Karibu sana tutazame uchambuzi na vidokezo vya ubashiri katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza hii leo utakaowakutanisha Fulham dhidi ya Arsenal mchezo utakaopigwa katika dimba la Craven Cottage.

Katika mchezo wa hii leo kwanza kabisa tukitazama msimamo wa ligi kati ya Arsenal na Fulham ni kwamba Arsenal wao wako nafasi ya 4 wakijikusanyia Alama 40 katika mechi 19 ambazo wamecheza mpaka sasa huku Fulham wao wakiwa na alama 21 katika mechi 19 walizocheza huku wakiwa nafasi ya 14.

Katika zile mechi ambazo Arsenal na Fulham wamekutana washika mitutu wa London wanaongoza kwa kuwafunga Fulham lakini pia kukiwa na sare nyingi kati yao lakini pia na idadi ya magoli kuanzia mawili lakini pia kutokea kwa GG.

Katika mechi 5 za mwisho kabla ya kukutana na Arsenal leo klabu ya Fulham imeshinda mechi 2 na kupoteza mechi 3 kwa wastani wa goli 2 kupanda juu wakati klabu ya Arsenal wao katika mechi 5 za mwisho wameshinda mechi 2 na kupoteza mechi 2 na sare 1 ambazo zote hakuna mechi ambayo hawakupata goli.

VIDOKEZO VYA UBASHIRI

Katika mchezo wa leo Fulham ana asilimia 16 ya kushinda kutokana na mwenendo wake wa kusuasua katika ligi huku Arsenal wao wakiwa na asilimia 62 za kushinda mechi hii. Kutokana pia na namna sare zinavyotokea katika mechi dhidi yao kuna asilimia 22 tu.

Unaweza kubashiri kwa njia zifuatazo:

Arsenal Win

Arsenal Win with over 1.5 goals

Kwa wale wanaopenda kubashiri magoli unaweza weka Over 1.5

Kwa wale wasioamini Straight win ya Arsenal wanaweza kuweka Arsenal ashinde au apate sare 2x.

Endelea kufuatilia vidokezo mbalimbali vya ubashiri kwa kusoma hapa.

1 Comment

  1. Pingback: Tottenham vs Bournemouth: Utabiri Na Vidokezo Vya Kubeti - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version