Ilipoishia Alimtumia meseji Mage akamwabia”asante sana Rafiki yangu” Brahama hakuona sababu ya kutoka tena, alisubiria hadi muda ambao atahisi Sylvia ameamka, hakutaka kumsumbua Mwanamke aliyempenda sana.

Endelea

SEHEMU YA SITA – 06

Muda huo, Robson na Mark walikuwa wakikutana Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage nyerere, ndege aina ya Boeing ilikuwa ikipakia abiria kuelekea Mwanza.

Miongoni mwa abiria ambao walipanda ndege hiyo walikuwa ni Mark na Robson ambao walikuwa na vibegi vidogo kama Watalii, walichukua siti ya Hadhi ya juu kidogo sababu Maisha yao yalikuwa ya hadhi hiyo, utawaambia nini wasomi wenye kazi nzuri lakini mmoja akiwa anateswa sana na Mapenzi

“Umemwambiaje Sylvia?” aliuliza Mark wakiwa wanakaa vizuri kwenye siti zao

“Hatuzungumzi siku hizi, nimemuandikia meseji tu nimemwambia kuwa nina safari ya kikazi” Alisema Robson akiwa anaweka simu yake Mfukoni

“Ok! punguza mawazo Mtu wangu, Mwanza inaenda kutupa ufumbuzi wa tatizo linalokusumbua, kuwa na amani japo ndoa yako ipo rehani ila tutaishinda hii vita” Alisema Mark ambaye alikuwa ndiye mshenga wa Robson

Dakika chache baadaye walianza kuliaga anga la Jiji la Dar-es-salaam, matairi ya Boeng yalikuwa yakitembea kwa kasi kutafuta spidi nzuri ya kulivamia anga zuri lisilo na mawingu huku kijua kikianza kutoka kuashiria kuwa siku ilikuwa imeanza rasmi.

Mark na Robson waliondoka Dar siku hiyo…

Sylvia alipoamka na kutuliza akili yake alikutana na ile meseji ya Robson kuwa anaenda Dodoma kikazi, hakuijali sana. Alikumbuka kuwa kuna Mtu alimpigia simu akiwa Usingizini, aliitafuta namba na kuipiga akiwa hajui kuwa alikuwa akimpigia Mwanaume aliyekuwa akimnyima Usingizi, simu ilipokelewa na sauti ya Brahama iligonga ngoma za masikio ya Sylvia ambayo yalitamani sana kuisikia sauti hiyo, kwanza alisimama kutoka kitandani alipokuwa amekaa

“Brahama?” Aliuliza Kwa mshangao uliojaa furaha, hakutaka kuyaamini masikio yake

“Naam Sylvia, ni Mimi” alisema Brahama

“Siamini kama nazungumza na wewe Brahama, nimehangaika kuitafuta namba yako, umeweza vipi kuipata yangu?” Aliuliza Sylvia akiwa katika hali ile ile ya furaha iliyoambatana na mshangao Mkuu

“Mage amenipa namba yako, alikueleza kuwa nipo Dar kwa ajili yako?” Sasa hapa ndiyo alizidi kumvuruga Sylvia, alihisi mwili wote unalowa

“Ndiyo alinieleza Brahama” alisema Sylvia akiwa katika hali ya kutaka kulia

“Nimekuja kwa ajili yako Sylvia, nimeshindwa kuhimili upweke wa kuishi mbali na wewe, natamani sana nikae nizungumze mengina wewe” alisema Brahama, Sylvia alishindwa kabisa kuongea, alikuwa akilia sana.

“Sylvia usilie, nimekuja tuongee. Najutia kukuacha ukiwa mpweke, najuwa umeolewa kwasababu uliamini nimepotelea Ulaya na siwezi kurudi tena, niliumiza moyo wako, nimerudi kuupoza”

Kila alivyozidi kuzungumza Brahama alimfanya Sylvia ashindwe kuzungumza chochote.

“Bra….hamaaa…Siamini naona kama ndoto, siamini mama ni kweli nazungumza na wewe. Nilipokuona Mwanza nilitamani kukwambia vingi Brahama, sina hata furaha na ndoa, sikuoelewa kwasababu ya mapenzi na Robson bali sikuwa na chaguo Mimi” alisema Sylvia huku akipiga kwikwi mfululizo

“Nahitaji tuonane leo”

“Wapi?”

