Watu wengi bila shaka watakua wanajiuliza maswali mengi kichwani mwao nah ii ni baada ya kutangazwa kwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambacho kinakwenda kushiriki michuano ya FIFA Series nchini Azerbaijan.

FIFA Series 2024 ni michuano mipya ya Shirikisho la soka duniani FIFA ambapo inahusisha mashindano ya timu kutoka mashirikisho tofautitofauti ya soka duniani ambapo hapa kutakua na michezo ya kirafiki kutoka mashirikisho tofauti ya kimabara.

Makala ya kwanza kabisa ya michuano hii inahusisha mfuatano 5 ya michuano ambapo itafanyika katika nchi 4 tofauti ambazo zitakua mwenyeji wa michuano hiyo kuanzia mwezi wa 4 tarehe 18 mpaka tarehe 26.

Michuano hii ilianza kutangazwa rasmi na FIFA kuanzia mwezi wa 12 mwaka 2022 ambapo ilipewa jina la “FIFA World Series” na baadae Rais wa FIFA Gianni Infantino akayatangaza rasmi kuanza kwake mwezi huu wa 3.

TIMU ZITAKAZOSHIRIKI

Series Team Confederation FIFA Rankings
February 2024
[5]
Algeria  Algeria CAF 43
 Andorra UEFA 164
 Bolivia CONMEBOL 86
 South Africa CAF 58
Azerbaijan  Azerbaijan UEFA 113
 Bulgaria UEFA 83
 Mongolia AFC 190
 Tanzania CAF 119
Saudi Arabia A  Cambodia AFC 179
 Cape Verde CAF 65
 Equatorial Guinea CAF 79
 Guyana CONCACAF 157
Saudi Arabia B  Bermuda CONCACAF 171
 Brunei AFC 194
 Guinea CAF 76
 Vanuatu OFC 170
Sri Lanka  Bhutan AFC 184
 Central African Republic CAF 129
 Papua New Guinea OFC 165
 Sri Lanka AFC 204

SOMA ZAIDI: Tuendelee Kuuamini Ukuta Wa Yerikho Simba SC?

1 Comment

  1. Pingback: Yanga vs Geita Gold: Uchambuzi Kiufundi Na Pengo La AUCHO - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version