Ilipoishia “Mambo kama haya ni lazima kwanza niyaelewe ndipo nifanye uamuzi japo nina imani hadi asubuhi kila kitu kitakuwa kimeisha” Alisema Baba yake Robson, waliondoka Usiku huo huo wakafika Mwanza Alfajiri.

Endelea

SEHEMU YA 08

 

Baada ya kuingia Uwanja wa ndege wa Mwanza, Baba Robson akaingia kwenye Tax akaelekea kituo cha polisi ambacho Robson alikuwa ameshikiliwa, kwanza akakumbuka kumpigia Mkuu wa polisi wa Jiji la Mwanza akampa taarifa kuwa Kijana wake anashikiliwa, Mkuu huyo akapiga simu kituo cha polisi ili

Robson aachiwe, hadi Baba yake Robson anafika kituo cha polisi simu ilikuwa imeshapigwa na maelekezo maalum yalikuwa yametolewa, alipofika palikuwa panaanza kupambazuka, akamkuta Robson akiwa ameketi mahali na Mark maana wote waliachiwa kwa pamoja baada ya maelekezo kutolewa.

“Shikamoo Baba” Wote walisalimia kwa pamoja maana walimjuwa Mzee huyo jinsi alivyo mkali

“Hebu kaeni” alisema kisha wote wakaketi ili Robson aeleze kilichotokea hadi wakashikiliwa kituoni hapo

“Hebu nieleze umefikaje huku na kwanini ulikamatwa Robson?” Alihoji akiwa katika hali ya umakini, Robson akamtazama Mark kisha akapewa ishara na Mark kuwa ni bora aeleze kilichotokea. Robson alimsimulia Baba yake kila kitu hadi wao kukamatwa kwa kosa la kumtishia kifo Mage

Robson akajikuta anapigwa kibao cha nguvu na Baba yake, Mark akashtuka sana japo anamjuwa Mzeee huyo kuwa ni mtata lakini hakutegemea kama angelimpiga kibao Robson tena mbele ya askari pale kituoni

“Sijawahi kuona Mtu mdhaifu kama wewe Robson, kulikuwa na sababu gani ya kuomba wakili kwenye mambo ya kipuuzi kama haya?” Alihoji Baba yake Robson

“Lakini Baba….” Mark akataka kusema jambo akakatishwa

“Mark huu upuuzi mnaoufanya, yaani mmetoka Dar hadi Mwanza kisa mapenzi? Robson wewe ni msomi, Baba yako nina hela, kitu gani kinachokutia wazimu wakati una uwezo wa kuwa na yeyote?

Mke gani mpuuzi yule…. Sasa unajuwa alichokifanya huyo Sylivia?”

“Amefanya nini Baba?” Aliuliza Robson

“Amemgonga na gari Baba yake na kumsababishia maumivu hadi sasa yupo Hospitali?” Alisema Baba yake Robson, Robson akashtuka sana akauliza kwa mshangao

“Sylvia amewezaje kufanya hivyo Baba?”

“Hebu turudi Dar sasa hivi yote utayasikia huko, lakini nakwambia ukweli Robson huu ni upumbavu, unanidharirisha Mimi na familia kwa ujumla” Alisema Baba yake Robson kisha alisogea akazungumza machache na Askari aliyekuwa zamu

“Nini kimetokea, Ina maana mambo yamefikia hatua hii?”

Aliuliza Mark, Robson hakujibu chochote huku moyoni akizidi kuumia, alifikiria kufanya hivyo kungeituliza ndoa yake kumbe ndiyo kwanza ndoa inazidi kuparaganyika.Dakika chache Baba Robson akawa amerudi, wakaondoka kuelekea Uwanja wa ndege tayari kurudi Dar.