“Ocean view Hotel” Alisema Brahama, wakakubaliana waonane hapo Ocean view Hotel ili wazungumze zaidi.

Saa 7 Mchana, Robson na Mark waliingia Jijini Mwanza tayari kuanza kazi ya kumsaka Mage, Robson akampigia Richard wakakutana kwenye Hoteli ambayo walipanga, Richard aliwapa ramani halisi ni wapi anakoishi Mage. Wakachukua tax jioni kuelekea huko

“Nyumba hiyo hapo yenye uzio wa Blue ndipo anapoishi Mage”

Alisema Richard wakiwa ndani ya Tax

“Mpigie muulize yupo wapi” Alisema Mark ambaye alionekana kuwa na haraka sana na Mage, Richard alimpigia simu Mage na kumuuliza yupo wapi, ilitumika namba ngeni ili Mage asije shtuka maana Hawakuwa na ukaribu wa kuulizana yupo wapi

“Nani wewe?” Aliuliza Mage

“Naitwa John tulisomaga wote Udom, nipo Mwanza nikaona nikutafute” alisema uwongo Richard huku akiwakonyeza akina Robson kuona kama Mtego utaenda sawa, ukimya ukawa mwingi

Mage akitafakari sauti ya Richard kisha akasema

“Oooh upo Mwanza sehemu gani, jina siyo ngeni” Wote walishusha pumzi baada ya kuona mambo yanaenda kukaa sawa

“Nyegezi hapa”

“Ooh siyo mbali nipo nyumbani ila nataka kutoka muda siyo mrefu nikitulia tutaongea” Alisema Mage, mara walimuona akifunga mlango wa nyumba, haraka Richard alikatatisha maongezi akamuaga

“Haya tutaongea” Alisema Mage kisha baada ya simu kukatika walimuona akitafakari, kisha alipuuzia akawa anasogea ili kutoka getini.

Tax iliyokuwa nje ya nyumba yake ilimuwazisha Mage, aliitazama kidogo kisha alifunga geti, Tax nyingine ikaja kumchukua.

“Fuatilia ile Tax” alisema Robson, dereva aliondoa gari kwa spidi ya taratibu ili kuifuata tax hiyo ambayo ilionekana kuelekea Mjini.

Umakini ulikuwa wa hali ya juu huku wakifanya utafiti wao ili kubaini kama Brahama yupo Tanzania,”

“Taratibu atashtukia Mzee” Alisema Mark akiwa anampa tahadhari dereva ambaye alikuwa akiifuata Tax kwa karibu zaidi.

Dar Es Salaam
Mishale ya jioni kabisa, Sylvia alimpigia Simu Brahama kuwa yupo tayari kuelekea Ocean view Hotel, alipewa maelekezo maalum, hakuwa na wasiwasi sababu alijuwa Robson yupo Dodoma kwa wakati huo.

Alitumia gari ya Robson akatoka kuelekea Hotelini, mwendo wa saa moja na nusu alikuwa katika maegesho ya magari ya Hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano, moyo wa Sylvia haukutaka kuchelewa hata sekunde moja ili amuone Brahama.

Ilikuwa hivyo hata kwa Brahama ambaye alikuwa na kiu kubwa ya kuwa karibu na Sylvia, alichukua lifti ili kusonga ghorofa ya juu ambako ndiko alipokuwa Brahama.

Chumba namba 404 kilikuwa mbele ya macho yake, harufu ya pafyum ya Brahama ikapenya kwenye pua za Sylvia na kumpa taarifa kuwa Brahama alikuwa hapo, akagonga mlango ambao ulifunguliwa haraka sana kuonesha kuwa Brahama naye alikuwa akimsubiria sana Sylvia, macho yao yaligongana wakatazamana kwa sekunde kadhaa huku wakiwa kwenye hali ya kutafakariana.

Aliyekuwa wa kwanza kumvuta mwenzie alikuwa ni Brahama ambaye alimvuta sylvia na kukutanisha ndimi zao na kuanza kupigana mabusu moto moto.

Walikumbatiana kwa nguvu sanaa kuonesha ile hali kuwa kila mmoja alikuwa akimuwaza sana mwenzie, chozi lilibubujika kwenye macho ya Sylvia. Alimtazama Brahama kwa sekunde kadhaa kisha alishindwa kuzuia hisi zake, kabla ya maongezi yoyote yale, walipeana penzi moto moto la raundi tatu za nguvu kisha baadaye waliporudi kuoga ndiyo walianza kuongea.

