Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili wa funga kazi unatarajiwa kuwa Mei 28 2024 kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Ipo wazi bingwa ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi hesabu ni kwenye tuzo ya kiatu bora na nani atamaliza nafasi ya pili msimu wa 2023/24.

Mechi za mwisho ni maamuzi kwa kuwa tofauti ya Simba na Azam ni kwenye mabao ya kufunga ambapo mtaji wa Azam FC ni kwenye safu ya ushambuliaji yenye mabao mengi na ukuta haujaruhusu mabao mengi.

LICHA ya mashabiki wa Simba kuikatia tamaa timu hiyo kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu na kuinasa tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Azam FC iliyoganda nafasi hiyo kwa muda mrefu, kwa upande wa kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda hajakata tamaa, huku akiwatuliza mashabiki.

Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 kama ilizonazo Azam, ila inazidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, ikizidiwa manane na Wanalambalamba na kesho Jumanne kila moja itakuwa uwanjani kumalizia msimu kwa kucheza mechi dhidi ya JKT Tanzania na Geita Gold zilizopo pabaya.

Hii hapa ratiba ya mzunguko wa pili raundi ya 30 upo namna hii:-

  • Simba dhidi ya JKT Tanzania
  • Geita Gold dhidi ya Azam FC
  • Yanga dhidi ya Tanzania Prisons
  • Namungo dhidi ya Tabora United
  • Coastal Union dhidi ya KMC
  • Ihefu dhidi ya Mtibwa Sugar
  • Singida Fountain Gate dhidi ya Kagera Sugar

Tusisahau pia kuwa kwenye vita ya ufungaji bora wa Ligi Kuu yupo Aziz Ki wa Yanga mwenye mabao 18 pamoja na Feisal Salum wa Azam Fc mwenye magoli 18 pia sasa macho na masikio yote yako kwao huku kwingine ni jinsi ambavyo nafasi ya pili inavyotafutwa kwa udi na uvumba.

SOMA ZAIDI: Kuhusu Aziz KI Msimamo Wangu Ni Huu Hapa

3 Comments

  1. Pingback: Wakilingana Magoli Kanuni Iko Hivi Mfungaji Bora Ligi Kuu

Leave A Reply


Exit mobile version