 

Wazazi wa Sylivia walijaribu kumpigia sana simu Sylvia lakini simu haikuita, ilionesha ilikuwa imezimwa, Mama yake Sylvia ndiye aliyekuwa akihangaika zaidi sababu Baba alikuwa katika hali ya kuuguza jeraha la Mguu, alipiga sana simu bila mafanikio yoyote

“Baba Sylvia, tumekosea katika hili tunapaswa kuwajibika” Akasema Mama Sylvia wakiwa wodini

“Nilisimama Kama Baba, ukasimama kama Mama, huu ni ujinga wake Mke wangu.,Kijana aliyemuowa mbona walikuwa marafiki wazuri sana, kuna nini hapa kati?”

“Baba Sylvia moyo wangu unaniuma sana yaani, sijui hata nifanye nini kwasasa, naomba nikamwangalie Sylivia nyumbanikwake” Akasema Mama Sylvia, alishindwa kuvumilia akiwa kama Mama kwa kile kilichokuwa kinaendelea

“Sawa nitabaki salama” alisema Baba Sylvia japo kwa shingo upande sana, palikuwa pameshapambazuka kabisa, Mama Sylvia akachukua Bajaji hadi nyumbani kwa Robson ili kujuwa kinachoendelea kwa Sylivia.

Geti lilikuwa limefungwa, haikuonekana dalili kuwa Sylvia alilala hapo, Mama Sylvia aliumia sana akakaa hapo maana hata ile nguvu ya kutoka hakuwa nayo, alikaa hapo huku nawazo yakimtafuna, alijiuliza na kujijibu mwenyewe hadi jua lilipokuwa kali, hapakuonekana na dalili ya Sylvia kurejea, akaamuwa kunyanyuka aondoke, Mara aliona Tax ikifika hapo, akashuka Robson na Baba yake….Naaam! Walikuwa wameshafika Dar kutokea Mwanza

“Mama mbona upo nje?” Alihoji Robson

“Nimegonga sana bila mafanikio, nimepiga simu ya Sylvia bila mafanikio pia” Akajibu Mama Sylvia huku akionekana kukata tamaa kabisa, Robson akajipapasa akachukua funguo, akafungua geti kisha akawakaribisha ndani Baba yake na Mama Sylvia

“Hivi ni nini kinaendelea Robson, maana wewe ndiye Mtu wakaribu wa Sylvia” aliuliza Mama yake Sylvia

“Kusema ukweli Mama ukiniuliza kinachoendelea nitashindwakukupa jibu linaloeleweka kwasababu hata Mimi nipo njia panda kwa yanayoendelea” alisema Robson

“Sasa atakua yupo wapi?” Alihoji Mama Sylvia

“Mama ngoja niangalie vizuri” alisema Robson kisha akaingia chumbani, ndipo alipogundua kuwa siyo tu Sylvia hayupo bali hata mabegi yake na nguo zake zote hazipo, Robson akatoka mbio hadi Sebleni

“Kuna nnini?” Akauliza Baba Robson kwa mshangao mkubwa sana

“Baba….Sylvia ameondoka hapa, ameondoa nguo zake zote sijui hata ameenda wapi aaah” alisema Robson huku akiwa amejishika kichwa chake

“Unasemaje?” Aliuliza Baba Robson

“Sylvia ameondoka?” Akadakia Mama Sylvia kuuliza

“Ndiyo Mama hakuna chochote chake humu ameondoka hapa au atakuwa amerudi kwenu?” Aliuliza Robson,,Haraka Mama Sylvia akapiga simu kwa msichana wa kazi, akajibiwa kuwa Sylvia hakwenda huko kabisa

“Oooh Mungu wangu huyu Mtoto sasa ameenda wapi?” Aliuliza Mama Sylvia

“Ukituuliza sisi utakuwa unakosa majibu sababu hakuna anayejuwa alipo Binti yako” alijibu Baba Robson, likawa limeibuka jambo jipya nalo ni kutoweka kwa Sylvia ambaye hakujulikana alikuwa wapi

“Baba….Sylvia anawasiliana na Mtu anaitwa Brahama, hapana shaka wapo pamoja hivi sasa” Aliesema Robson akiwa amechoka, akatua kitini akiwa hoi kabisa, mwili na akili vilichoka kufanya maamuzi, aliumia mno

“Brahama ndiyo Nani?” Aliuliza Baba Robson

“Ndiye Mwanaume anayekisumbua sana kichwa cha Sylvia, ndiye anayeharibu ndoa yangu” Chozi likambubujika Robson

“Ndiyo sababu ya nyie kwenda Mwanza?” Alihoji Baba Robson

“Ndiyo Baba!!”