“Nilimiss penzi lako tamu Sylvia, nimekumbuka mbali snaa baby” alisema Brahama akiwa tayari amekula penzi la Mke wa Mtu bila kujuwa kuwa Robson alikuwa Mwanza mawindoni na mlengwa kwa wakati huo alikuwa ni Mage ambaye alifahamu hii siri ya mahusiano hayo.

“Hunishindi Mimi mpenzi wangu,,nimekuwa nikikuwaza kila siku za Maisha yangu na nilikuwa tayari kukusubiria hata kama ingechukua miaka kumi, hakuna Mwanaume anayeweza kunipa furaha katika Maisha yangu zaidi yako” alisema Sylvia akiwa kwenye kifua cha Brahama

“Ndiyo maana nimerudi Tanzania Sylvia, nisamehe kwa yote najiona ni mwanaume mpumbavu kufanya jaribio la kutaka kuwa mbali na Mwanamke anayenipenda”

“Hayo si kitu kwangu kwa sasa, kwakuwa uko karibu yangu sina ujanja wowote mbele yako”

“Itakuwaje kwenye hili penzi la siri Sylvia, kila ninapofikiria kuwa ni Mke wa Robson roho yaniuma sana, natamani lirudi lile penzi letu la Udom ambalo hakukuwa nakikwazo cha sisi kuwa pamoja kama sasa ilivyo.”

“Oooh! Hata Mimi nawaza sana, ndoa ya kanisani ni lazima mmoja afe Brahama, istoshe wewe ni Muislam” Alisema Sylvia

“Oooh Shit!!” Alisema Brahama huku simu yake ikiwa inaita, aliangalia aliyekuwa anapiga akaona ni Mage.

“Nani huyo jamani” aliuliza Sylvia

“Mage!!” Alijibu Brahama

“Pokea basi”

“Aah unafikiria atasema nini Bwana”

“Pokea huwezi juwa anataka kukwambia nini” alisema Sylvia

“Sawa!!”

Brahama alipokea simu ya Mage akasikia akisema

“Kuna gari inanifuatilia huku tokea natoka nyumbani hadi jioni hii, inanipa hofu Brahama” alisema Mage

“Kuna gari inakufwatilia?”

“Ndiyo!!! Napata hisia mbaya sababu kuna Mtu amenipigia anasema tumesoma wote, ameniuliza nipo wapi, sasa nilipotoka nyumbani ndiyo nikaona hiyo Tax inanifuata kila niendapo” Alisema Mage kwa sauti ya hofu

“Upo wapi sasa?”

“Nipo Mall hapa nazuga ili nitokee mlango wa nyuma nirudi nyumbani..”

“Mmh!! Sasa ni nani anayeweza kufanya hivyo na kwanini tena” Aliuliza Brahama

“Isije kuwa Robson”

“Robson?….Mmh! Hapana kwani anajuwa mimi nipo Tanzania?”

“Aaah ngoja kwanza nitoke hapa maana naogopa sana” alisema Mage kisha alikata simu

“Nimesikia unamtaja Robson, ni huyu wangu au?” Aliuliza Sylvia, Brahama hakutaka kulipa uzito lakini Sylvia alizidi kutaka kujuwa

“Ndiyo lakini ni mawazo tu aende Mwanza kufanya nini Bwanaa” Alisema Brahama, Mage aliketi kitako akamwambia Brahama

“Robson hayupo Dar tokea asubuhi”

“Ameenda wapi?”

“Yupo Dodoma kikazi”

“Mhhh! Una hakika?”

“Ndiyo”

“Aaah lakini hawezi kuwa Mwanza sababu hajui chochote kuhusu Mimi na wewe si ndiyo?”

“Anaanzia wapi kujuwa wakati simu yangu ina namba za siri ambazo hazijui, istoshe Mimi na yeye tuna ugomvi ambaohauhusu masuala haya Bwana” alisema Sylvia akiwa ameshashusha presha yake akiamini kuwa Robson hajui chochote kile.

Waliendelea kula raha hapo Hotelini, uzuri ni kuwa walikuwa huru hata kulala pamoja sababu Robson aliaga kuwa anaenda Dodoma. Waliyafanya yote waliyokuwa wakiyafanya zamani na hata mambo mapya walioyoyajuwa kuhakikisha tu kuwa wanafurahia siku yao.

