Ukimtazama ni wazi kuwa huwezi kukataa ya kuwa ni mchezaji ambaye ana umbo halisi la mshambualiaji na naweza kusema kuwa Freddy Michael ni usajili mzuri lakini umekutana na changamoto ya presha ya timu kubwa ya klabu ya Simba.

Ameshindwa kuidhibiti presha iliyopo pale katika klabu ya Simba ambayo unaona kabisa ni miongoni mwa zile timu kubwa ambazo ukisajiliwa ni wazi utakua na presha kubwa sana ukiachana na presha ya mechi husika ambayo utakua umepangwa.

Naon ani wazi kuwa presha ndicho kitu cha kwanza kinamtafuna zaidi na kushindwa kufanya vizuri, kuweka mpira wavuni na nafikiri kuwa Abdelhak Benchikha na Daktari wake wa saikolojia wakae na Freddy Michael ili kutatua tatizo lake la kutokuwa na utimamu mzuri anapokua uwanjani, kuna vitu vya kupata kutoka kwa kocha na jitihada za mchezaji kufanya vya kutosha.

Ni mchezaji mzuri anajua kukaa kwenye nafasi nzuri uwanjani lakini pia anakua na changamoto ya umaliziaji pekee huku akiwa na njia nzuri ya kuwa na hatari zaidi kwenye mpira lakini tatizo kubwa zaidi ameshindwa kuimeza na kuidhibiti presha iliyopo pale Msimbazi, ikiwa kinyume yake maana atakuwa tegemeo.

Kuna wachezaji wengi wazuri tu ambao baada ya kusajiliwa katika klabu hizi kubwa za Kariakoo wameonekana kutokua sawa katika viwango vyao lakini wakiondoka huwa wanakua na balaa la maana tun a uzuri mifano ya wachezaji ipo.

Ni wakati sasa kwa mashabiki kumpa moyo zaidi wa kupambana lakini pia na benchi la ufundi kumtaftia mtaalam wa saikolojia ili aweze kumweka sawa kupambana na maisha ya kitanzania ili aweze kuanya vyema katika klabu yake ya Simba.

SOMA ZAIDI: Tunamkosea Heshima GSM Tuuzungumze Ukweli Tu

 

1 Comment

  1. Pingback: Barua Hii Ikufikie Barbara Gonzalenz - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version