“Uuupsss!! Hili jipya sasa, au watakuwa wameenda Mwanza?”

Aliuliza Baba Robson, hakuna aliyekuwa na jibu la moja kwa moja kuwa Sylvia alikuwa ameenda wapi na huyo Brahama kama hisia zao zilivyowatuma.

Mama Sylvia akaondoka hapo bila hata kuaga alikuwa amechanganikiwa sana kama ambavyo Robson alikuwa amechanganyikiwa, Baba Robson akamtuliza kijana wake akamwambia

“Popote alipo kama wapo ndani ya Nchi hii, tutawapata. Huyo Brahama ni mshenzi sana” Alisema Baba Robson, alijuwa siyo vizuri Robson akakaa mwenyewe kutokana na kilichotokea, akahofia angeweza kujidhuru, akamchukua akaenda naye nyumbani kwao.

Taarifa ya kutoweka kwa Sylvia ikatikisa vichwani mwa wanafamilia na walioyafahamu mahusiano kati ya Robson na Sylvia, Baba Robson akaenda kutoa taarifa polisi ili wamsaidie kumtafuta Sylvia kila kona ya jiji la Dar-es-salam

“Robson Mwanangu sikujuwa kama una moyo mdogo kiasi hiki, hizi ni changamoto za kawaida sana katika Maisha ya Mwanadamu….naamini atarudi kwako siku moja” Alisema Baba yake Robson wakiwa wameketi kwenye Bustani

“Aah Baba ni ngumu kuamini hivyo kwasababu Brahama ni ufunguo wa moyo wa Sylvia, kabla yangu alikuwa na huyo. Nilifanya jitihada kubwa sana kuhakikisha nakuwa naye lakini mara zote amekuwa Mtu ambaye ananiumiza na kurudisha mawazo yake nyuma” Alisema Robson kwa sauti ya upole sana

“Hakuna kizuri kinachopatikana kirahisi, kama kweli unamhitaji Sylvia ni lazima upambane kuhakikisha anarejea kwako, pigana vita ya kiume” Akasema Baba Robson akiwa anampiga bega Kijana wake

“Nimepigana sana Baba hadi nikamuowa Sylvia, naona naanza kukata tamaa, inakuwa ngumu sana kumrejesha mikononi mwangu….nianzie wapi na sijui alipo Baba” alisema Robson

“Yule Binti wa Mwanza ambaye alitoa taarifa za Sylvia na huyo Kijana anayesumbua akili yake anaweza kuwa ufunguo wa kujua Sylvia yupo wapi” Alisema Baba yake Robson kisha akatabasamu

ili kumtia moyo Mwanaye

“Una maanisha nirudi tena Mwanza?”

“Ndiyo lakini unapaswa kutumia akili zaidi ya nguvu zako, tukijua alipo itakuwa rahisi sana…jiandae urudi Mwanza, Kwa upande wangu nitashirikiana na familia ya Binti kujuwa alipo”

Alisema Baba yake Robson kwa sauti ambayo Robson hakuitegemea kabisa, yaani Baba yke alipoa kabisa kutokana na unyonge ambao Robson alikuwa nao, mara akaingia Mama Robson akiwa amebeba Juisi, akampatia Mwanaye kisha kamtazama kwa sekunde kadhaa alafu akauliza

“Mna mpango gani?”

“Nimemshauri Robson arudi Mwanza kwa yule Binti aliyetoa taarifa Mwanzo, pengine atakuwa anajuwa walipo akina Sylivia kama kweli yupo na huyo Kijana”

“Robson, kuwa makini sana hatuna Mtoto mwingine zaidi yako, Tunakutegemea sana” Aliongezea Mama Robson kisha aliondoka zake, Robson akamtazma Baba yake kwa uchungu sana huku Mzee huyo akimpa ishara ya kumtia moyo Kijana wake.