Upande wa pili, giza tayari lilikuwa limetanda jijini Mwanza, nyumba ya Mage ilikuwa giza kuanzia ndani hadi nje, Mage alikuwa ndani akisikilizia mapigo yake ya moyo.

Alipochungulia dirisha aliiyona Tax iliyokuwa ikimfwatilia kutwa nzima ikiwa kando ya nyumba yake, akakumbuka jinsi alivyowatoroka pale Mall, ilikuwa hivi…

Alipomaliza kuzungumza na Brahama ile jioni, alilichungulia lile Tax akaona linaegesha kwenye maegesho ya Magari, hakuna aliyeshuka. Aliamuwa kupitia mlango wa nyuma, akakutana na

mlinzi ambaye alimzuia kuutumia mlango huo lakini Mage alimuomba sababu kuna watu waliokuwa wakimfwatilia, Mlinzi alimruhusu ndipo Mage alipowatoroka na kurudi nyumbani kwake.

Alipomaliza kukumbuka aliiyona ile tax ikiondoka pale nje, alishusha presha yake iliyopanda kila wakati, huku akiwa anatafakari ni Nani aliyekuwa akimfwatilia kutwa nzima na alikuwa akitaka nini.

Alipata nguvu ya kumpigia tena Brahama.

“Ondoa hofu Mage huyo Mtu angekuwa anataka kukudhuru angekudhuru muda mwingi, tulipe hili jambo muda ili tuone matokeo yake” Alisema Brahama

“Sawa, lakini nina hofu sanaa na Robson sijui kwanini akili yangu inamuwaza sana” alisema Mage akiwa kitandani, sauti nzito ya Brahama ilimjibu

“Ondoa hofu Bwana, ushajuona umekosea si ndiyo, sasa anaweza vipi kuja Mwanza wakati hajui kama Mimi nipo Tanzania?”

Alisema Brahama, wakazungumza kwa zaidi ya dakika kumi huku Brahama akiwa anambembeleza Sylvia alale, Sylvia naye alikuwa akisikia raha sana kuwa na Brahama sababu alikuwa akijuwa sana mahaba ya namna hiyo ndiyo maana akili yake ilikuwa mgando kwa Mwanaume huyo mwenye asili ya Shombe shombe.

Baadaye akakata simu huku akijitupa ili apate kupumzisha akili yake ambayo siku hiyo ilitawaliwa na hofu kubwa mno.

Asubuhi ya Siku iliyofuata, Sylvia alipokea simu kutoka kwa

Baba yake Robson kuwa Wanamhitaji nyumbani kwao.

“Baby!! Umeamka poa?” Alisalimia Sylvia huku akimwangalia Brahama ambaye alikuwa na usingizi mzito sababu usiku kucha aliutumia kumbembeleza Sylvia

“Ndio Bebe…sijui wewe” alisema Brahama akiwa anapikicha macho yake huku akinyoosha mgongo wake

“Salama pia, naomba nikuache sababu nimepigiwa simu na wazazi wa Robson wananihitaji nyumbani kwao””Mh! Itakuwa wanataka kukwambia nini?”

“Sijui kwakweli ila huwenda ni masuala ya Robson na Mimi, wacha nikawasikilize” alisema Sylivia huku akitabasamu kwa jinsi ambavyo alikua mwenye furaha sana kuwa na Brahama.

“Haya mpenzi uwe makini pia utanijulisha”

“Haya! Mwaaaa..” Sylivia alimpiga busu Brahama kisha alivalia gauni lake huku akisema ndani ya nafsi yake kuwa akifika nyumbani kwake akaoge vizuri.

Akaingia kwenye gari kisha akaondoka hapo kurudi nyumbani kwao, alipofika aliona Kuna Mtu ambaye pengine alikuwa akibisha hodi hapo na alipoona mlango haufunguliwi akawa anaondoka zake, Sylivia alipiga Honi, Mtu huyu alikuwa

Mwanaume na aliyevalia shati lenye nembo ya kampuni ambayo Robson alikuwa akifanya kazi

Akashusha kioo kisha akamsalimia, Mwanaume huyo akasogea dirishani

“Samahani ulikuwa una shida gani?” Aliuliza Sylivia

“Nilikuwa na ripoti ambayo nilitaka kumpa Robson, nimempigia simu hapatikani” alisema

“Ooh sawa nikabidhi Mimi ni Mke wake”

“Sawa hii hapa” Alimkabidhi bahasha ya kaki

“Asante!!”

