Baada ya Singida Big Stars kujihakikisha nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa kwa msimu ujao, tayari mabosi wa timu hiyo wako kwenye mazungumzo na kiungo wa KMKM, Khalid Habibu ‘Fei Toto’.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zilieleza kuwa mchezaji huyo amependekezwa na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Hans Van Der Pluijm ili akakichezee kikosi hicho kwa msimu ujao.

“Mazungumzo baina ya mchezaji na viongozi wake yako kwenye hatua nzuri na kilichobaki ni mambo madogo tu, tuna amini sana uwezo alionao na ndio maana tunamuhitaji,” kilisema chanzo hicho.

Kocha Mkuu wa KMKM, Hemed Suleiman ‘Morocco’ akizungumzia jambo hilo alisema nyota huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo hivyo suala la kuondoka kwake na kusaini kwingine hafahamu.

Kwa upande wa Kocha, Pluijm akizungumzia hilo alisema malengo yao kwa sasa ni kumaliza msimu huu kwanza na baada ya hapo atapeleka ripoti kwa viongozi wake kwa ajili ya maandalizi yao yajayo.

Taarifa za awali nyota huyo amewekewa mkataba wa miaka miwili ndani ya Singida huku akisifika kwa uchezaji wake mzuri ambao anafananishwa na mchezaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto‘.

Khalid anaungana na nyota mwingine beki wa kulia, Nicholaus Wadada aliyejiunga pia kwenye kikosi hicho akitokea Ihefu.

Singida Big Stars wamekuwa na mafanikio yao wenyewe na wameonyesha uwezo wao katika mashindano ya ndani ya Tanzania.

 

Leave A Reply


Exit mobile version