Sylvia alikuwa zake Hotelini na Brahama wakipanga mpango wa kuondoka Nchini ili wakaishi Maisha ya uhuru zaidi maana waliamini wanatafutwa

“Ni lazima tuondoke Sylvia kama kweli tunataka kuishi Maisha ya uhuru na kufurahia penzi letu, Robson atatutafuta Kila kona ya Nchi hii” Alisema Brahama akiwa anatabasamu mbele ya Sylvia ambaye moyo wake ulikuwa na furaha sana, hakujali maumivu aliyomsababishia Baba yake

“Mimi naona tusikilizie hili jambo kwanza hadi lipoe ndipo tuondoke maana bila kufanya hivi itakuwa vita kubwa, Namjuwa Robson na ukichaa wake” Alisema Sylvia

“Kwahiyo tuendelee kuishi hapa Hotelini?”

“Ndiyo hatuna mahali pengine pa kwenda Mpenzi wangu”

“Haya, usemacho ni sheria Sylvia, siwezi kukupinga kwa lolote lile..”

 

“Lakini namuonea huruma sana Mama yangu, sababu huko alipo atakuwa analia kwa kufikiria kama nipo salama, hajui nilipo lakini najuwa atahuzunika ila atasahau. Wao ndiyo sababu ya Mimi kuolewa na Robson”

“Usijali, Mama yako atakuwa sawa Sylivia” akasema Brahama, Waliamua kuishi hapo ili kuwakwepa akina Robson

Mchana mmoja Robson alimpigia Mark wakapanga kuonana, wakakutana Baa moja iliyopo Mikocheni A, wakaagiza kwanza Bia ili kuondoa uzito mwilini, kisha maongezi yakaanza

“Kilichonifanya nikupigie ni kwa ajili ya kukueleza kuhusu Alichokisema Baba, wakati polisi wanafanya upelelezi wao na sisi tunatakiwa kufanya jitihada binafsi” Alisema Robson kisha akapiga funda la Bia

“Amesemaje?”

“Turudi Mwanza kwa ajili ya kumfuatilia Mage, huwenda anajuwa mahali alipo Brahama, ni lazima atakuwa pamoja na Sylvia

“Si unakumbuka kilichotukuta tukakamatwa na polisi, safari hii tunaenda na mpango gani?”

“Ndiyo maana nimehitaji kuongea nawe Mark ili tupeane Mawazo ya namna ya kuingia Mwanza na kutekeleza jambo letu”

“Kwenda Mwanza siyo tatizo kabisa, ila hofu yangu tunawezarudia kile kile, safari hii itakuwa mbaya zaidi” alisema Mark huku Bia zikizidi kunyweka

“Mimi nina wazo moja, tumteke Mage ili tumlazimishe aseme ni wapi alipo Brahama”

“Unasemaje?” Alihoji kwa mshituko Mark

“Ndiyo…kwasababu bila hivyo itakuwa ndiyo vilevile, nafikiria kwa kufanya hivyo Mage atasema kwa haraka na hatutomwachia hadi tumpate Brahama sababu naamini wanawasiliana” Alisema Robson huku akimwangalia Mark ambaye alikuwa ameduwaa

“Mh! Baba yako analijuwa hili wazo?”

“Hapana na hawezi kukubali hili wazo, ila niamini Mimi itakuwa ni rahisi zaidi kumpata Brahama, unafikiria ni rahisi kumpata kwenye Nchi hii kubwa?”

“Ok sawa! Kama ni hivyo basi ni lazima turudi Dar na Mage hakuna njia nyingine”

“Sawa tutaondoka na Prado ya Mzee ili iwe rahisi kurudi na Mage hapa Dar” Yakawa ndiyo makubaliano warudi Mwanza wamchukue Mage ili aseme ni wapi alipo Brahama.