“Haya, Nawatakia fungate njema” Alisema Jamaa huyo kisha alitabasamu, Sylivia alishtuka kisha akamrudisha

“Umesema Fungate?”

“Ndiyo..si mnaenda kumalizia Fungate leo Mwanza?” Alisema, Sylvia alizidi kushtuka

“Oooh haya asante” alisema Sylvia kisha alimtazama jamaa huyo akiwa anaondoka, akashuka na kufungua geti kisha akaingiza gari ndani, akatulia ndani ya gari akiyatafakari maneno ya yule jamaa kuwa wanaenda kumalizia fungate

“Ina maana Robson yupo Mwanza? Kaenda kufanya nini? Kwanini kaniaga kuwa anaenda Dodoma?” Akafikiria sana, Mara simu yakeikaita, Baba Mkwe wake ndiye aliyekuwa akimpigia, akaipokea haraka sana

“Abee Baba” Alisema Sylivia baada ya kuwa ameshapokea

“Mbona hadi sasa haufiki Mwanangu?” Aliuliza Baba yake Robson

“Baba ndiyo natoka hapa nyumbani nakuja huko samahani kwa kuchelewa”

“Haya jitahidi uwahi” alisema Baba yake Robson kisha akakata simu.

Sylivia akawa na mawazo chungu nzima, kwanza kusikia kuwa Robson yupo Mwanza kulizidi kumpa mawazo akajumlisha na tukio la Mage kufwatiliwa kutwa nzima, kingine kilichompa mawazo sana ni kuitwa na Baba yake Robson, akajiuliza kuna nini?

Akatamani kumueleza Brahama lakini akaona ni bora aende kwanza kwa Baba yake Robson kisha akirudi ndiyo amueleze vyote kwa pamoja.

Akaingia ndani haraka kujiandaaa kisha akaingia tena kwenye gari akanza safari ya kwenda ukweni.

Mwanza

Asubuhi hiyo, Jijini Mwanza…Robson na Mark wakiwa Hotelini walikuwa wakipanga namna ya kuupata huo ukweli Wakajiuliza Mage aliweza vipi kuwatoroka wasimuone, wakaanza kufikiria huwenda Mage ameshtukia kuwa anafwatiliwa

“Cha kufanya hapa ni kwenda kwake na kuzungumza naye, vinginevyo tutatumia siku nyingi bila mafanikio yoyote” Alisema Mark

“Tukienda unafikiria atakubali kusema?”

“Kwanini asiseme?”

“Akikataa je?”

“Anakataaje kwa mfano?” Yalikuwa ni mazungumzo yao ya asubuhi hiyo, wakakubaliana waende moja kwa moja nyumbani kwa Mage ili kumuuliza kama Brahama amerudi japo walijuwa haitokuwa rahisi, wakapata kwanza chai huku wakizidi kupambanua mambo

“Endapo hatotoa jibu alafu akampigia Brahama itakuwaje, unajuwa sitaki Mke wangu ajuwe chochote” Alisema Robson

“Hilo niachie Mimi Robson, Yule Mwanamke atasema tu atake asitake”

Walipomaliza kunywa chai walikodi Tax hadi nyumbani kwa Mage, Wakatumia ukuta kuingilia, kisha Robson akajificha mahali, Mark akagonga mlango. Kelele za kugongwa mlango zilimshtua Mage ambaye alikuwa Usingizni, akajiuliza ni Nani anayegonga mlango wake bila kupitia getini, akajiuliza au aliacha geti wazi ila hakukubaliana na wazo hilo sababu alikumbuka kuwa alifunga milango yote kwasababu ya woga.

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya 07

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

Fungate Sehemu Ya Kwanza 

Fungate Sehemu Ya Pili

Fungate Sehemu Ya Tatu

FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04

 

 

 

24 Comments

  1. Dah hii riwaya n noma yaan silali kutwa kuchungulia page yenu yaan admin akiwa hajaipost nakia na mawazo . Mwanadishi ameweza🔥🔥🔥

  2. Sencha bacsem on

    Ikiwezekana mtoe yote tu tuenjoy maana dah utamu umekata sehemu nadhifu sana dah leta vitu admin

Leave A Reply


Exit mobile version