliyempenda sana.

Mambo yanazidi kuwa mazito zaidi. Nini Kitatokea? Robson anamfata Brahama Mwanza wakati tayari yuko mjini Dar Es Salaam. Sylvia anaendeleza vitimbwi zaidi. Ungekua Wewe ungefanyaje? USIKOSE SEHEMU YA SITA

 

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

Fungate Sehemu Ya Kwanza 

Fungate Sehemu Ya Pili

Fungate Sehemu Ya Tatu

FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04

 

 

21 Comments

  1. Aiseee Admin sina cha kueleza🥲story hii inataka kifanana kabisa na mmi na ndoa yangu na bado huyo mtu niliyempenda , akafanya niolewe na mtu mwingine , sahvi amerudi maishani mwangu 🥺moyo unauma kuicha ndoa yangu maana nikimuonaga tu ama kuona simu yake naishiwa nguvu🥲

  2. Daaah!! Ila mwanaum mjinga hupotez Penz lak la kwel kwa mwanamk ampenda kwa dhat alaf baadae akajutia aseeeh😢
    Admin Nataman nion mwish wa hii story coz na me ntajifunz kitu🤔🤔

Leave A Reply


Exit mobile version