Wakanywa pombe hadi wakalewa, Mapenzi ni rahisi kuyasikia na kuyaelewa kwa Mtu mwingine ila yanapokukuta ndipo unapokuja kutambua si jambo la kawaida, wivu ukawa umemjaa sana Robson

kila alipofikiria kuwa Brahama yupo na Mke wake, aliporudi kwao alimueleza Baba yake kuwa Mchana wa siku inayofuata watafanya safari kwa kutumia Prado

“Hivi ni akili yako au pombe? Kuna sababu gani ya kutumia gari kwa safari ndefu? Robson kama huna pesa niambie nikupe upande ndege na siyo gari” Alisema Baba yake Robson hukuakiwa anamtazama Mwanaye ambaye alikuwa tungi sana.

“Baba si unanipenda Mwanao, si unanijali na kunithamini? Basi niache niondoke na Prado nina mipango nimeipanga” Akasema Robson akiwa anasinzia kochini, mwisho akalala hapo hapo,

Baba yake alisikitika sana

“Oooh Mapenzi haya, Mwanangu umekuwa kichaa kwasababu ya Mwanamke, upo sahihi sijui unapitia maumivu kiasi gani” alisema

xxx

 

Asubuhi mapema taarifa ambayo ilisambaa kwenye familia zote mbili ni kupatikana kwa Mage ambaye alikuwa akifahamu walipo, pia maamuzi ya Brahama ya kukubali kumrudisha Sylvia

“Mume wangu hizi ni habari njema sana hatimaye Binti yako anarejea” Alisema Mama Sylvia mbele ya Baba Sylvia

“Anarudi kufanya nini hapa? nimekuwa kilema kwasababu yake, sitaki kusikia tena kuhusu Sylvia, tena Mungu angempa laana akafa kifo kibaya sana” Alisema kwa hasira sana Baba Sylvia

“Usiseme hivyo Baba Sylvia, Binti yako amejifunza vya kutosha hupaswi kumwadhibu kiasi hiki” Alisema Mama Sylvia lakini haikubadilisha msimamo wa Baba. Sylvia

Nako upande wa pili, Baba Robson alikuwa ameketi sofani akitafakari taarifa ya kupatikana kwa Mage huku akifikiria maamuzi ya Brahama kuhusu kubadilishana Mage na Sylvia

“Mume wangu kwanini hauna raha?” aliuliza Mke wake akiwa anamuandalia chai.

“Mke wangu, Robson na mapenzi yake kwa huyu Binti yanaweza yakaharibu kabisa Maisha yake, Mimi nina wazo?” alisema kwa sauti iliyojaa umakini wa hali ya Juu sana

“Wazo lipi hilo?”

“Tumuuwe huyu Binti ili asirudi kwenye Maisha ya Robson, sababu kama ataendelea kuwa hai atamsumbua sana Kijana wetu, sasa ni Bora afe ili Robson alie asahau kabisa” Kauli ya Kumuuwa Sylvia ilimtisha sana Mama Sylvia

“Unasemaaje? umeyafanya hayo ukiwa Jeshini kwasasa sitaki utende dhambi za Kinyama Baba Robson, Kumbuka yule Binti ana wazazi wake. Najuwa unataka kumlinda Robson lakini njia hii siyo sahihi” Alisema Mama Robson akiwa anamtazama kwa makini Mume wake anbaye alionekana kudhamiria kutenda tukio hilo

“Hakuna njia nyingine zaidi ya kumpoteza tu, Mark na Robson wapo Barabarani wanarudi, napaswa kuifanya hii kazi. Brahama na Sylvia wapo Ocean View ambako mabadilishano yatafanyika, napaswa kuwahi” Alisema Baba Robson kisha aliingia chumbani akachukua Bastola

“Mume wangu hebu acha hili jambo kuna namna ya kulimaliza bila kuathiri chochote kile”

“Nimesema hakuna njia nyingine, tuna Mtoto mmoja tu Mama Robson alafu tuje kumpoteza kisa mpuuzi ambaye hana msimamo?yule Binti anastahili kifo” alisema kwa hasira sana na kumfanya Mama Robson ashindwe kumzuia Baba Robson, akamuacha akatoka.

Masaa matano yalipita, ndani ya Hoteli ya Ocean view hakukuwa na maelewano mazuri kwa Sylvia na Brahama, Msimamo wa Brahama wa kutaka kuacha kila kitu ulimfanya Sylvia ajawe na hasira sana akawa anamlaumu Brahama

“Hiki ndicho ulichoniahidi na kunitia hasara ya Maisha Brahama?” Alisema Sylvia akiwa mbele ya Brahama

“Sylvia nakupenda lakini siwezi ruhusu kibaya kimkute Mage, ana thamani kubwa ni rafiki wa muda mrefu kwangu” Alisema

“Sasa kama ulijuwa itakuja kuwa hivi kwanini uliniaminisha, kwanini uliniongopea? nakuuliza Brahama nijibu” AliSema kwa hasira sana Sylvia huku chozi likimvuja

“Nimelazimika Sylvia, nimefanya jitihada nyingi za kumficha Mage lakini imeshindikana, ilipofikia hapa hakuna njia nyingine zaidi ya kukubaliana na hali halisi kuwa mpango wetu umefeli. Sikutaka kumaliza namna hii kwanini hautaki kunielelewa?” akalalama Brahama

“Ok sawa!! lakini kaa ukijuwa kuwa nitakuchukia katika Maisha yangu yote endapo hatutoondoka Nchini Brahama, utakuwa adui yangu kuanzia siku ambayo utanikabidhisha kwa Robson”

“Sylvia….Rob ni Mumeo sikupeleki kwa adui yako bali kwa Mtu ambaye amekuowa kwa ndoa…..” Alisema Brahama kisha akaingia Bafuni, akawa anajimwagia maji ili kuondoa hofu iliyokuwa imemtawala.

Muda huo Baba Robson alikuwa ameshafika katika Hoteli hiyo kwa ajili ya Kumuuwa Sylvia kama ambavyo alikuwa amepangilia, hakutaka kujiuliza mara mbili akaisoma meseji ya Robson iliyokuwa inaonesha chumba ambacho Sylvia na Brahama walikuwepo, akapandisha ngazi taratibu akiwa ameficha Bastola yake kiunoni, alitembea akiwa na uhakika sana wa kutekeleza mauwaji hayo

Chumba Namba 404 ndicho ambacho Sylvia na Brahama walikuwepo,

Mzee huyo alifika hadi mbele ya mlango huo, akatafakari kidogo kisha akagonga mlango, Sylvia akashtuka kisha akauliza

“Nani wewe?” Muda huo bado Brahama alikuwa akijimwagia maji hivyo hakusikia kelele za kugongwa kwa mlango wala sauti ya Sylvia, Baba Robson alikaa kimya.

Sylvia akanyanyuka taratibu na kuuelekea Mlangoni ili aangalie ni nani alikuwa akigonga, laiti kama angelijuwa asingeliinuka akaenda mlangoni, Baba yake Robson alitumia maelekezo ya Robson kupajuwa walipo na alikuwa amesimama kuhakikisha anamuuwa Sylvia. Alipofungua mlango kwa kufikiria

huwenda ni Mhudumu wa Hoteli alikutana na sura ya Baba Robson ikiwa kavu sana.

 Nini Kitatokea? Pamotooooo Eeeeh Usikose Sehemu Ya 09

Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezo kijiweni.co.tz unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.

Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hii editor@kijiweni.co.tz  

Fungate Sehemu Ya Kwanza 

Fungate Sehemu Ya Pili

Fungate Sehemu Ya Tatu

FUNGATE (Sehemu Ya Nne) Fungate-04

 

 

 

 

 

38 Comments

  1. Oya mzee sehemu ya 8 ni ya moto sana fanya utawahishie sehemu ya 9 ikiwezekana hadi saa 1 moja usiku iwe tayari

  2. Ni bomba sana 🔥🔥
    Sema admin fanya unaweka muda maalum wa kutuma 🕛
    Pia tunaomba utupe cha tisa leo🙏

  3. Kila siku ninapo soma hiii story napat ujumbe mpya na weny maan na dhamani matika hiii dunia.mwandishi pongezi kwako na Pia ungeendelea na mwendelezo .

Leave A Reply


Exit mobile version